STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 2, 2014

As Roma yaiua Parma na kupunguza pengo la pointi kwa Juve

Francesco Totti celebrates his goal against Parma
Totti akishangilia bao lake aliloifungia As Roma wakati wakiiua Parma
KLABU ya AS Roma imezidi kupunguza pengo la pointi na vinara wa Ligi ya Italia, Juventus baada ya usiku huu kuicharaza Parma mabao 4-2 katika mfululizo wa ligi hiyo maarufu kam Seria A.
Gervinho alianza kuiandikia wenyeji Roma bao katika dakika ya 12 kabla ya wageni kulirejesha katika dakika tatu baadaye kupitia kwa Acquah na Francisco Totti akiiongezea Roma bao la pili dakika ya 16.
Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko na katika kipindi cha pili, Roma walianza kwa kufunga bao la tatu kupitia kwa Pjanić katika dakika ya 49 kabla ya Taddei kuongeza la nne dakika nane kabla ya pambano hilo kumalizika.
Hata hivyo wageni walijipatia bao lao la pili la kufutia machozi katika dakika ya 90 lililofungwa na Biabiany.
Ushindi huo umeifanya Roma kufikisha pointi 73, nane pungufu na za vinara wa ligi hiyo Juve yenye pointi 81.

No comments:

Post a Comment