STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 12, 2014

Usiku wa Mwambao Asilia kufanyika Dar Apr 19

Kundi la Dar Modern litakaloshiriki Usiku wa Mwambao Asilia
KUNDI la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), wanatarajiwa kutoa burudani ya aina yake katika onesho maalumu la ‘Usiku wa Mwambao Asilia’, ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam, Aprili 19.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mlezi wa Heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema wadau wa muziki wa taarabu watafurahia usiku huo wa Mwambao Asilia kutoka kwa wanamuziki nguli wa miondoko hiyo hapa nchini na visiwani.

“Usiku wa Mwambao Asilia, utasheheni magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, kutoka kundi la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan, ambao wataporomosha nyimbo za taarabu asili za zamani na za sasa,” alisema Asia Idarous.

Aliongeza kuwa, pia usiku huo utapambwa na ‘surprise’, ikiwemo watu mbalimbali kupita kwenye zuria jekundu ‘red carpet’ na kupiga picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria usiku huo.

Alisema katika usiku huo, kiingilio kitakuwa ni sh 10,000 ambako tayari tiketi zimeshaanza kuuzwa sehemu mbalimbali.

Asia, alizitaja sehemu hizo kuwa ni pamoja na duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda. Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashion

Nusu fainali za UEFA Europa League hii hapa

http://theoriginalwinger.com/wp-content/uploads/2014/04/Europa-Draw.jpg

http://news.images.itv.com/image/file/375918/article_img.jpg
Juventus
KLABU za Sevilla na Valencia zote kutokea Hispania zimepangwa pamoja katika pambano la Nusu Fainali ya Ligi Ndogo ya Ulaya (Europa League) huku mabingwa wa Italia Juventus wakitupiwa Benfica ya Ureno kupepetana nao katika hatu hiyo katika droo ilitangazwa jana.
Valencia na Sevilla ambazo zilipindua matokeo yao ya awali walipolazwa ugenini na kushinda nyumbani kwa idadi kubwa ya mabao dhidi ya Porto na Basel zinakutana kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya.
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa April 24 na kurudiana Mei Mosi kabla ya timu zitakazofuzu hatua hiyo kuumana kwenye fainali Mei 14 mjini Torino, nchini Italia.
Sevilla waliowahi kutwaa taji hilo mara mbili 2006 na 2007 itaikaribisha mabingwa wa 2004 nyumbani kabla ya kuwafuata wapinzani wao sawa itaklavyokuwa kwa Benfica ambayo haijawahi kunyakua taji hilo itakapoikaribisha Juventus waliotwaa taji hilo mara tatu 1977, 1990 na 1993katika mechi ya mkondo wa kwanza kabla ya kuwafuata Waitalia nyumbani kwao mechi ya marudiano.

Miyeyusho, Cheka kuvuna nini leo PTA?

Miyeyusho (kulia) na mpinzani wake walipopima uzito jana

Cheka akipimwa uzito huku mpinzani wake kutoka Iran akishuhudia
MABONDIA  Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ na Francis Cheka 'SMG' wanatarajiwa kupanda ulingoni leo kwenye ukumbi wa PTA, Dar es Salaam kupambana na wageni kutoka Thailand na Iran.
Miyeyusho atazipoga na Sukkasem Kietyongyuth na Cheka akivaana na Gavad Zohrehvand kutoka Iran katikkaa mipambano isiyokuwa na ubingwa.
Pambano hilo la Miyeyusho litakuwa la raundi 10 na linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na mabondia wote kujiandaa vizuri.
“Maandalizi niliyofanya ni makubwa, hii yote kwa sababu sitaki kuwaangusha Watanzania, kwani hili ndilo pambano langu la kwanza la kimataifa kufanyika katika ardhi ya nyumbani, hakuna haja ya kupoteza zaidi ya ushindi wa K.O,” alisema Miyeyusho. 
Pambano la Cheka litakuwa la raundi nane na litakuwa la utangulizi. 
Promota wa pambano hilo, Mussa Kova, amewataka wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kwenye mapambano hayo ya kihistoria.
Cheka atapanda ulingoni ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipotwanga Urusi na kupoteza taji lake la Dunia la WBF alilolitwaa Agosti 30 kwa kumpiga Mmarekani, Phil Williams.
Katika michezo hiyo pia kutakuwa na mechi za utangulizi zitakazowakutanisha mabondia mbalimbali za jijini Dar es Salaam likiwa kati ya Ibrahim Class dhidi ya Mustafa Dotto.

NUSU FAINALI ULAYA IKO HIVI

* Chelsea vs Atletico, Real v Bayern
http://www.scaryfootball.com/wp-content/uploads/2014/04/Champions-league-semi-final-draw-real-madrid-bayern-munich-atletico-madrid-chelsea-2014-winner.jpg 
http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/002/843/906/a5b49d9267ff1018c37bbe654ea8770f_crop_north.jpg?w=630&h=420&q=75
Mashabiki wanasubiri kuona vita kama hii katika Nusu Fainali ya Ligi ya Ualaya baina ya Atletico Madrid na Chelsea
http://www.fifa.com/mm/photo/tournament/competition/01/27/28/06/1272806_full-lnd.jpg
Nyota hawa Robben na Casillas watakutana kwenye mechi baina ya timu zao za Bayern Munich na Real Madrid
KLABU ya Chelsea imejikuta ikiangukia mikononi mwa Atletico Madrid katika mechi ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Droo ya Nusu Fainali iliyofanyika jana imemtupa kocha Jose Mourinho kwa vinara wa La Liga, Atletico Madrid waliyoing'oa Barcelona katika Robo Fainali.
Real Madrid itamenyana na mabingwa watetezi, Bayern Munich katika Nusu Fainali nyingine huku mechi za kwanza zikichezwa Aprili 22 na 23 na marudiano wiki inayofuata.
Ikumbukwe kipa tegemeo wa Atletico Thibaut Courtois mwenye umri wa miaka 21 anachezea timu hiyo kwa mkopo kutoka Chelsea.
Tayari UEFA imetoa ruksa kwa Atletico kumtumia kipa huyo baada ya kushtukia dili lililokuwa likifanywa na Chelsea la kutaka kwanza walipwe fedha kutoa baraka hizo.

Ashanti United kulipa kisasi kwa Simba kesho?

Ashanti United
Simba
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea leo na kesho kwa mechi saba za raundi ya 25 ambapo Simba na Ashanti United zitapambana kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo, Ashanti ilikubali kipigo cha mabao 4-2 hivyo itakuwa na kazi ya kulipiza kisasi kesho kwa vijana wa Msimbazi sawia na kutafuta pointi za kuwaweka pazuri ili wasiwe miongoni mwa timu zitakazocheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo katika mfululizo wa ligi hiyo Mtibwa Sugar itakaribisha  Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Manungu mjini Turiani Morogoro, huko mjini Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani wenyeji Coastal Unioni watavaana na JKT Ruvu na Prisons itaialika Rhino Ranger kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mebya.
Kesho ndiyo kutakuwa na funga kazi ukiondoa pambano la Simba na Ashanti United jijini Dar viwanja vitatu zaidi vitawaka moto, ambapo kwenye uwanja  wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Yanga inahitaji ushindi na huku ikiwaombea mabaya Azam wanaoongoza msimamo na wakiwa mkono mmoja kwenye taji la ubingwa ili wafanye vibaya mjini Mbeya pia kesho kwenye uwanja wa Sokoine watakapovaana na Mbeya City.
Azam wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 56, huku Yanga wakifuata wakiwa na pointi 52 na Mbeya wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45 na kujihakikisha nafasi ya tatu ikiwa ni msimu wao wa kwanza kucheza ligi hiyo na kuonyesha makeke ya kusisimua.
Pia kesho kutakuwa na kivumbi cha mechi kati ya Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.