TIMU ya soka ya taifa ya Morocco imeendelea kutoa dozi kwa wapinzani kwenye mechi za kirafiki baada ya usiku wa jana kuikong'ota Kenya Harambee Stars kwa mabao 3-0 ikiwa ni siku chache tangu iishindilie Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mabao 4-0 siku ya Ijumaa.
Mabao ya dakika 15 za mwisho yalitosha kuwatia adabu Harambee Stars ambao walionyesha kandanda zuri kwa muda mrefu wa mchezo kabla ya kuruhusu mabao hayo matatu.
El Mehdi Karnass, Mbark Boussoufa na Mouhcine Iajour kila mmoja alifunga bao moja ndani ya dakika hizo 15 kabla ya pambano hilo kumalizika na kuwapa wenyeji ushindi huo kwenye uwanja wa Marrakech na kuzidi kumpa CV nzuri kocha Ezzaki Badou ambaye katika mechi tatu za karibuni ameshinda zote kwa idadi ya mabao 10 baada ya awali kuwalaza pia Libya mabao 3-0..
Kwa Harambee inayoniolewa na kocha Adel Amrouche ilikuwa ni mechi ya sita ya kimataifa bila kupata ushindi wowote.

No comments:
Post a Comment