TIMU
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza inaendelea
vizuri katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani
yanayoendelea Rio de Janeiro nchini Brazil ambapo katika mchezo wake wa
kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2 na Burundi.
Juzi
(Machi 31 mwaka huu), timu hiyo inayoongozwa na mjumbe wa Mkutano Mkuu
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka Mkoa wa Mwanza,
John Kadutu ilicheza mechi mbili. Katika mechi ya kwanza iliifunga
Argentina mabao 3-0 na baadaye ikailaza Nicaragua mabao 2-0.
Michuano hiyo ya siku kumi inashirikisha timu kumi. Mbali ya Tanzania, nyingine ni
Argentina,
Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan.
Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia,
Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment