STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 2, 2014

Man Utd yakomaa kwa Bayern, Barca yabanwa nyumbaniBayern

Bayern Munich wakichomoa bao la Man Utd
Heka heka kati ya Manc Utd na Bayern Munich jana

Neymar akionyesha manjonjo yake

Messi akipasua mbele ya wachezaji wa Atletico Madrid
MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich jana ilishindwa kufurukuta nyumbani kwa Manchester United baada ya kulazimishwa sare ya 1-1, kama ilivyokuwa kwenye pambano la wenyeji Barcelona dhidi ya vinara wa La Liga, Atletico Madrid katika mechi mbili tofauti za Robo Fainali ya michuano hiyo ya Ulaya.
Manchester Unitd ikiwa kwenye dimba lake la Old Trafford, walionyesha wamepania kuondoa unyonge na kuwafurahisha mashabiki wao walioikatia tamaa kutokana na mwenendo mbaya iliyonayo kwa msimu huu baada ya kutangulia kupata bao lililofungwa na Nahodha, Nemanja Vidic katika dakika ya 58 akimalizia kona murua iliyochongwa na Wayne Rooney na yeye kufunga kwa kichwa.
Hata hivyo dakika nane baadaye wageni walicharuka na kujipatia bao la kusawazisha lililofungwa na Bastian Schweinsteiger aliyemalizia kazi nzuri ya Mario Mandzukic.
Hata hivyo mfungaji huyo Schweinsteiger alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya nyongeza kabla ya mchezo kuisha kwa kumchezea vibaya Rooney na hivyo atakosa mechi ya marudiano jumatano ijayo.
Katika pambano jingine la michuano hiyo Mbrazili Neymar aliisawazishia timu yake ya Barcelona kwenye uwanja wa nyumbani wa Camp Nou na kuepuka kipigo toka kwa wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa wa La Liga, Atletico Madrid iliyojikuta ikimpoteza nyota wao, Diego Costa aliyeumia mapema kipindi cha kwanza.
Mchezaji aliyechukua nafasi ya Costa, Mbrazil Diego aliifungia Atletico bao dakika ya 56  kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Gabi kabla ya Neymar kuja kusawazisha katika dakika ya 71 kwa pasi ya Andres Iniesta na kuwafanya wageni hao kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya 10 kama watapata sare isiyo na magoli kwao.
Timu hizo zitarudiana jumatano ijayo kujua hatma ya mmoja wao kuitinga nusu fainali.

No comments:

Post a Comment