STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 3, 2014

Younes Kaboul aikana Arsenal

http://www.myfootballfacts.com/4047.jpg
Beki Younes Kaboul anayevumishiwa kutaka kutimkia kwa mahasimu wao Arsenal
BEKI mahiri wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Younes Kaboul amesisitiza kuwa tetesi za yeye kuhamia Arsenal sio za ukweli kwa asilimia 100. 
Mapema jana gazeti la Daily Star la Uingereza liliripoti kuwa Kaboul amewaambia marafiki zake anataka kujiunga na Arsenal wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. 
Lakini beki huyo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa hana mpango huo kama ilivyoelezwa na gazeti hilo. 
Kaboul anaonekana kujitetea yasije kumkuta yaliyomkuta Sol Campbell mwaka 2001 ambaye alikataa kusaini mkataba mpya na Spurs na badala yake kuichagua Arsenal hatua ambayo ilipelekea kuchukukiwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Nahodha Ngorongoro ahidi ushindi Kenya

http://1.bp.blogspot.com/-vnFsbMFfWIE/Ug-jLjmJ7sI/AAAAAAAAxew/QkAT-OhkRQM/s1600/IMG_0938.JPG
Aishi Manula akiwajibika uwanjani na timu yake ya Azam
NAHODHA wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Aishi Manula amesema wamejipanga kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi dhidi ya Kenya itakayochezwa Jumapili (Aprili 6 mwaka huu) katika mji wa Machakos.
Akizungumza jana (Aprili 2 mwaka huu) kwenye hafla ya kukabidhiwa bendera kwa timu hiyo kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Manula ambaye pia anaidakia timu ya Azam alisema lengo lao ni kufanya vizuri kwenye mechi hiyo.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda akikabidhi bendera hiyo, aliwataka wachezaji hao kujituma na kutanguliza uzalendo mbele bila kusahau kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ushirikiano.
Alisema Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, hivyo waliopata fursa ya kuwemo Ngorongoro Heroes wakati huu wajue kuwa wamepata bahati, na wanatakiwa kufahamu kuwa wao ni wawakilishi wa Tanzania, na Watanzania wana kiu ya kusikia matokeo ya mechi hiyo.
Ngorongoro Heroes inayofundishwa na John Simkoko inaondoka kesho (Aprili 3 mwaka huu) saa 4.30 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways, na mara baada ya kuwasili itakwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya Garden iliyopo Machakos ambayo ndiyo imepangiwa kufikia na Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF).
Wachezaji waliopo kwenye msafara huo unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF), Ayoub Nyenzi ni Abrahman Mohamed, Aishi Manula, Ally Idd, Ally Mwale, Athanas Mdamu, Ayoub Semtawa, Bryson Raphael na Edward Manyama.
Wengine ni Gadiel Michael, Hamad Juma, Hassan Mbande, Ibrahim Ahmada, Idd Ally, Kelvin Friday, Michael Mpesa, Mohamed Ibrahim, Mudhathir Yahya, Pato Ngonyani, Peter Manyika na Salum Mineli.

Taribo West aitabiria Nigeria kuizima Argentina

http://deeksobserver.com/wp-content/uploads/2013/02/taribo.jpg
Taribo West enzi akiichezea Nigeria
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Nigeria,Taribo West, ameitabiria timu ya taifa ya Nigeria Green Eagles kuwa itapata ushindi dhidi ya Argentina.
Tai hao wa Kijani watacheza mechi hiyo dhidi ya Albiceleste huko Brazil wakati wa Kiangazi katika michuano ya kombe la Dunia. 
Nyota huyo wa zamani, anasema kwa sasa siyo tu kuwafunga bali kusonga mbele huko Rio 2014 katika Fainali hizo za Dunia .
“Kama tumefungwa mara mbili lazima tuwe na aibu ,Nina aamini tumejifunza kutokana na uzoefu. Mara mwisho tulicheza na  Argentina  2010 katika Kombe la Dunia Afrika Kusini." alisema na kuongeza;
"Hata benchi lote linaelewa hali iliyo, mechi dhidi ya Argentina wakati huu itakuwa Bora Kwetu itakuwa Bora ,” West aliuambia mtandao Goal.
Nigeria wamekuwa hawana bahati dhidi  Albiceleste Tumeshindwa katika safari tatu za Kombe la Dunia  1994, 2002 na 2010. 
Lakini West anaamini kuwa timu yake itafanya vizuri huko  Brazil.