|
Sehemu ya igizo hilo kama lilivyokuwa likionekana kwenye screen |
|
Wadau wakipata uhondo wa Kipusa |
|
Iizo likiendelea kwenye runinga |
|
Wadau na wasanii walioshiriki igizo hilo wakifuatilia kwa makini |
|
Joti aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa kujadili igizo hilo akizuingumza na wadau waliohudhuria onyesho hilo |
|
We kichwa bana na mkikomaa mtafika mbali na kuleta mapinduzi katika tasnia yetu: Ni kama Raia wa TAFF Simon Mwakifamba akimwambia Katibu wa New Kaole Sanaa, Issa Kipemba |
|
Rais wa TAFF, Simon Mwakifanya (kulia) akitoa nasaha zake huku Joti akimsikiliza kwa makini |
|
Simon Mwakifamba Rais wa TAFF akiwa na Mwenyekiti wa New Kaole, Ndimbangwe Misayo 'Thea'. |
|
Mabrekaaaa! Swebe Santana (kulia) Bi Staa na Bi Terry nao walikuwapo na Muongozaji wa filamu hiyo, Christant Mhengga akionekana kwa nyuma yao (shati jeusi) |
|
Yaani ilikuwa ni fursa ya kuwaona wasanii wakali waliosahaulika kitambo |
|
Nyie wenyewe mmeiona ni bab' kubwa---Joti akizungumza leo |
|
Wadau wakiwa makini kufuatilia igizo kwenye runinga |
|
Ilikuwa ni full burudani toka kwa wakali hao waliokumbusha enzi zao kupitia KIPUSA |
|
Watu walikuwa makini kufuatilia |
|
Chifu Husseni Msopa, Sheikh Sadik Godegode na Sheikh Kassim wakiwa makini kufuatilia igizo hilo |
|
Abdallah Mkumbira 'Muhogo Mchungu' Makamu Mwenyekiti wa New Kaole na mmoja walioling'arisha igizo hilo la Kipusa naye alikuwapo kujishuhudia. |
|
Oyaa umeona pale da! Kama wanaambizana Chifu Msopa na Sheikh Godegode |
|
Watu walikuwa makini kupita maelezo |
|
Viongozi wa Kaole, waigizaji wa Kipusa na wageni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla hiyo |
|
Hakuna aliyetaka kupitwa na uhondo |
|
Sehemu ya waliohudhuria wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii walioshiriki igizo la Kipusa |
|
Muongozaji mahiri wa tamthilia na filamu nchini, Christant Mhengga akitoa nasaha zake |
|
Mwenyekiti wa Kaole Sanaa, Ndimbangwe Misayo 'Thea' akizungumza yake kushukuru wadau waliohudhuria |
|
Kusudio letu ni hili....Thea akizungumza |
|
Kama Mwinjilisti! Thea akiendesha dua maalum ya kufungia hafla mbele ya wadau |
|
'Tunakuomba kwa Jina la Bwana Yesu Kristo Ameen" Wadau wakiwa makini wakati dua maalum iliyoendeshwa na Thea |
KUNDI la Kaole Sanaa ambalo kwa karibu miaka 10 lilikuwa kimya, leo limeitambulisha kwa wadau wao tamthilia yao mpya iitwayo 'Kipusa' inayowarejesha rasmi katika ulimwengu wa sanaa nchini.
Utambulisho wa tamthilia hiyo
inayorejesha kumbukumbu ya enzi za kundi hilo lilipokuwa likitisika
anga la sanaa, ulifanyika kwenye ukumbi wa Dar Modern, uliopo Magomeni
Mikumi, jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuwaonjesha kidogo uhondo
mzima wa tamthilia hiyo, lakini wadau waliohudhuria waliburudika vya
kutosha na kuwasifia wasanii walioanzisha wazo hilo la kurejesha kundi
hilo.
Baadhi ya wadau waliopata nafasi ya kutoa maoni yao baada ya
kushuhudia sehemu mbili kati ya 25 za tamthilia hiyo walikiri Kaole ni
Baba wa Sanaa na kuwataka wasanii hao kutorudi nyuma.
Miongoni mwa
waliohudhuria ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon
Mwakifamba, viongozi wa Taasisi ya Amani Tanzania, Sheikh Sadik Godegode
na Mwenyekiti wa Baraza la Habari la Kiislam (BAHAKITA), Chifu Hussen
Msopa.
Katika nasaha zake ndogo Rais wa TAFF aliwasifia viongozi na
wasanii wa Kaole kwa kutoa wazo la kulirejesha kundi hilo na kudai kuwa
wao ndiyo wasanii wa ukweli na wanaojua wanachokifanya.
Mwakifamba
pia aliwasisitizia kundi hilo kulenga soko la kimataifa ili angalau
Tanzania iweze kutamba na kunyakua tuzo kama ambavyo wasanii wa mataifa
ya Nigeria, Kenya na nchi nyingine.
Mwenyekiti wa kundi hilo,
Ndimbangwe Misayo 'Thea' aliwashukuru waliohudhuria na kuwataka
waendelee kuwaunga mkono katika safari yao ambayo ndiyo kwanza
wameianza.
Naye Muongozaji na mmoja wa waasisi wa kundi hilo,
Christant Mhenga, alisema anachukua maoni, ushauri na hata ukosoaji
uliotolewa na baadhi ya wadau kama changamoto za kuboresha kazi yao.
Msanii
wa muziki, Vitalis Maembe 'Mzee wa Sumu ya Teja' aliahidi kuwapiga tafu
Kaole ili kuendeleza mipango yao ya kurejesha heshima ya sanaa ya
maigizo nchini.
No comments:
Post a Comment