STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 26, 2013

Wakazi Ujiji wahimizwa kujenga tabia ya kulipa kodi

Mstahiki Meya wa Ujiji-Kigoma, Bakari Husseni Beji (kushoto) 

UONGOZI wa Manispaa ya Mji wa Ujiji mkoani Kigoma umewahimiza wakazi wa mji huo kujenga tabia ya kupenda kulipa kodi za manispaa hiyo kwa hiari kwa ajili ya kujiletea maendeleo badala ya kusubiri kushurutishwa.
Aidha Manispaa hiyo ilijikadiria kwa mwaka huu unaomalizika Juni 30 kukusanya jumla ya Sh Bil 1.3 kupitia vyanzo vyake vya fedha, lakini ikidai mpaka sasa lengo hilo halijatimia kutoka na wakazi wengi wa mji huo kuwa wagumu katika ulipaji wa kodi hasa zile za Majengo.
Akizungumza na MICHARAZO Mstahili Meya wa Manispaa ya Ujiji, Bakari Beji alisema uongozi wao umekuwa na wakati mgumu katika kukusanya kodi toka kwa wananchi wao kutokana na wengi wao kutokuwa na tabia ya kulipa kodi.
Mstahiki Meya huyo alisema kutokana na hali hiyo wamekuwa wakishindwa kufikia malengo ya kimaendeleo waliyojiwekea kutokana na tabi ya wakazi wa mji huo kushindwa kulipa kodi kwa hiari wakidhani fedha hizo zinahishia mikononi mwa watu, ingawa ukweli ndizo zinazosaidia huduma za kijamii.
Alisema kwa mfano kwa kipindi cha bajeti cha mwaka unaomalizika Juni 30, walikadiria kukusanya jumla ya Sh. Bil 1.3, lakini mpaka sasa japo bado hawajakaa chini kutathimini wamebaini lengo lao halijafikiwa kwa ufanisi.
"Kumekuwa na ugumu kwa wakazi wa mji wetu kulipa kodi hasa hizi za majengo, hivyo tunawahimiza wananchi hao kujenga tabia ya kulipa kodi hizi kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na mji wao kwa ujumla," alisema.
Mstahiki Meya huyo alisema pamoja na kwamba mara kadhaa wamekuwa wakitumia nguvu kulazimisha wakazi hao kulipa kodi wameona bado hajawajafanikiwa hivyo wameona boira watumie elimu ya uhamasishaji zaidi ili kuwaelimisha wananchi hao kujua umuhimu wa ulipaji wa kodi hizo.
"Tumeanza kuendesha kampeni za kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi kwa kutumia njia mbalimbali, tunaamini wakazi hao watabadilika na kusaidia kuiwezesha Manispaa yao kupata fedha na kuwaletea maendeleo ya kijamii," alisema Meya Beji.
Alisema Manispaa yao inapata ugumu katika ukusanyaji wa kodi ya majengo kuliko zile za Ushuru wa Masoko na Vizimba,Maegesho ya Magari, Ushuru wa Huduma ya Mji, Hoteli na Nyumba za Wageni na Mabango ya Matangazo.

No comments:

Post a Comment