STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 25, 2013

MACHINGA WAONDOLEWA MANZESE OPERESHENI SAFISHA JIJI 

ASKARI WA JESHI LA POLISI KIKOSI CHA KUZUIA GHASIA AKIWA KATIKA DORIA LEO ENEO LA MANZESE


HALI HALISI KATIKA ENEO LA WAFANYABIASHARA ULINZI


BAADHI YA WAFANYABIASHARA WAKIWA HAWAJUI LA KUFANYA

ENEO LA MANZESE MITAA IKIWA WAZI

ASKARI WA MGAMBO WAKIWA KATIKA DORIA

MOJA YA MTAA ENEO LA MANZESE

WAKAAZI WAKIPITA MBELE YAN ASKARI

WAKAZI WAKIPITA ENEO LA BIASHARA LIKIWA WAZI

WAKAZI WAKIPITA ENEO LA BIASHARA LIKIWA WAZI


ASKARI WA JIJI WAKIWA PATRO ENEO LA MANZESE

KIJIKO CHA UJENZI WA BARABARA YA MWENDO KASI ENEO LA MANZESE
WAFANYABIASHARA ndogo ndogo (Machinga) waliokuwa wamehodhi eneo la Manzese wametimuliwa ikiwa ni muendelezo wa kusafisha jiji hasa katika kipindi hiki cha ujio wa Rais wa Marekani, Barrack Obama.
Hata hivyo taarifa za chinichini toka kwa baadhi ya watendaji wa Manispaa ya Kinondoni ni kwamba machinga hao wameondolewa kutokana na mkandarasi anayetengeneza barabara ya Morogoro kupata wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yake kutokana na eneo kubwa kujaa wachuuzi hao kiasi cha kuwafanya wafanye kazi zao katika mazingira magumu.
MICHARAZO ilipita nyakati za mchana na kushuhudia barabara hiyo ikiwa nyeupe kukiwa hakuna biashara yoyote inayofanyika zaidi ya doria ya magari ya askari polisi, mgambo na walinzi shirikishi wengine, huku vijana waliozoea kuendesha biashara zao wakiwa wanawaangalia kwa chuki askari hao kwa kuwasababishia wakose riziki kwa doria wanalofanya.
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika eneo hilo walionyesha kuunga mkono operesheni hiyo kwa sababu imewafanya watembee kwa kujinafasi japo wengine walikuwa wakihisi kutumuliwa kwa machinga hao kunaweza kusababisha hali ya uhalifgu kukithiri mitaani kwani vijana hao watakosa kazi za kuwaingizia riziki kama walivyokuwa wakifanya

Wagosi wa Kaya kufanya mkutano wao Jumapili jijini Tanga

http://4.bp.blogspot.com/-0IbpT2QPvrE/T6dzaPeecXI/AAAAAAAAEEQ/EAZtVUtpkuk/s320/Coastal+Union+logo.JPG

WANACHAMA wa klabu ya soka ya Coastal Union ya jijini Tanga wanatarajiwa kufanya mkutano wa pamoja ulioitishwa na uongozi wa klabu hiyo utakapofanyika siku ya Jumapili.
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi ilinukuliwa kwenye mtandao wa klabu hiyo ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili na kupanga mikakati ya ushiriki wao wa Ligi kuu Tanzania Bara inayaotarajiwa kuanza kivumbi chake Agosti mwaka huu.
Taarifa hiyto ya uongozi wa Coastal umewahimiza wanachama kujitokeza kwa wingi bila kujali wana kadi au la mradi kufanikisha mkutano huo na kujiweka mguu sawa wakiwa kitu kimoja ili kurejesha heshima iliyowapa ubingwa mwaka 1988.
Ebu jisomee mwenyewe taarifa hiyo hapo chini juu ya mkutano huo

Uongozi wa Coastal Union unawatangazia mashabiki wake walio ndani na nje ya nchi kuwa siku ya jumapili wiki hii June 30 kutakuwa na mkutano mkuu wa wanachama utakaofanyika mjini Tanga.

Mkutano huo ni muhimu kuhudhuria hata kama huna kadi ya uanachama, kwani itakuwa ni fursa pekee ya kupanga mikakati ya msimu ujao wa soka 2013/14 ili kuhakikisha kikosi imara cha wana Mangush kinaweka heshima ya soka nchini kwa kuchukua ubingwa kama walivyofanya mwaka 1988.

Uongozi unaweka wazi kuwa kwa yeyote ambaye ana malalamiko ama ushauri juu ya kuendesha timu ili kufikia mafanikio, basi ahudhurie kwenye mkutano ili kumaliza kiu yake na si kusema pembeni bila tija.

Siku hiyo mbali ya ajenda za kujenga timu pia kutakuwa na mikakati ya viongozi na kugawa majukumu kwa wanachama, pia kutajadiliwa namna ya kuhakikisha mashabiki walio mikoani na nje ya nchi wanatambulika rasmi na kukaribisha michango ya hali na mali kwa lengo moja tu, kuleta ushindi msimu ujao.

Tayari timu yetu imesharudi nyoyoni mwa wapenda soka, kilichobaki ni kuhakikisha hatuwavunji moyo wapenzi wetu cha kufanya ni kupata kadi ya uanachama ambazo zitatolewa siku hiyo, na pia kutawekwa utaratibu bora wa kuhakikisha timu inatunisha mfuko wa maendeleo.

Wanachama wengi wanawasiliana katika mitandao lakini hawajuani kwa sura hii itakuwa nafasi ya kipekee kuweza kujuana na kubadilishana mawazo, tayari wanachama wengi kutoka mikoa ya jirani wamethibitisha kuhudhuria mkutano huo, umebaki wewe tu.

Tuache kusemasema vipembeni tuelekee kwenye mkutano mkuu tarehe 30 June, 2013.

Cheka uso kwa uso na Mmarekani DarBango linaloonyesha mapambano ya ngumi za kulipwa zinazotarajiwa kuwakutanisha wakali wa mchezo wenye sifa kubwa nchini.

Hatimaye mume wa Joyce Kiria aonekana hadharani

Bw.Henry Kileo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.
Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.
 Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo.
 Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013

Na Josephat Isango wa Tanzania Daima.

KAIMU Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa  Dar es Salaam, Henry Kilewo, anashikiliwa  na polisi , akihusishwa na  tukio la kumwagiwa tindikali, Musa Tesha. Tesha alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana Septemba 9, mwaka juzi kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, uliomuweka madarakani Dk. Kafumu Dalali.
Akizungumza juzi na Tanzania Daima kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi, Kilewo alisema hajui anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi hilo kuwa afike ofisini kwao. “Sijui ninachoitiwa, nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito, nimesha wataarifu mawakili wangu ninaowaamini, kwa kuwa chochote kinaweza kutokea cha msingi Watanzania wapenda mageuzi waniombee kwa Mungu,” alisema Kilewo.
Wakili wa Kilewo, Peter Kibatala, alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa muda wa saa tano juzi alielezwa kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya kutumia tindikali na kujeruhi.
Kibatala alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja wake ilhali kosa wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha mahakamani. Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia tindikali na kudhuru watu ni pamoja na  Oscar Kaijage wa Shinyanga na Evodius Justinian wa Bukoba.
Evodius Justinian alikamatwa na  Jeshi la Polisi mjini Bukoba na kushikiliwa kwa siku kadhaa kabla ya  kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam. Kabla ya kusafirishwa na kufikishwa jijini Da r es Salaam, Justinian alieleza kuteswa na kupigwa na askari waliokuwa wakimzuia katika vituo mbalimbali kuanzia mjini Bukoba.
Joyce Kiria alipoandamana kushinikiza serikali imuonyeshe mumewe yupo wapi baada ya ukimya tangu afikishwe kituo kikuu cha Polisi Dar.

Maajabu ya Mungu! Msaidie mama huyu kuwaokoa watoto wake


MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Kasumuru, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Grace Joel Lwesha (19), amelia baada ya kujifungua watoto walioungana.


Akizungumza na waandishi wetu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jengo la Watoto, Grace alilia kutokana na kile alichodai kujifungua watoto walioungana wakati yeye ni maskini.


Watoto hao mapacha wa kiume, Eliudi na Elikana wameungana sehemu ya makalio hivyo kulazimika kutumia sehemu moja ya haja kubwa.

Grace aliwaambia waandishi wetu kwamba, watoto hao walizaliwa katika Hospitali ya Kyela, Februari 20, mwaka huu wakiwa na miguu miwili na mikono miwili kila mmoja.


“Baada ya kujifungua Machi mosi nilihamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa uchunguzi zaidi ili waweze kujua ni jinsi gani watakavyotenganishwa,” alisema.


Hata hivyo, hospitali hiyo ya mkoa haikufanikiwa badala yake Machi 16, walimhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kuanzia hapo mpaka sasa anafanyiwa maandalizi kwa ajili ya safari ya kupelekwa nchini India kwa upasuaji.

 “Ninawapenda sana watoto wangu hawa pamoja na kwamba wapo katika hali hii, ndugu zangu walipokuja hospitalini kuniona akiwema mama yangu walinifariji na kunisihi nisiwachukie nizidi kuwapenda.

“Kuwatunza ni kazi ngumu sana kwani mara nyingi wamekuwa wakininyima usingizi kwa sababu wamekuwa wakilala kwa nyakati tofauti.

“Nakumbuka siku niliyojifungua mume wangu alikosa raha lakini sasa anawapenda kwani amejua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.

 “Maisha yetu ni magumu kwani tunatoka kwenye familia maskini, kazi yetu ni kilimo cha kutumia jembe la mkono hivyo bado kuna mahitaji mengi nashindwa kumudu.


Nichukue nafasi hii kuwaomba msaada Watanzania wote walioguswa na tukio hili,” alisema Grace.

Grace alifunga ndoa na Erick William Mwakyusa Desemba 23, 2010 na katika ndoa yao wamejaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Lide (3) na hao mapacha ni uzao wake wa pili.

Mama huyo anaomba msaada kwa mtu yeyote aliyeguswa na habari hii atume mchango wake kupitia namba 0753308525 ambayo ni ya mumewe au aende kumuona Muhimbili.

Askari Polisi 114 watimuliwa kazi, kisa....!

http://2.bp.blogspot.com/-HFY83aRnIf0/UQlOtZQQmPI/AAAAAAAAAKw/J1v9b9t_vE4/s640/12-Naibu+Waziri+wa+Mambo+ya+Ndani+ya+Nchi+Pereira+Ame+Silima+akijibu+hoja+mballimbali+za+wizara+yake+Bungeni.JPG
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima
http://www.gushit.com/files/bookmark_photos/8e1effe441L.jpg
IGP, Said Mwema

JUMLA ya askari  wa 114 wa Jeshi la Polisi wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa maadili ya kazi zao na baadhi yao wakiwa wamefikishwa mahakamani katika kipindi cha mwaka 2007-2010.
Takwimu hizi zimefichuliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima wakati  akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM), Jaku Hashim Ayoub.
Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kudhibiti vitendo vya baadhi ya askari kuwabambikia kesi raia kinyume na misingi ya haki za binadamu.
Pia alitaka kujua serikali imewachukulia hatua gani za kinidhamu na kisheria askari waliojihusisha na vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa askari wengine.
Akijibu, Silima alisema serikali ina mikakati ya kukabiliana na kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora pamoja na vitendo vya baadhi ya askari kuwabambikia kesi na kuwatishia raia ili wasifuatilie kesi zao vituoni.
“Kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 jumla ya askari 114 wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa maadili na maadhi yao wamefikishwa mahakamani” alisema.
Hata hivyo, alisema mafanikio ya jeshi la polisi yanategemea upatikanaji wa taarifa za matukio hayo kutoka kwa wananchi ambao wanatendewa vitendo hivyo na baadhi ya askari ambao siyo waaminifu.

Hivi karibuni askari karibu 10 nchini waliripotiwa kutimuliwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwemo wale waliokuwa wakitumia fuvu la mtu kuwapakazia kesi wananchi katika mkoa wa Morogoro.

Mwantumu Mahiza aapishwa kuwa Skauti Mkuu wa Tanzania

 Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania mteule Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijiandaa kuvishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi baada ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Jaji Kiongozi Fakih Jundu na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na viongozi wa maskatu na skauti  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza na familia yake baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na waheshimiwa wabunge ambao ni maskauti  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na skauti Ismail Aden Rageh na wabunge maskauti  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na wanachama wa UWT wilaya ya Ilala  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza na viongozi wa skauti nchini baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na skauti Livingstone Lusinde ambaye pia ni Mbunge wa Mtera  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013

Majambazi waua walinzi wawili wakipora fedha kituo cha mafuta

Kaimu Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Njombe, Focus Malengo

WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wamewaua kwa kuwapiga risasi walinzi wawili  wa kampuni binafsi ya ulinzi ya Makambako Security Guard katika mji mdogo wa Makambako mkoani Njombe.
Tukio hilo lilitokea jana saa 12:30 asubuhi baada ya watu hao kuvamia kituo cha kuuzia mafuta cha Oryx cha mjini hapa.
Walinzi waliouawa wametajwa kuwa ni Chesco Mpogole (30) na Damas Sanga (28), wakazi wa Ubena na Uhuru mjini hapa.
Mbali na watu hao kuuawa, pia majambazi hayo yamemjeruhi vibaya Meneja wa Kituo hicho, Jonas Msengi (43), mkazi wa Mji Mwema ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Ilembula kwa matibabu.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Njombe, Focus Malengo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda Malengo alisema majambazi hayo yalivamia kituo hicho kwa kutumia usafiri wa pikipiki na kujifanya wateja wa kununua mafuta.
“Lakini wakiwa tayari wameuziwa mafuta ya Sh. 5,000, yalitoa noti ya Sh. 10,000, hivyo mhudumu aliyewahudumia Ibrahim Manga, alikwenda kwa mwenzake Mwanaidi Kalinga (32) kwa ajili ya kufuata chenji,” alisema Kamanda Malengo.
Aliongeza kuwa wakati jambazi moja likisubiria chenji, mwingine aliwafuata walinzi hao na kuwashambulia kwa kuwapiga risasi na kusababisha vifo vyao papo hapo.
Kamanda Malengo alisema baada ya kufanya mauaji hayo, majambazi hayo yalimfuata Meneja Msengi, ambaye wakati huo alikuwa akiingia ofisini kwake na kuanza kumshambulia.
“Lakini pia majambazi hayo yalipora kiasi cha kati ya Shilingi milioni sita na saba kwa taarifa za awali kwani wamiliki wa kituo hiki wanaendelea kufanya hesabu zao,” alisema Kamanda Malengo.

After Death ya Kanumba kuachiwa hadharani Julai 30

http://2.bp.blogspot.com/-OipoVBqCZ9g/UWUMhWxHuuI/AAAAAAAAFmw/UGvIWQeSRBk/s1600/Kanumba1.jpeg

FILAMU iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo 'After Death' na iliyozinduliwa rasmi katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu msanii huyo aage dunia inatarajiwa kuachiwa mtaani mwezi ujao.
Filamu hiyo iliyotungwa na tayarishwa na msanii Jacklyne Wolper na kuongozwa na Leah Richard 'Lamata' ilipangwa kutolewa mwezi huu wa Juni, lakini Lamata aliiambia MICHARAZO kwamba kazi hiyo itaachiwa rasmi Julai 30 mwaka huu.
Lamata alisema wameamua kusogeza muda wa kuiingiza sokoni kutokana na foleni kubwa iliyopo kwa wasambazaji na pia kujipanga kuweza kuwafikia mashabiki karibu wote nchini, ikiwa ni siku chache baada ya kuiachia hadharani filamu ya "my Princess'.
"Baada ya kuachia 'My Princess' tunajipanga kuitoa hadharani 'After Death' filamu maalum iliyotengenezwa kwa ajili ya kumuenzi Kanumba, tumepanga kuiachia Julai 30," alisema Lamara.
Ndani ya filamu hiyo imeshirikisha wasanii chipukizi walioibuliwa na marehemu Kanumba kama Patrick na Jennifer, wamo pia Branco, Uncle D, Shamsa Ford, Wolper, Mainda, Patcho Mwamba, Stanley Msungu na wengine ambao walikuwa wakiigiza na msanii huyo.
Kanumba alifariki Aprili 7 mwaka jana baada ya kuanguka katika kilichoelezwa ugomvi baina yake na mpenzi wake, Elizabeth Michael 'Lulu'  na kuacha majonzi kwa mashabiki na wale waliokuwa wakifanya naye kazi kutokana na ufanisi wake katika tasnia ya filamu na uigizaji kwa ujumla.

Jordi Alba ajishangaa kuwa 'Man of the Match'

http://en.rian.ru/images/17604/24/176042404.jpg

BEKI wa timu ya taifa ya Hispania, Jordi Alba amejishangaa kwa kuweza  kufunga mabao mawili na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi baada ya kuisaidia timu yake kushinda 3-0 dhidi ya Nigeria katika mechi yao ya mwisho ya makundi ya Kombe la Mabingwa wa Mabara 2013 juzi usiku.
Mlinzi huyo wa kushoto wa Barcelona alifunga goli kali la juhudi binafsi mapema kipindi cha kwanza kabla ya kutupia la tatu baada ya kukimbia kutokea katikati ya uwanja na kumpiga chenga kipa Vincent Enyeama katika dakika za mwisho.
"Si kawaida kwangu kufunga magoli mawili katika mechi moja," Alba aliwaambia waandishi wa habari. "Nadhani hii ni mara ya kwanza.
"Hii ni mpya kwangu, kwa sababu, kama ulivyosema, mara nyingi tuzo hii (ya mchezaji bora wa mechi) hupewa washambuliaji au wale walio mbele katika mechi kubwa. Najivunia kupata tuzo hii."
Kocha Vicente del Bosque alilalamikia hali ya hewa mjini Fortaleza Jumapili jioni, na Alba alikiri kwamba joto limekuwa likiziathiri timu katika michuano hiyo.
"Tulisikia joto katika mechi nzima, ilikuwa ni joto sana," aliendelea. "Miguu yako inaungua... Lakini iko hivyo kwa timu zote."
Hispania sasa itacheza dhidi ya Italia katika nusu fainali katika mechi ambayo ni kama marudio ya fainali ya Euro 2012, ambayo Hispania ilishinda 4-0, lakini Alba amesisitiza kwamba timu yake ni lazima iwe katika kiwango cha juu ili kuishinda timu ya kocha Cesare Prandelli.
"Dhidi ya timu kama Italia hujui nini kitatokea," alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. "Wanajipanga vyema nyuma na wanajua kukaa na mpira.
"Watakuwa wagumu kwetu, kama ambavyo wamekuwa kila siku. Tunapaswa kudumusha staili yetu ya kucheza na kutoruhusu magoli nyuma."

Shasta aonja utamu wa penzi la H-Mbizo


MUIGIZAJI wa kike wa filamu nchini, Leah Mussa 'Shasta' amefuata mkondo wa shoga zake Shilole na Snura kwa kujitosa kwenye muziki akikamilisha wimbo wake wa kwanza uitwao 'Utamu wa Penzi' ambao amemshirikisha Hamis Mbizo 'H-Mbizo'.
Akizungumza na MICHARAZO Shasta alisema wimbo huo upo hatua ya mwisho kabla ya kukamilika akiwa ameurekodia katika studio za prodyuza More Fire aliyetengeneza wimbo wa Snura uitwao 'Majanga'.
Alisema kuingia kwake kwenye muziki siyo kwa kubahatisha kwani tangu utotoni alikuwa akijishughulisha na muziki akiimba kanisani na shuleni na mpaka sasa yeye ni mwalimu wa muziki na anaimba kwaya ya kanisa lake la Sabato, ila hakuifanya kazi hiyo  kibiashara kutokana na kutingwa na majukumu ya uigizaji wa filamu.
"Wengine wanaweza kuhisi landa nimevamia fani ya uimbaji, hapana mimi ni mwanamuziki kamili nikianza kuimba kanisani na shuleni tangu nikiwa mdogo na hata sasa naimba kwaya kanisani, ila kwa vile nataka kuwaonyesha wengine kwamba watu tuna vipaji zaidi ya kimoja ndiyo maana nimeamua kutoka na wimbo huo wa 'Utamu wa Penzi' kisha kufuatiwa na nyimbo nyingine," alisema Shasta.
Nyota huyo wa filamu ya 'Kisasi cha Mzimu', 'Julia', 'Deception', 'Ongwana', Pete ya Ajabu na nyingine, alisema mara baada ya kuachia hewani wimbo huo klabla ya kuanza kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani unaoanza wiki mbili zijazo ataanza mipango ya kukamilisha video yake kabla ya kutoa kazi mpya hapo baadaye.

Kipemba, Mapigo 7 wahamasisha ulipaji kodi Ujiji-Kigoma


      
Msanii Yasini Mapigo Saba akiwa na Issa Kipemba
    
MUIGIZAJI nyota wa zamani wa kundi la Kaole Sanaa, Issa Kipemba 'Kipemba' akishirikiana na msanii Yassini  Mapigo Saba wa mkoani Kigoma, wameendesha kampeni ya kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa wakazi wa manispaa ya kigoma Ujiji.

Kampeni hizo zilizoambatana na burudani ya ngoma asilia, vichekesho na uigizaji, ziliandaliwa na ofisi ya Manispaa ya mji huo wa Ujiji –Kigoma kupitia mradi wa Tanzania Strategic Cities Project (TSCP) chini ya Mstahiki Meya Bakari Beji.

Alisema alijikuta akishiriki kampeni zilizoambatana na utoaji wa elimu ya ulipaji wa kodi za manispaa hiyo kwa ajili ya kuongeza chachu ya maendeleo alipoenda kwa likizo fupi na kama msanii alijiona ana dhima ya kuisaidia jamii yake.

"Nilikuwa nimeenda kusalimia nyumbani na kukuta uhamasishaji huo na mie kushiriki kama msanii na mwenyeji wa Ujiji na tumefanya kazi kubwa nikishirikiana na msanii mkongwe wa Kigoma, Mapigo Saba," alisema.

Naye mstahiki meya wa manispaa ya Kigoma ujiji  alithibitisha kufanyika kwa kampeni hizo akidai zilikuwa zina lengo la kuchochea hamasa kwa wakazi wa mji huo kujenga tabia ya kulipa kodi zilizopo katika manispaa yao ili kuongeza kasi ya maendeleo ya manispaa yao.

"Ni kweli Kipemba na wasanii wengine akiwamo Mapigo Saba walikuwa hapa kuendesha kampeni ya elimu na uhamasishaji wa ulipaji wa kodi za manispaa na kwa kiasi kikubwa wamefanya kazi kubwa na tunasubiri utekelezaji toka kwa wananchi," alisema  Mstahiki Meya Beji.

Aidha mweka hazina wa manispaa hiyo ndugu Edward Malima alianisha kodi zilizoahamasishwa kwa wananchi wa Kigoma - Ujiji kuwa ni pamoja na kodi za Majengo, Ushuru wa Huduma ya Mji, Maegesho ya magari, Masoko na Vizimba, Hoteli na Nyumba za wageni (guest), na Mabango ya Matangazo.

Ndugu Malima alitilia mkazo kwa kutofautisha kodi za maegesho ya magari na ile ya Stendi za mabasi ambapo alitanabahisha umuhimu wa ulipaji wa kodi hizo kwa ustawi na maendeleo ya mji wa Kigoma Ujiji huku akitoa mifano lukuki ya maendeleo ya sasa ya manispaa hiyo ukilinganisha na hapo nyuma.

Kipute cha Ligi Kuu msimu wa 2013-2014 kuanza Agosti 24

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2012/11/Vodacom-Premier-League.jpg

PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 unatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu, imefahamika.
Akizungumza jijini jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia, alisema kuwa tarehe hiyo imeshapitishwa katika kalenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na tayari pia mechi za ligi hiyo zimeshapangwa lakini hazijathibitishwa na kamati yake kama taratibu zinavyoeleza.
Karia alisema kuwa tayari 'wataalamu' ambao huhusika na zoezi la kupanga ratiba za mechi wameshakamilisha zoezi hilo lakini kamati yake ndiyo inasubiriwa kupanga siku ya kukutana ili kuithibitisha.
"Ligi itaanza tarehe 24 Agosti ila nani ataanza na nani ndiyo bado hatujapitisha, tukishakutana na kupitia hilo kwa kuzingatia mazingira yetu ya timu kusafiri ndiyo itatolewa hadharani. Tutakuwa makini sana kwa sababu hatutaki makelele yaliyojitokeza mwaka jana na miaka ya nyuma yaendelee," alisema Karia ambaye ameshasema kuwa atawania cheo cha Makamu wa Rais katika uchaguzi ujao wa shirikisho hilo utakaofanyika Septemba.
Hata hivyo, Karia alisema kuwa suala la wadhamini wa ligi hiyo bado halijakamilika lakini kubwa wanachotaka ni kuona ni klabu zinafaidika na udhamini utakaopatikana.
Alisema kuwa kamati yake inatarajia kukutana Julai 3 asubuhi ili kupitia taarifa za msimu uliopita na kupata washindi wa tuzo mbalimbali na jioni yake washindi hao watatangazwa na kutunukiwa.
"Tumepanga tukutane siku hiyo hiyo ya tuzo ili habari zisivuje, kwa sababu kila mtu na kifua chake cha kuweka mambo…  hadi sasa ni bingwa, mshindi wa pili na wa tatu ndiyo wanajulikana. Lakini kocha bora na tuzo nyingine tutajua siku hiyo baada ya kuangalia na kuthibitisha rekodi tulizonazo," aliongeza Karia.
Kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, bingwa mtetezi Yanga na mshindi wa pili, Azam watakutana katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kama kanuni za ligi zinavyosema.
Timu 14 za msimu ujao wa ligi ni pamoja na Yanga, Azam, Simba, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Coastal Union, JKT Oljoro, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Mgambo Shooting, Prisons na zilizopanda daraja ambazo ni Mbeya City, Ashanti na Rhino Rangers ya Tabora.

NIPASHE

TFF yamlilia Mathias Kissa yaipa pole Cosmopolitan

http://4.bp.blogspot.com/-9Gyrke_foMI/UOHTImoa4mI/AAAAAAAAe3Q/t1bVgNQl8hA/s320/tff_LOGO.jpg
Na Boniface Wambura
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Cosmopolitan na Taifa Stars, Mathias Kissa (84) kilichotokea leo alfajiri (Juni 24 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani enzi zake, Kissa akiwa na timu ya Tabora alitamba katika michuano ya Kombe la Taifa wakati huo ikiitwa Sunlight Cup. Alikuwa akicheza katika nafasi ya ulinzi.

Baadaye alijiunga na Cosmoplitan ya Dar es Salaam, na pia kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambapo enzi zake akiwa na wachezaji kama Yunge Mwanansali wakiiwakilisha Tanganyika na baadaye Tanzania Bara walitamba katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati huo ikiitwa Gossage, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

Kissa ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora wa karne kwa upande wa Tanzania, tuzo inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) alikuwa ndiye mchezaji msomi kupita wote wakati akichezea timu ya Taifa akiwa amehitimu elimu ya Darasa la Kumi.

Kwa mujibu wa binti yake, Erica, marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alioupata miaka mitano iliyopita, na kisukari. Baadaye alipata kidonda ambacho ndicho kilichosababisha kifo chake.

Msiba uko nyumbani kwa marahemu, Masaki, Mtaa wa Ruvu karibu na Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Maziko yatafanyika keshokutwa, Jumatano (Juni 26 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kisa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Cosmopolitan na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Kisa mahali pema peponi. Amina