STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 4, 2012

Bwana Misosi avunja ukimya na mpya

Bwana Misosi katika pozi

STAA wa kitambo wa muziki wa Bongofleva, ambaye kwa sasa amejitosa kwenye fani ya filamu, Joseph Rushahu 'Bwana Misosi', amevunja ukimya kwa kuachia wimbo mpya uitwao 'Iweje'.
Wimbo huo umefyatuliwa na Bwana Misosi, baada ya kipindi kirefu cha ukimya tangu mwaka jana alipoachia nyimbo mbili za 'Pilato na Game' alioimba na Sir Juma Nature na Fid Q na ule wa 'Mungu Yupo Bize'alioimba na Said Chigunda 'Chegge'.
Akizungumza na MICHARAZO, Bwana Misosi, alisema wimbo huo mpya ameurekodia studio za HM Records zilizopo Kawe na anatarajiwa kuachia hivi karibuni sambamba na video yake aliyoanza kuishuti.
"Kaka nimekamilisha 'ngoma' mpya iitwayo 'Iweje' ambayo nimekamua mwenyewe bila kupigwa tafu na mtu na kwa sasa nakamilisha mipango ya video kabla ya kuachia kwa pamoja itakapokamilika video hiyo," alisema Bwana Misosi.
Msanii huyo alisema wimbo huo kama zilizotanguliwa zitakuwa za kufanyia show tu na wala hana mpango wa kutoa albamu kama alivyofanya mwaka 2004 na 2007.
"Sina mpango wa kutoa albamu, natoa singo tu kuwapa burudani mashabiki wangu sawia na kupata nafasi ya kugonga shoo," alisema.
Aliongeza wakati akiendelea na mchakato wa kupakua video ya wimbo huo wa 'Iweje', pia anaendelea na zoezi la upigaji picha wa filamu mpya ya pili anayotarajiwa kuibuka nayo.
Bwana Misosi , aliyeingia kwenye fani hiyo akiwa na filamu ya 'Mkoba' ambayo ipo njiani kuachiwa mtaani ikiwa imeshirikisha wakali kama Amanda na Mzee Majuto, alisema filamu hiyo mpya ya pili ipo hatua ya mwisho kabla ya kukamilika.

Zuku Tv yazindua huduma mpya ya malipo kwa wateja wao

Meneja wa kampuni ya Wananchi Satellite Ltd, Fadhil Mwasyeba (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma za malipo kwa wateja wao uliofanyika leos asubuhi jiji Dar es Salaam baada ya kampuni hiyo kuingia mkataba na kampuni ya Selcom Wireless Ltd. Anayeonekana kati ni Meneja Uhusiano wa Selcom, Juma Tumaini Mgori.KAMPUNI ya Wananchi Satellite Ltd inayomiliki televisheni ya kulipia ya Zuku kikishirikiana na kampuni ya Selcom Wireless Ltd zimeingia mkataba wa kuanza kutoa huduma rahisi ya malipo kwa wateja wa televisheni hiyo kwa nchi nzima.
Uzinduzi wa huduma hizo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa pande hizo mbili kusaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond, uliopo  Ubungo.
Meneja wa Wananchi Satellite kwa hapa nchini, Fadhili Mwasyeba alisema wameamua kurahisisha huduma ili kuwapa fursa wateja wao kufanya malipo kwa njia nyepesi na ya haraka tofauti na siku za nyuma.
"Tuna furaha juu ya ushirikiano huo mpya na utakaowajali wateja wetu wa Zuku. Ahadi yetu ni kutoa ufumbuzi rahisi kwa wateja wetu wafanyabiashara na wauzaji na ufumbuzi huui utatuwezesha kufika mbali zaidi ya matarajio ya vwateja wetu." alisema.
Aidha Mwasyeba aliongeza kuwa wakati wakiwarahisishia unafuu wa kulipa malipo ya kila mwezi kwa wateja wao, pia kampuni yao inaendelea na promosheni yao ya kuwazawadia wateja wao iitwayo Zuku Tunakuthamini-Pata Tv Bure'.
Alisema kinachotakiwa kwa wateja kuwaunganisha wateja watano kujiunga na Zuku na kulipia malipo na kisha kujishindia runinga kati ya inchi 22 na wale watakaofikisha idadi ya wateja 10 watanyakua rungina ya inchi 42 na walioungwanishwa nao wakiambulia 'offer' nyingine zinazotolewa na kampuni yao kupitia promosheni hiyo.
Naye Meneja Uhusiano wa Selcom, Juma Tumaini Mgori, alisema kuanza kutoa huduma hiyo kwa wateja wa zuku ni fursa ya kuwapa unafuu wateja wa televisheni hiyo popote walipo nchini kutokana na kampuni yao kuwa na vituo vya malipo zaidi ya 1500.
"Tunajitahidi kufanya kazi kwa ufanisi kwa malipo ya ushirikiano wa kipekee na zuku ili kuwafikia wateja kwa ukaribu zaidi," alisema na kuongeza;
Tuna furaha kufanya kazi na Zuku na tunaamini huu ni mwanzo tu wa ushirikiano wa kibiashara," alisema.
Televisheni ya Zuku inatoa uchaguziu mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja na habari, michezo na sinema, majarida na muziki ikiwa imejumuisha chaneli za kimataifa kama BBC, MTV Base. Sentanta Sports, MGM Movies na nyinginezo ka gharama nafuu kwa ubora na kiwango cha hali ya juu.
Mameneja wa kampuni za Wananchi Satellite Ltd, Fadhil Mwasyeba (kushoto) na Juma Tumaini Mgori wa Selcom Wireless wakibadilishana mkataba waliosaini leo ili kutoa huduma rahisi na ya haraka ya malipo kwa wateja wa Zuku Tv. Uzinduzi huo uliofanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

PICHA ZA TIMU ZA TAIFA ZA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZILIZOPOWEZA KUTINGA NUSU FAINALI ZA KLOMBE LA CHALENJI NCHINI UGANDA. (zote kwa hisani wa Bongostaz

Wachezaji wa Bara wakimpongeza Bocco baada ya kufunga bao la pili katika Robo Fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Rwanda. Bocco alishangilia huku akichechemea baada ya kufunfa bao hilo kutokana na kuumia, baada ya kugongwa na kipa wa Rwanda, Jean Claude Ndoli wakati anaenda kufunga. Bara ilishinda 2-0 na kutinga Nusu Fainali. 


Kaseja amedaka, huku Yondan akiwa tayari kumsaidia


Manahidha wakisalimiana kabla ya mechi, Juma Kaseja wa Bara kulia na Haruna Niyonzima wa Rwanda kushoto


Kikosi cha Rwanda leo


Kikosi cha Bara leo


Watanzania waliokuja kuisapoti timu hapa


Shomary Kapombe akimdhibiti Dadi Birori 


Athumani Iddi 'Chuji' akiruka juu kulia kuokoa


Amri Kiemba anamkokota mchezaji wa Rwanda


Kocha Milutin Sredojevic 'Micho'


John Bocco akiwashughulisha mabeki wa Rwanda


Refa anaonyesha kati, baada ya Kiemba anayekimbia nyuma yake kufunga bao la kwanza


Bao la Kiemba


Mwinyi Kazimoto kulia akimburuza mchezaji wa Rwanda


Ulinzi mkali langoni mwa Rwanda, lakini bado mbili zilipenya


Bocco anasababisha


Jean Claude Ndoli wa Rwanda aliyeruka hewani kudaka moja ya michomo ya hatari iliyoelekezwa langoni mwake