STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 14, 2014

Neymar 4 Japan 0, China yaigonga Paraguay, Costa Rica ikiiua Korea

International friendlies - Four-goal Neymar destroys Japan to reach 40 for Brazil
Akishangilia bao lake la tatu
Neymar célèbre sa prestation exceptionnelle avec le Brésil contre le Japon
Neymar akishangilia moja ya mabao yake mchana huu wakati wanaizamisha Japan kwa mabao 4-0
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Neymar amethibitisha kuwa yeye ndiye kila kitu Brazil baada ya kuifungia timu yake mabao manne wakati timu yake ya taifa ikiiadhibu Japan katika mechi ya kurafiki ya kimataifa.
Neymar alifunga mabao hayo wakati wakipata ushindi wa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Singapore ambapo Japan walikuwa kama hawapo uwanjani kwa jinsi alivyothibitiwa.
Mkali huyo alianza kuandika bao dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri ya Diego Tardelli kabla ya kuongeza jingine dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Coutinho.
Neymar aliongeza bao la tatu dakika ya 77 kabla ya kupigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 81 kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi pasi ya Kaka na kuzidi kumpa raha kocha Dunga anayeinoa Brazil kwa sasa.
Katika mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa, China iliiduwaza Paraguay kwa kuwacharaza mabao 2-1. Mabao ya washindi yalifungwa dakika 20 za awali na Zheng Zi na Wu Lei kabla Ortigoza kuipatia Paraguay bao la kufutia machozi dakika za jioni.
Nayo timu ya Costa Rica Iliiadhibu Jamhuri ya Korea kwa mabao 3-1 katika mchezo mwingine mkali wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa mapema mchana wa leo.
Katika mechi nyingine inayoendelea kwa sasa nchini Hongkong, wenyeji wameshakandikwa mabao 6-0 na Argentina na bado dakika kama 15 kabla ya mchezo huo kuisha, Messi akifunga moja na mengine yakiwekwa kimiani na Higuan mawili na Gaitan pia mawili na Banega

No comments:

Post a Comment