STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 14, 2013

Man City yainyoa Chelsea na kuifuata Wigan fainali FA Cup

Kun Aguero aliyeifungia Man City bao la pili

Vincent Kampany akichuana na Torres

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City muda mfupi uliopita imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la FA baada ya kuinyuka Chelsea kwa mabao 2-1 na kuifuata Wigan Athletic iliyotangulia katika hatua hiyoi tangu jana.
Chelsea ilijikuta ikienda mapumziko katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Wembley, Londoni ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lililofungwa na Samir Nasir katika dakika ya 35.
Sergio kun Aguero aliiandikia Manchester City bao la pili dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili na kuifanya timu yake katika mchezo huo wa nusu fainali kucheza kwa kujiamini zaidi.
Demba Ba, alifutia machozi Chelsea kwa kutumbukiza bao pekee ambalo halikuwasaidia kitu katika dakika ya 66 na kufanya hjadi dakika ya mwisho Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kusubiri pambano la fainali dhidi yake na Wigan iliyoing'oa Milwall jana kwa mabao 2-0.

SIMBA, AZAM HAKUNA MBABE, YANGA YAPUMUA KILELENI

 Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa akichuana na beki wa Azam FC, John David katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilifunga mabao 2-2 (Picha na Habari Mseto Blog)  
 Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Azam FC, Joockins Atudo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu  Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kuapata bao la pili.
Kiungo wa timu ya Simba, Abdallah Seseme akiwatoka wachezaji wa Azam FC, Himid Mao (kulia) na Salum Abubakar wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2.

LICHA ya tambo nyingi kabla ya pambano lao timu za Simba na Azam jioni ya leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na kuwafanya vinawa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupumua.
Yanga mabo mashabiki wake leo walionyesha kioja kwa kuwashangilia watani zao Simba dhidi ya Azam, wanapumua kwa vile Azam inayowafukuza kwenye mbio za ubingwa imepunguza pengo la pointi moja tu na kuipa nafasi Yanga kuhitaji pointi tano tu kati ya mechi zake nne zilizosalia kutangaza ubingwa msimu huu.
Yanga yenyewe ina pointi 52 wakati Azam waliopo nafasi ya pili wana pointi 47, huku kjwa sare hiyo ya leo Simba imeendelea kusalia kwenye nafasi ya nne akiwa na pointi 36.
Ramadhani Singano 'Messi' ndiye aliyeipa Simba uongozi wa mabao katika pambano hilo lililochezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga kwa kufunga mabao mawili katika dakika ya 10 na 14 akimalizia kazi murua iliyofanywa kwa ushirikiano wa Mrisho Ngassa na Haruna Changono.
Dakika ya 29 Kipre Tchetche aliifungia Azam bao la kwanza baada ya Khamis Mcha kuangushwa akielekea kumsalimia kipa Abel Dhaira na kumfanya afikishe bao la 15 msimu huu.
Dakika mbili baadaye kocha wa Azam, Stewart Hall alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kutokana na maamuzi yake na hadi mapumziko matokeo yalikuwa mabo 2-1.
Kipindi cha pili Azam walionyesha uhai zaidi kwa kushambulia lango la Simba na kufanikiwa kupata bao la pili na la kusawazisha dakika ya 72 kupitia kwa Humphrey Mieno.
Kwa matokeo ya pambano hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kutokana na tambo zilizokuwa zikitolewa na pande zote mbili na mkasa ulioibuka baada ya mechi yao ya kwanza ambapo Simba walishinda mabao 3-1 na kupelekea Azam kusimamisha wachezaji wake wanne kwa tuhuma za rushwa, msimamo upo hivi;


                                       P     W     D     L     F     A     D     PTS
    1.  Young Africans       22    16     4     2    40    12    28    52
    2. Azam                      23    14     5     4    41    19    22    47    
    3 . Kagera Sugar         22    10     7     5    25    18    7      37     
    4.  Simba                     22     9     9     4     32    21    11    36
    5.  Mtibwa Sugar         23     8     9     6     26    24     2     33   
    6. Coastal Union          22     8     8     6     23    20     3     32    
    7.  Ruvu Shooting         23     8     6     9     21    22    -1    30     
    8.  JKT Oljoro FC       23     7     7     9     22     27    -5    28     
    9. Tanzania Prisons       24     6     8    10    14     21    -7    26    
    10.JKT Mgambo         22     7     3     12    14     22    -8    24
    11.Ruvu Stars              21     6     4     11     19     34   -15   22
    12. Toto Africans         24     4    10    10     22     32   -10   22
    13. Polisi Morogoro     23     3    10    10     11     21    -10  19    
    14.  African Lyon         23     5     4     14     16     35    -19  19

WAWILI WAFA KATIKA AJALI KAGERA


 

Magari yaliyohusika na ajali hiyo iliyotokea jana jioni huko Ngara, Kagera

Watu wawili wamefariki dunia  papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari aina ya Mercedec benz lenye namba ya usajili T 908 ABZ semitrailer lililokuwa ikitokea nchini Burundi, kuacha njia leo(April 13,2013) muda wa saa 12 jioni na kupinduka katika eneo la Kumuyange nje kidogo ya mji wa Ngara mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi wilaya ya Ngara  Abel Mtagwa amewataja watu hao waliofarki katika ajali hiyo kuwa ni Edward Filimon alie kuwa akiendesha pikipiki yake yenye namba za usajiri T 756 BZJ na abiria wake ambae hadi sasa haja fahamika jina lake.
Kamanda Mtagwa amewataja majeruhi wa ajari hiyo kuwa ni Dereva wa gari hilo Hajji Omary Ibrahim(29) mkazi wa gongolamboto jijini Dar es salaam na tingo wake aliyejulikana kwa jina la Kambi simba(40).
Kamanda Mtagwa ameongeza kuwa katika ajal i hiyo nyumba moja mali ya Bi.Bibiana John (58) imegongwa na gari hilo na kuharibika.
Aidha Kamanda Mtagwa amesema kuwa chanzo cha ajari hiyo ni  gari hilo kufeli  mfumo wa Breki  jambo ambalo Dereva wake alishindwa kulimudu kuliendesha ndipo lilipanda mtaro na kubomoa nyumba hiyo. 
 
Aidha Majeruhi wa Ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Murugwanza wilayani Ngara.
 
CHANZO:MWANA AFRIKA

Simba, Azam. ni vita ya kisasi leo taifa

Simba

Azam

SIMBA na Azam jioni ya leo wanatarajiwa kushuka dimbani kumenyana katika pambano pekee la Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni huku, ambalo limetabiriwa na wengi kama vita ya kisasi baina ya timu hizo.
Timu hizo zitakutana kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kila moja ikiwa na malengo tofauti, Azam kulipa kisasi ya kipigo cha mabao 3-1 ilichopewa kwenye pambano lao la kwanza lililosababisha iwasimamishe wachezaji wake wanne kwa tuhuma za kuihujumu kupitia rushwa.
Simba wenyewe wakaikabilia Azam wakiwa na hasira za kutuhumia na rushwa sakata ambalo lilimalizwa nna Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuibuka ikitaka kulipwa fidia ya Bilioni 1 kwa tuhuma hizo nzzito.
Pia Simba inashuka uwanja wa Taifa ikiwa inataka kulinda heshima yake katika ligi ya msimu huu kutokana nna ukweli imeshatemeshwa ubingwa na ipo hatua chachee kukosa hata nafasi ya uwakilishi wa nchi katika michuano ya Kimataifa mwakani.
Tayari kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' ametamka wazi kwamba wanashuka dimbani leo kwa lengo moja tu la kutaka kulinda heshima yao mbele ya Azam na pia kuhakikisha wanamaliza ligi wakiwa katika nafasi nzuri baada ya kutemeshwa taji.
Azam mbali na kuhitaji kulipa kisasi kwa Simba ikiamini kwamba mechi ya kwanza walifungwa kwa hila, lakini pia inasaka ushindi ili kuifukuzia Yanga kileleni ambayo jana ilitakata kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya maafande wa JKT Oljoro na kuzidi kujichimbia kwenye nafasi ya kwanza.
Yanga mbali na kuendelea kuongoza na kuongeza pendo la pointi dhidi yake na Azam, pia imejihakikisha nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika mwakani mpaka sasa kati ya nafasi mbili za uwakilishi wa nchi.
Kwa kuangalia mazingira hayo, huku Azam wakijinafasi kwamba kiu yao ni kutwaa ubingwa msimu huu na kuweka rekodi, ni wazi pambano la jioni litakuwa ni patashika nguo kuchanika.
Wachezaji wanne waliohusishwa na tuhuma za rushwa baada ya pambano hilo la duru la kwanza, nahodha wa zamani Aggrey Morris, Said Morad, Erasto Nyoni na kipa Deo Munishi 'Dida' tayari wameripoti kambini katika kikosi cha timu hiyo wakielezwa wanaweza kushuka dimbani leo kuwakabili 'Mnyama'.
Hata hivyo kwa mazingira yalivyo huenda ikawa vigumu kwa wachezaji hao kucheza pambano hilo ikizingatiwa kwamba ni Simba hao hao waliowaponza hata kuingia matatani kabla ya kusafishwa na TAKUKURU.
Mashabiki wa soka watakuwa na hamu kubwa ya kuona kipi kitakachotokea katika mechi hiyo baada ya dakika 90 huku macho na masikio yakielekezwa kwa washambuliaji nyota wa Azam, Kipre Tchetche na John Bocco 'Adebayor'.
Tchetche anaangaliwa kutokana na kasi yake ya ufungaji mabao akifunga karibu kila mechi tangu arejee dimbani katika duru la pili, huku Adebayor kwa bahati yake ya kuitungia Simba kila timu hizo zinapokutana.
Bila shaka kujua nani atakayecheza ua kulia leo taifa ni suala la kusubiri kuona baada ya dakika 90 za pambano hilo la kusisimua.

MIUJIZA:ABIRIA ZAIDI YA 100 WANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE

  
ZAIDI ya abiria 100 wamenusurika kimiujiza katika ajali ya ndege iliyoanguka muda mfupi baada ya kuruka hewani kando ya pwani ya bali, nchini Indonesia.
Mashuhuda wa tukio hilo lililoikumba ndege ya Lion Jet iliyoanguka ikitoka kuruka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Ngurah Rai nje kidogo ya mji wa Denparsar walisema walisema manusura wa ajali hiyo walionekana kuhamanika wakati wakiokolewa kutoka kwenye ndege hiyo iliyozama baharini kwa futi kadhaa.
Inaelezwa ndege hiyo ilikuwa imebebea jumla ya abiria 101 na watumishi wapatao saba wakati ikianguka majini kutoka umbalio wa Mita 50 juu.