STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 12, 2014

Ashanti United kulipa kisasi kwa Simba kesho?

Ashanti United
Simba
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea leo na kesho kwa mechi saba za raundi ya 25 ambapo Simba na Ashanti United zitapambana kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo, Ashanti ilikubali kipigo cha mabao 4-2 hivyo itakuwa na kazi ya kulipiza kisasi kesho kwa vijana wa Msimbazi sawia na kutafuta pointi za kuwaweka pazuri ili wasiwe miongoni mwa timu zitakazocheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo katika mfululizo wa ligi hiyo Mtibwa Sugar itakaribisha  Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Manungu mjini Turiani Morogoro, huko mjini Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani wenyeji Coastal Unioni watavaana na JKT Ruvu na Prisons itaialika Rhino Ranger kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mebya.
Kesho ndiyo kutakuwa na funga kazi ukiondoa pambano la Simba na Ashanti United jijini Dar viwanja vitatu zaidi vitawaka moto, ambapo kwenye uwanja  wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Yanga inahitaji ushindi na huku ikiwaombea mabaya Azam wanaoongoza msimamo na wakiwa mkono mmoja kwenye taji la ubingwa ili wafanye vibaya mjini Mbeya pia kesho kwenye uwanja wa Sokoine watakapovaana na Mbeya City.
Azam wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 56, huku Yanga wakifuata wakiwa na pointi 52 na Mbeya wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45 na kujihakikisha nafasi ya tatu ikiwa ni msimu wao wa kwanza kucheza ligi hiyo na kuonyesha makeke ya kusisimua.
Pia kesho kutakuwa na kivumbi cha mechi kati ya Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment