STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 26, 2013

Ancelotti achekelea kutua Real Madrid

Kocha Carlo Ancelotti
KOCHA Carlo Ancelotti amefunguka na kusema uteuzi wake wa kuinoa timu ya Real Madrid kumehitimisha ndoto zake za muda mrefu kuwa kweli.
Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 54 amesaidia mkataba wa miaka mitatu wa kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutambulishwa rasmi leo Jumatano.
Aidha kocha huyo ameweka wazi hana mpango wa kustaafu mapema badala yake angependa kuendelea kuwepo Santiago Bernabeu kwa muda mrefu zaidi.
"Naupenda mpira wa miguu na kwanini Real Madrid imekuwa klabu ya ndoto yangu, na nashukuru leo ndoto hiyo imekuwa kweli," alisema Ancelotti.
"Sidhani kama Real Madrid itakuwa ndiyo mwisho wangu wa kufundisha, lakini nina matumaini nitakuwepo hapa kwa muda mrefu," alisema kocha huyo aliyewahi kuzinoa timu za Ac Milan na Chelsea.
Kocha huyo alijibu kiungwana alipotupiwa swali kutaka kulinganishwa na Jose Mourinho aliyempokea mikoba yake Madrid kwa kusema yeye na Mourinho ni makocha tofauti, japo anaendelea kumheshimu.
"Niko tofauti kiwasifu na Mourinho, lakini naendelea kumheshimu mno," alisema.

No comments:

Post a Comment