STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 18, 2015

Jeshi Nigeria ladai kuua Boko Haram 300

http://d.ibtimes.co.uk/en/full/1418176/nigeria-boko-haram-2000-feared-killed-after-baga-attacked-second-time-days.png
baadhi ya wapiganaji wa Boko haram wakiwa 'kamili' na zana zao
ABUJA, Nigeria
ZAIDI ya wanamgambo 300 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika zoezi la kijeshi huko Kaskazini-Mashariki ya Nigeria, limesema jeshi la Nigeria.
Baadhi ya askari wamekamatwa na silaha kadhaa zimeharibiwa, alisema msemaji wa jeshi hilo, Chris Olukolade.
Pia katika tukio hilo askari wawili walipoteza maisha yao na wengine 10 walijeruhiwa wakati wa zoezi hilo la siku mbili huko katika jimbo la Borno, aliongeza.
Hatahivyo, vifo hivyo havijathibitishwa.
Jeshi la Nigeria lilituhumiwa katika siku zilizopita kuwa limekuwa likitoa taarifa za uongo kuhusu kujeruhiwa kwa maadui.
Boko Haram wamevamia raia huku wakiwaua maelfu wa askari tangu kundi hilo lianzishe vurugu kwa ajili ya kuanzisha taifa lao la kiislamu mwaka 2008.
Nigeria, Chad, Cameroon na Niger hivi karibuni vimeunda jeshi la muungano na kudai kuwa limekuwa likifanya vizuri dhidi ya Boko Haramu.
Tisho la kundi hilo linaelezwa ndiyo sababu ya kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu wa nchini huo uliokuwa ufanyike Jumamosi iliyopita na kupelekwa mbele hadi majuma sita yaani Machi 28.

No comments:

Post a Comment