STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 14, 2014

Argentina yaiangamiza Hong Kong, Messi aanzia benchi

International friendlies - Argentina stroll to seven-goal victory over Hong Kong
Wachezaji wa Argentina wakipongeza kwa kuinyoa Hong Kong mabao 7-0
ARGENTINA iliyotoka kukung'utwa mabao 2-0 na Brazil mwishoni mwa wiki nchini China, leo imezinduka kwenye mechi zake za kirafiki za kimataifa baada ya kuinyoa Hong Kong mabao 7-0.
Ever Banega alianza kuiandika wageni bao dakika ya 19 kabla Gonzalo Higuan kuongeza la pili katika dakika 42 kwa pasi ya Vangioni na Nicolas Gaitan kuongeza la tatu sekunde chache kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Higuan alikianza kwa kuongeza bao la tatu dakika ya 54 akimalizia kazi ya Gaitan na baada ya Messi kuingia dimbani aliongeza bao la tano dakika ya 66 kwa kazi nzuri ya Banega.
Gaitan hakutosheka kwa kufunga bao jingine lililokuwa la sita kwa Wanafainali hao wa Kombe la Dunia kwenye dakika ya 72 na Messi kuongeza bao la mwisho  dakika sita kabla a filimbi ya mwisho.

Neymar 4 Japan 0, China yaigonga Paraguay, Costa Rica ikiiua Korea

International friendlies - Four-goal Neymar destroys Japan to reach 40 for Brazil
Akishangilia bao lake la tatu
Neymar célèbre sa prestation exceptionnelle avec le Brésil contre le Japon
Neymar akishangilia moja ya mabao yake mchana huu wakati wanaizamisha Japan kwa mabao 4-0
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Neymar amethibitisha kuwa yeye ndiye kila kitu Brazil baada ya kuifungia timu yake mabao manne wakati timu yake ya taifa ikiiadhibu Japan katika mechi ya kurafiki ya kimataifa.
Neymar alifunga mabao hayo wakati wakipata ushindi wa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Singapore ambapo Japan walikuwa kama hawapo uwanjani kwa jinsi alivyothibitiwa.
Mkali huyo alianza kuandika bao dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri ya Diego Tardelli kabla ya kuongeza jingine dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Coutinho.
Neymar aliongeza bao la tatu dakika ya 77 kabla ya kupigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 81 kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi pasi ya Kaka na kuzidi kumpa raha kocha Dunga anayeinoa Brazil kwa sasa.
Katika mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa, China iliiduwaza Paraguay kwa kuwacharaza mabao 2-1. Mabao ya washindi yalifungwa dakika 20 za awali na Zheng Zi na Wu Lei kabla Ortigoza kuipatia Paraguay bao la kufutia machozi dakika za jioni.
Nayo timu ya Costa Rica Iliiadhibu Jamhuri ya Korea kwa mabao 3-1 katika mchezo mwingine mkali wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa mapema mchana wa leo.
Katika mechi nyingine inayoendelea kwa sasa nchini Hongkong, wenyeji wameshakandikwa mabao 6-0 na Argentina na bado dakika kama 15 kabla ya mchezo huo kuisha, Messi akifunga moja na mengine yakiwekwa kimiani na Higuan mawili na Gaitan pia mawili na Banega

Walcott aleta faraja Emirates, arejea dimbani

http://1.bp.blogspot.com/-P9huTUKnjx4/UVEmIVazb-I/AAAAAAAAEFw/4z77MC2CELU/s1600/Theo+Walcott+wallpaper+13.jpgWINGA machachari, aliye nyota wa Uingereza, Theo Walcott ameleta faraja kwa mashabiki wa Arsenal baada ya kurejea dimbani kutoka kwenye hali ya majeruhi kwa muda wa miezi 10 iliyopita kwa kujiumiza vibaya goti lake.
Walcott, 25, hajacheza tangu kukata mishipa ya goti lake la kushoto kwenye ushindi wao wa 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspurs katika Kombe la FA Januari.
“Ni shangwe kukukaribisha tena @theowalcott!” Arsenal waliandika kwenye anwani yao rasmi ya mtandao wa kijamii wa Twitter pamoja na picha yake akipasha misuli na wenzake.
Arsenal watakaribisha Hull City Jumamosi kwenye pambano la Ligi Kuu ya England akiungana na kiungo mwenzake wa pembeni, Serge Gnabry aliyekuwa akiuguza pia goti tangu Machi.
Wawili hao wameinua mioyo ya Ze Gunnerz ambayo itawakosa nyota wake kadhaa waliopo kwenye 'wadi' ya majeruhi viunga vya Emirates akiwamo Mesut Ozil.

Kuziona Simba na Yanga ni Buku 7 tu

Yanga
Simba
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, limetengaza viingilio vya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga litakalochezwa Jumamosi ambapo cha chini kabisa ni Sh. 7,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000. Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro.
Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. 
Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.

Morocco yaigonga Kenya 3-0 kirafiki

http://i.ytimg.com/vi/fkaBqomsiF4/maxresdefault.jpgTIMU ya soka ya taifa ya Morocco imeendelea kutoa dozi kwa wapinzani kwenye mechi za kirafiki baada ya usiku wa jana kuikong'ota Kenya Harambee Stars kwa mabao 3-0 ikiwa ni siku chache tangu iishindilie Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mabao 4-0 siku ya Ijumaa.
Mabao ya dakika 15 za mwisho yalitosha kuwatia adabu Harambee Stars ambao walionyesha kandanda zuri kwa muda mrefu wa mchezo kabla ya kuruhusu mabao hayo matatu.
El Mehdi Karnass, Mbark Boussoufa na Mouhcine Iajour kila mmoja alifunga bao moja ndani ya dakika hizo 15 kabla ya pambano hilo kumalizika na kuwapa wenyeji ushindi huo kwenye uwanja wa Marrakech na kuzidi kumpa CV nzuri kocha Ezzaki Badou ambaye katika mechi tatu za karibuni ameshinda zote kwa idadi ya mabao 10 baada ya awali kuwalaza pia Libya mabao 3-0..
Kwa Harambee inayoniolewa na kocha Adel Amrouche ilikuwa ni mechi ya sita ya kimataifa bila kupata ushindi wowote.

Suarez arejea na mabao Uruguay, afunga mbili wakiiua Oman x3

http://level3.soccerladuma.net/cms2/image_manager/uploads/News/166456/7/default.jpgMSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Luis Suarez amerejea uwanjani na makali yake yale baada ya usiku wa jana kuisaidia timu yake ya taifa ya Uruguay kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wao Oman.
Pambano hilo la kimataifa la kirafiki lililochezwa kwenye uwanja wa Sultan Qoboos mjini Muscat, Suarez aliyekuwa akicheza mechi yake ya pili ya kimataifa tangu alipotoka kifungoni alifunga mabao mawili.
Suarez alifunga mabao hayo kwenye dakika ya 57 akimalizia kazi nzuri ya Rolan na katika dakika ya 67 kwa pasi ya Ramirez kabla ya Jonathan Rodriguez kufunga la tatu dakika ya 87.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool alifungiwa na FIFA kutokana na kitendo cha kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini katika michuano ya Kombe la Dunia zilizochezwa nchini Brazil.

WENGER HAJUTII KUTOMSAJILI FABREGAS

http://static.sportskeeda.com/wp-content/uploads/2014/06/104741_heroa-1402851267.jpgKOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesisitiza kwamba hajuti kumsajili Cesc Fabregas katika kipindi kilichopita cha usajili.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alijiunga na Chelsea akitokea Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 27 mwezi Juni na ametisha chini ya Mourinho akitoa pasi za mwisho zilizozaa magoli 7 katika mechi 7, idadi ambayo ni sawa na pasi za mwisho zote zilizopigwa na timu nzima ya Arsenal hadi sasa.
Fabregas ambaye aliichezea Arsenal kwa miaka nane kabla ya kurejea Barcelona 2011, alibainisha katika barua yake ya wazi kwamba Arsenal walikataa kukitumia kipengele cha mkataba cha kumsajili tena kama wanamhitaji kabla ya klabu nyingine kupewa ofa hiyo.
Lakini, Wenger amesisitiza kwamba ana wachezaji wengi wa eneo la kiungo na anaamini kwamba timu yake itapunguza pengo la pointi dhidi ya Chelsea licha ya kulala 2-0 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kabla ya wikiendi ya mechi za kimataifa. 
"Sijutii kutomchukua Cesc kwa sababu tayari tuna wachezaji wengi wa ubunifu katika eneo letu la kiungo," Wenger aliiambia BeIN Sports.
"Chelsea watatakuwa na kipindi kigumu (katika msimu). Ratiba yetu ilikuwa ngumu mno na ninaamini kwamba tunaweza kuziba pengo dhidi yao."