STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 2, 2013

Unyama! Mwanamke abakwa, alawitiwa hadi kufa

Kamanda wa Polisi wa Kilimanjaro, Robert Boaz
WATU wasiojulikana, walimvamia mwanamke mmoja wa kijiji cha Mrimbo Uuwo, Mwika mkoani  Kilimanjaro nyumbani kwake wakambaka na kumlawiti hadi kupoteza maisha.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho, Elizabert Mkonyi, alisema mama huyo alivamiwa juzi saa 3 usiku na kufanyiwa unyama huo na baadaye kufungwa mikono na miguu.

Alisema, mama huyo alikutwa ndani kwake akiwa amefanyiwa unyama huo, huku chakula chake cha jioni kikiwa mezani na watu huo kutokomea na magodoro mawili.
“Tulitoa taarifa kwa jeshi la polisi na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Kilema,” alisema Mkonyi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alipoulizwa kuhusu kutokea kwa tukio hilo, hakupatikana na alipotafutwa kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu yake ya kiganjani alijibu: "Nina dharura nitakutafuta."

CHANZO: NIPASHE