STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 29, 2012

ZUNGU JIPYA YANGA LAAHIDI KUUA MNYAMA JUMATANO TAIFA

KOCHA MPYA YANGA AJIFUNGA MWAKA YANGA


Kocha mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Upande wa Yanga, uliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga ambaye alishuhudiwa na viongozi wengine wa klabu hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mussa Katabaro, Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako na Majjid Suleiman, mmoja wa watu muhimu kwenye klabu hiyo.
Brandts kulia na Sanga kushoto

Anamwaga wino

Brandts kulia na Sanga kushoto

Brandts na Sanga

Brandts na Sanga

Brandts na Sanga

Brandts na Sanga

Mkutano

Mwalusako akimshuhudia Sanga

Dina Ismail na Vicky Kimaro kazini

Brandts akifafanua jambo, kulia ni Majjid

Katabaro na Mwalusako

Makuburi Ally, pembezi ni wazee wa Yanga wakipiga chabo
CHANZO:BIN ZUBEIRY

Huyu ndiye Hemed Morocco kocha mpya wa Coastal Union

HUYU NDIYE KOCHA MKUU MPYA WA COASTAL UNION, ANAITWA HEMED SULEIMAN 'MOROCCO' NYOTA WA ZAMANI WA KIMATAIFA WA TANZANIA UPANDE WA VISIWANI

TFF YATOA ITC NNE, VODACOM, KLABU ZAMALIZANA  LIGI KUU 



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanne waliokuwa wakichezea timu mbalimbali nchini.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana jijini kuwa, wachezaji hao ni Tony Ndolo aliyejiunga na KCC ya Uganda kutoka Toto Africans, Felix Amech Stanley aliyekwenda Bahla ya Oman kutoka Coastal Union, Ernest Boakye kutoka Yanga aliyejiunga na Tripoli Athletics Club ya Lebanon na Derrick Walulya aliyerejea URA ya Uganda kutoka Simba.
Katika hatua nyingine, Wambura amesema wanamichezo 15 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
Aliwataja waliochukua fomu za kuwania uenyekiti ni Lina Kessy, Isabellah Kapera na Joan Minja. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeombwa na Roseleen Kisiwa pekee wakati Katibu Mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Makafu. Macky Mhango pia ni mwombaji pekee aliyeomba nafasi ya Katibu Msaidizi.
Alisema waombaji watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Furaha Francis, Juliet Mndeme na Zena Chande. Nafasi ya Mhazini nayo ina mwombaji mmoja tu ambaye ni Rose Msamila.
Alisema Sophia Charles, Rahim Maguza, Telephonia Temba na Jasmin Badar Soud wao wanaomba nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho kwenye uchaguzi huo ambao utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Ombeni Zavalla.
Wakati huo huo: Klabu za Ligi Kuu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom zimekutana jana mjini Dar es Salaam.
Wambura amesema mazungumzo yalilenga kipengele ya upekee (exclusivity) kilichopo kwenye mkataba wa udhamini ambacho kitaendelea kuwepo. Klabu zilikuwa zimeomba kwa mdhamini kuangalia uwezekano wa kukiondoa.
Alisema pande hizo zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja kwa ajili ya kuitafutia kila klabu mdhamini binafsi kwa lengo la kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika ligi hiyo na kwamba klabu zote zimeshapata vifaa kutoka kwa Vodacom ukiondoa African Lyon ambayo ilitarajia kuchukua vifaa hivyo leo kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo.
Kuhusu mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA), Wambura alisema unaanza rasmi Septemba 30 mwaka huu kwa uchukuaji fomu kwa wagombea.
Alisema kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, fomu kwa waombaji uongozi zitaanza kutolewa Septemba 30 mwaka huu, na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni Oktoba 4 mwaka huu.
Alisema fomu hizo zinapatikana ofisi za TAFCA zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 alasiri. Ada ya fomu kwa waombaji wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi ni sh. 200,000.
Alisema nafasi zilizobaki za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ada ya fomu ni sh. 100,000. Uchaguzi wa TAFCA umepangwa kufanyika Novemba 10 mwaka huu.

Barnabas asisitiza soka ya vijana

Vincent Barnabas (kulia) katika pambano la Taifa Stars na Msumbiji

WINGA wa timu ya Mtibwa Sugar ya ligi kuu ya Bara, Vincent Barnabas, amesema ili nchi irejeshe makali yake katika soka la kimataifa ni lazima shirikisho la mchezo huo, TFF, na wadau kuwekeza nguvu zao katika maendeleo ya vijana.
Barnabas, alisema mataifa yanayotamba kwenye soka duniani yaliwekeza fedha katika soka la vijana baada ya kuwa na mipango endelevu katika mchezo huo kuanzia ngazi za chini.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum na MJICHARAZO, Barnabas aliyewahi kuwika na timu za Kagera Sugar na Yanga, alisema timu za Tanzania kuanzia za taifa hadi klabu zinafanya vibaya katika michuano ya kimataifa kwa kupuuza soka la vijana.
"Mbali na kupuuza soka la vijana, pia maandalizi duni na kutokuwepo kwa mipango endelevu ya kuinua kandanda katika ngazi zote imekuwa ikiikwaza Tanzania kutamba kimataifa," alisema.
"Lazima tubadilike iwapo tunataka kufika walipo wenzetu."
Alisema nchi imejaliwa vijana wenye vipaji vya soka lakini vinaishia njiani kwa kutoendelezwa, hivyo ni lazima kuwepo na uwekezaji wa kutosha katika soka la vijana ili kuifanya nchi ing'are kama mataifa mengine.
Akizungumzia ligi kuu ya Bara iliyoingia katika mzunguko wa nne sasa alisema, "ni ngumu na haitabiriki.
"Ila kwa aina ya wachezaji tuliopo Mtibwa nadhani msimu huu utakuwa wetu licha ya upinzani toka kwa timu nyingine shiriki."
Mtibwa Sugar iliyomaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya nne, keshokutwa itacheza na Ruvu Shooting ikiwa na kumbukumbu ya kunyukwa bao 1-0 na Azam siku chache baada ya kuisasambua Yanga 3-0 mjini Morogoro.

KARAMA, CHEKA KUONYESHANA KAZI LEO PTA

Bondia  Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Karama Nyilawila  litakalofanyika leo Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.

 Karama Nyilawila akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka litakalofanyika leo Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.


MABONDIA Francis Cheka 'SMG' na Karama Nyilawila 'Captain' leo wanatarajiwa kumaliza ubishi nani mbabe baina yao wakati watakapopanda ulingoni jijini Dar es Salaam kupigana katika pambano linalosaiwa kuwa la kuwania ubingwa wa Mabara wa shirikisho la UBO.
Pambano hilo la uzito wa super middle la raundi 12 lililoandaliwa na kampuni ya Afrika Kabisa chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini, PST, litafanyika kwenye ukumbi wa PTA.
Cheka aliyemshinda kwa pointi Nyilawila katika pambano lao lililopita lililofanyika Februari 28 mwaka huu, ametamba amejiandaa vya kutosha kushinda mchezo huo wa leo ili kulinda heshima yake kwa mashabiki kwa kumpiga mpinzan wake.
Nyilawila amesisitiza rekodi yake ya kutoshindwa mapambano ya ubingwa inamfanya aamini atashinda leo.
"Sijawahi kupigwa kwenye pambano lolote la kuwania ubingwa, hivyo nina imani hata kesho nitaendeleza ubabe kwa kumpiga Cheka na kulipiza kisasi cha kupigwa nae mapema mwaka huu akiwa kwao Morogoro," alisema jana Nyilawila.
Mratibu wa pambano hilo, Robert Ekerege, alisema litasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi na burudani ya bendi ya Mashujaa.
Ekerege aliwataja mabondia watakaopigana katika utangulizi kuwa ni Seba Temba dhidi ya Stan Kessy, Juma Kihiyo atakayepigana na Ibrahim Mahokola, Anthony Mathias atakayechapana na Shaaban Kilumbelumbe na Cosmas Cheka dhidi ya Fadhil Awadh.
Mapambano mengine ya utangulizi ni Husseni Kidebe atakayepigana na Deo Samuel huku Amos Mwamakula akionyeshana kazi na Sadiki Momba.
Michezo yoye hiyo imedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola Kwanza itakayouza soda zake za chupa za plastiki, na Dume Condoms.

AZAM YAIENGUA SIMBA KILELENI, YAILAMBA JKT 3-0


TIMU ya soka ya Azam Fc,  usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nyingine, baada ya kuilaza timu ngumu ya JKT Ruvu 3-0 katika mechi iliyocheza jijini Dar es Salaam.
Azam imeiengua Simba ambayo ndiyo iliyokuwa ikiongoza na leo inatarajiwa nao kushuka dimbani jioni kuumana na Prisons ya Mbeya, baada ya kufikisha jumla ya pointi 10 moja zaidi ya ilizonazo Simba.
Ushindi huo wa pili mfululizo kwa Azam ulipatikana katika mechi kali iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa na na kurushwa 'live' na kituo cha Super Sport kwa mabao yaliyofungwa na nyota wa timu hiyo, John Bocco 'Adebayor' na mapacha toka Ivory Coast, Kipre Tchetche na Kipre Balou.
Kipigo hicho cha jana ni cha tatu mfululizo kwa JKT Ruvu inayonolewa na kocha Charles Kilinda baada ya awali kunyukwa mabao 4-1 na Yanga kabla ya kulazwa mabao 2-1 na Simba katika mechi yao iliyopita.
Katika muendelezo wa Tanzania Soccer Weekend leo jioni mabingwa watetezi Simba watakuwa wakijaribu kurejea kileleni kwa kuikaribisha Prisons ya Mbeya kabla ya kesho watani zao Yanga kuumana na African Lyon na Jumatatu kuwa zamu ya Mtibwa Sugar kupaishwa na Super Sport kwa kuumana na Ruvu Shooting.
Mechi ya mwisho katika mlolongo huo, ni pambano la watani wa jadi Simba na Yanga zinazotarajiwa kuvaana katika mechi yao ya kwanza kwa msimu huu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa siku ya Jumatano.
Mechi hiyo ya watani inayosubiriwa kwa hamu kubwa inatarajiwa kurushwa hewani kuanzia majira ya saa 1;30 usiku siku hiyo ya Oktoba 3.


KOCHA MPYA YANGA AWASILI, KUTAMBULISHWA LEO

 

Brandts wa pili kutoka kulia, akiwa na viongozi wa Yanga. Kulia ni Seif Magari. Kushoto kwake ni Bin Kleb na Majjid


Anapakia mizigo kwenye gari la Bin Kleb

Anazungumza na Waandishi wa Habari

Akiwa na viongozi wa Yanga

Kulia kwake Bin Klerb, kushoto Mwalusako

Anatoka Uwanja wa Ndege



KOCHA mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, anatarajiwa kutambulishwa leo saa 3:00 asubuhi katika Mkutano maalum na Waandishi wa Habari utakaofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, katika Mkutano huo, pamoja na kuelezwa mkataba ambao klabu imeingia na kocha huyo, lakini pia Waandishi watapata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kocha huyo.
Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, aliwasili jana majira ya saa 3:45 usiku katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na ndege ya KLM na kupokewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako na viongozi wengine, Abdallah Ahmad Bin Kleb, Seif Ahmad ‘Magari’ na Majjid Suleiman.
Yanga, imetimiza malengo yake ya kuwa kocha mpya, kabla ya kucheza na wapinzani wao wa jadi, Simba SC, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kumfukuza Mbelgiji, Tom Saintfiet, kutokana na kuwasili kwa Brandts, ambaye ataanza kazi mara moja leo.
Kikosi cha Yanga kipo kambini, hoteli ya Uplands, Changanyikeni, Dar es Salaam na kabla ya kucheza na Simba Jumatano, kesho kitacheza na African Lyon, Uwanja wa Taifa pia.
Mholanzi huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.
Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako ‘riziki’ yake imeisha miezi miwili iliyopita na sasa amepata maisha mapya Yanga.
Akiwa APR, Brandts alifungwa mechi zote mbili na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Mbelgiji Tom Saintfiet katika Kombe la Kagame, moja ya makundi 2-0 na nyingine ya Nusu Fainali 1-0. Yanga iliibuka bingwa, ikiifunga Azam FC 2-0 kwenye fainali.
Brandts atakutana na wachezaji wake wa zamani wawili Yanga, beki Mbuyu Twite anayeanza msimu wa kwanza katika klabu hiyo na kiungo Haruna Niyonzima anayeingia katika msimu wa pili, ambao alifanya nao kazi APR.
CHANZO:BIN ZUBEIRY