STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 2, 2014

Real Madrid yaifumua Dortmund, Chelsea yafa kwa PSG

Gareth Bale scores for Real
Bale akifunga bao lake

Ezequiel Lavezzi
Lavezzi akishangilia bao la kwanza alililoifungia PSG wakati wakiiangamiza Chelsea mjini Paris
REAL Madrid imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya muda mfupi uliopita kuifumua Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mabao 3-0, huku Chelsea ya England ikikong'otwa ugenini kwa m,abao 3-1 na PSG ya Ufaransa katika mchezo mwingine wa robo fainali.
Madrid inayosaka taji la 10 la Ulaya na baada ya kupita zaidi ya miaka 12 bila kulitwaa tzngu ilipofanya hivyo mwakaq 2002, iliutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuwashtukiza wageni kwa bao la mapema.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Gareth Bale katika dakika ya tatu tu ya mchezo akimalizia kazi ya Daniel Carvajal kabla ya ya Isco kuongeza la pili dakika ya 27 na kudumu hadi wakati wa mapumziko.
Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Cristiano Ronaldo alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 57 akimalizia kazi ya Luca Modric na kuiweka Real katika nafasi nzuri kabla ya mechi ya marudiano wiki ijayo.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mjini Paris Ufaransa,wenyeji PSG waliifanyia kitu mbaya Chelsea kwa kuizabua mabao 3-1 na kujiweka pazuri kufuzu nusu fainali kama itakomaa mechi yao ijayo mjini London.
Ezequiel Lavezzi aliifungia wenyeji bao la mapema la dakika 4 kabla ya Chelsea kuchomoa kwa mkwaju wa penati kupitia Eden Hazard katika dakika ya 27 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa kwa kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilikuwa kiama kwa Chelsea baada ya David Luiz kujifunga bao kdakika ya 61 kabla ya javier Pastore kumalizia udhia kwa kufunga bao la tatu katika dakika xa nyongeza na kuiweka PSG katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, ingawa Chelsea siyo ya kubezwa kutokana na kuambulia bao hilo la ugenini linaloweza kuwabeba kama wakishinda Stanford Bridge kwa mabao 2-0

No comments:

Post a Comment