WAFANYABIASHARA ndogo ndogo (Machinga) waliokuwa wamehodhi eneo la Manzese wametimuliwa ikiwa ni muendelezo wa kusafisha jiji hasa katika kipindi hiki cha ujio wa Rais wa Marekani, Barrack Obama.
Hata hivyo taarifa za chinichini toka kwa baadhi ya watendaji wa Manispaa ya Kinondoni ni kwamba machinga hao wameondolewa kutokana na mkandarasi anayetengeneza barabara ya Morogoro kupata wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yake kutokana na eneo kubwa kujaa wachuuzi hao kiasi cha kuwafanya wafanye kazi zao katika mazingira magumu.
MICHARAZO ilipita nyakati za mchana na kushuhudia barabara hiyo ikiwa nyeupe kukiwa hakuna biashara yoyote inayofanyika zaidi ya doria ya magari ya askari polisi, mgambo na walinzi shirikishi wengine, huku vijana waliozoea kuendesha biashara zao wakiwa wanawaangalia kwa chuki askari hao kwa kuwasababishia wakose riziki kwa doria wanalofanya.
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika eneo hilo walionyesha kuunga mkono operesheni hiyo kwa sababu imewafanya watembee kwa kujinafasi japo wengine walikuwa wakihisi kutumuliwa kwa machinga hao kunaweza kusababisha hali ya uhalifgu kukithiri mitaani kwani vijana hao watakosa kazi za kuwaingizia riziki kama walivyokuwa wakifanya
No comments:
Post a Comment