STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 26, 2013

Barbatov haendi kokote atasalia Fulham

Dimitar Barbatov
WAKALA wa mshambuliaji wa zamani wa Manachester United, Dimitar Berbatov, Emil Danchev amethibitisha kuwa nyota huyo atasalia kwenye klabu yake ya sasa ya Fulham kwa msimu ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 na aliyesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ilidaiwa alikuwa katika mipango ya kujiunga na klabu ya Zenit St Petersburg waliovutiwa naye.
Hata hivyo danchev alisema mkali huyo aliyewahi pia kukipiga Tottenham kabla ya kutua United ataendelea kusalia katika klabu hiyo.
"Ana mkataba wa  mwaka mmoja zaidi na Fulham na atasalia hapa mpaka mtakata utakapoisha, " alisema wakala huyo na kuongeza;
"Anajisikia furaha hapa Fulham na anataka kubaki kwa mwaka mmoja zaidi. Hataki kujadili suala la klabu nyingine kwa sasa. Hata kama kuna klabu zinamhitaji binafsi anafurahia kuwepo kwake Fulham na anataka kusalia hapa. Anataka kucheza angalau zaidi ya miaka miwili."
Berbatov ameifungia Fulham mabao 15 katika Ligi kuu kwa msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Manchester United.

No comments:

Post a Comment