STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 21, 2013

Chelsea, Mourinho wapumua, Liverpool ikifa nyumbani EPL

Oscar
Oscar akishangilia bao lake jioni hii
Beki Lavren akiitungua Liverpool kwa kichwa

VIJOGOO vya England, Liverpool leo wamejikuta wakiiangukia pua wakiwa uwanja wao wa nyumbani wa Anfield baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Southampton, na kuipisha Chelsea iliyozinduka leo kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao wa Fulham kukaa kileleni mwa msimamo.
Liverpool iliyokuwa haijaonja chungu ya kipigo katika mechi nne zilizopita za Ligi Kuu ya England ilitunguliwa bao hilo lililofungwa na Dejan Lavren katika dakika ya 53 na kuzima ubabe wake wa kuwafunga wenzake.
Nayo Newcastle United ikiwa nayo nyumbani ilicharazwa mabao 3-2 na Hull City, licha ya kuongoza hadi mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Chelsea muda mchache uliopita imetoka kupata ushindi kwa kuilaza Fulham kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa na Oscar katika dakika ya 52 na Obi Mikel aliyefunga la pili dakika sita kabla ya pambano hilo lililochezwa Stanford Bridge kumalizika na kumpa afueni kocha Jose Mourinho.
Mechi nyingine za ligi hiyo ya England, Everton ikiwa ugenini imeisulubu West Ham kwa mabao 3-2 nayo Sundeland ikiwa ugenini imetandikwa mabao 3-0 na West Brom na Aston Villa ikiizima Norwich City ikiwa kwake kwa bao 1-0.
Kipute cha ligi hiyo kinatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo nne, Arsenal itakuwa ikiufukuzia uongozi wa ligi hiyo baada ya kuenguliwa wiki iliyopita na Liverpool itaikaribisha Stoke City, Manchester City itakuwa nyumbani kuialika Manchester United, Tottenham Hotspur watasafiri hadi nyumbani kwa Cardiff City na Crystal Palace wataikaribisha Swansea City.

Mbeya City yapunguza kasi Msimbazi, Tambwe aendelee kufumania nyavu, Ashanti yaendelea kuwa mdebwedo


Mbeya City wakiomba dua
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi003q9axgmcyEwn769yPSk0p-qvp7iBWnxb70zu3q8AEvcVy2CrW_ALBPLt_ui4VS13-PzWbTpfaDxDBACnTatNnxlIyckN4u5SXDOATdaTiRtWevZ5goB1IekVocBA9ddoiZP-GkDw90/s400/kikosi1.JPG
Kikosi cha Simba

LILE 'fupa' lililowashinda Yanga kulitafuta, Mbeya City imedhihirisha wapo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kikazi baada ya jioni ya leo kuibana mbavu Simba na kwenda nao sare ya mabao 2-2 kwenye uwanja wa Taifa, huku mshambuliaji nyota toka Burundi, Tambwe Amissi akiendeleza libeneke lake kwa kufumania nyavu.
Simba ambayo hata hivyo inaendelea kukalia uongozi wa msimamo wa ligi hiyo ilishindwa kulinda mabao yake mawili yaliyofungwa na Tambwe katika kipindi cha kwanza na kuwapa mwanya 'wageni' Mbeya City kuyarejesha na kupata ponti yake ya pili ugenini.
Tambwe alifunga bao la kwanza dakika ya 22 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 33 na kumfganya afikishe jumla ya mabao sita na kuwaacha mbali wafungaji wenzake wanaomfukuzia kwenye orodha ya wafumania nyavu.
Hata hivyo Mbeya inayonolewa na kocha mzoefu, Juma Mwambusi ilijipatia bao la kwanza dakika nne baada ya kufungwa bao la pili na Simba kupitia Paul Nonga na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe 2-1.
Kipindi cha pili kilishuhudiwa kosa za hapa na pale kwa timu zote na hasa Mbeya kuonyesha kucharuka na katika dakika ya 69, Richard Peter aliisawazishia timu yake bao la pili na kuifanya Simba ipoteze umakini wake na kama siyo papara za washambuliaji wa Mbeya huenda wangeweza kuibuka na ushindi leo Taifa.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Mgambo JKT ikiwa uwanja wa Mkwakwani ililazimishwa sare ya bao 1-1 na maafande wenzao wa Rhino Rangers ya Tabora. Bao la wenyeji lilifungwa na Mwalimu Musuku dakika ya 60 kabla ya Rhino kuchomoa dakika za jioni kupitia Hamis Msafiri.
Nayo timu ya Prisons Mbeya imeendelea kujikongoja baada ya kuambulia sare ya pili mfululizo dhidi ya Mtibwa Sugar, mechi iliyochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya, wageni wakianza kupata bao kupitia nahodha Shaaban Nditti aliyefunga kwa kichwa dakika ya 26 akiiunganisha mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa na Said Mkopi kabla ya wenyeji kuchomoa bao dakika ya 58 kupityia kwa Peter Michael.
Kagera Sugar ikiwa uwanja wake wa Kaitaba, Bukoba iliishindilia bila huruma 'vibonde' wa ligi hiyo Ashanti United ya Dar kwa mabao 3-0. Mabao ya washindi yalitupiwa kimiani na Daud Jumanne, Seleman Kibuta na Clement Douglas.
 Kivumbi cha ligi hiyo kitaendelea kesho kwa mechi tatu zitakzaochezwa viwanja vitatu tofauti jijini Dar mabingwa watetezi watapimana ubavu na Azam watakaokuwa wenyeji, huku mjini Tanga Coastal Union itapepetana na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mkwakwani na JKT Ruvu itawalika Oljoro JKT.

Simba, Mbeya City nini bwana, ngoma kesho Yanga vs Azam

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPnNutozTJ6LUNDdmv05v7BvLNYLIQ6dp4CQ2ET3L3oazDgFevrgY8oyJQYiRwp0q85aEDxXie6rSVYqBOkl6hngu5QSM5xh24P58eJEep1bVkTQhE8P0a20N1ChhRt5YTQlf4pHuVo4dH/s1600/MWAIKIMBA.jpg
Wachezaji Azam wakishangilia mabao yao

WAKATI Mbeya City ikiwa na kibarua kigumu mbele ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, macho na masikio ya mashabiki yapo kwenye pambano la kesho kati ya mabingwa watetezi Yanga na makamu bingwa, Azam zitakazopepetana kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Yanga wakishangilia moja ya mabao yao
Simba na Mbeya zinaumana leo pia kwenye uwanja huo katika mfululizo wa ligi hiyo utakaoshuhudiwa pia mechi nyingine tatu katika miji tofauti.
Hata hivyo mashabiki wa soka watakuwa na hamu kubwa ya kushuhudia pambano la Yanga na Azama ambazo zote zimeshindwa kuonyesha makeke katika mechi zake mbili zilizopita.
baada ya kubanwa mbavu jijini Mbeya ikilazimishwa sare mbili mfululizo dhidi ya wenyeji wao Mbeya City na Prisons, Yanga kesho inarejea katika dimba lake la nyumbani kujaribu bahati yake tena kwa Azam.Azam nao kama ilivyo kwa Yanga imetoka kuambulia sare mbili dhidi ya Kagera Sugar na Ashanti na kujikusanyia pointi sita sawa na ilizonazo Yanga, Mbeya City na Coastal Union.
Pambano hilo la Yanga na Azam ni kati ya mechi tatu zitakazochezwa kesho katika ligi hiyo iliyoingia raundi ya tano, michezo mingine ikiwa ni maafande wa JKT Ruvu na Oljoro JKT zitakazopepetana kwenye dimba la Chamazi, Mbagala Dar es Salaam na ile ya 'Wagosi wa Kaya' Coastal Union itakyokuwa nyumbani uwanja wa Mkwakwani, Tanga kuumana na Ruvu Shooting.
Hata hivyo pamoja na mechi hizo nyingine kuwa na mvuto wake, pambano la Yanga na Azam ndilo linaloangaliwa kwa ukaribu na mashabiki wa soka nchini kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizo kila zinapokutana.
Timu hizo zenye pointi sita kila mmoja zikitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa zitakutana katika pambano lao la 11 la Ligi Kuu tangu 'Wana Lambalamba' wapande daraja mnamo mwaka 2008.
Klabu hizo zimeshakutana katika michuano kadhaa ikiwamo ya Kombe la Mapinduzi, Kombe la Kagame na Ngao ya Hisani ambayo mara ya mwisho walivaana Agosti 17 na Yanga kuitambia Azam kwa bao 1-0, lakini katika mechi za ligi kuu huwa na matokeo mengi ya kushangaza.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo tangu mwaka 2008 Yanga na Azam zimekutana mara 10 katika Ligi Kuu na Yanga kushinda mechi tano na Azam ikishinda mechi tatu huku michezo yao miwili ikiishia kwa sare.
Hivyo katika pambano hilo klabu hizo zitakuwa zikifukuzia nafasi ya kuvuna pointi tatu na wakati huo huo kulinda au kuboresha rekodi yao dhidi ya mwenzake, huku wadau wa soka wakitaka kuona kama wafungaji bora wa msimu uliopita nani anatayemfunika mwenzake.
Kipre Tchetche wa Azam ndiye aliyeongoza orodha ya wafungaji bora kwa kufunga mabao 17 na amezinduka majuzi baada ya kufunga bao lake la kwanza, huku aliyeyemfuata msimu uliopita, Didier Kavumbagu tayari akiwa na mabao mawili kibindoni mpaka sasa.
Kadhalika ni mechi itakayokuwa ikishindanisha makocha wawili wa kigeni wenye rekodi nzuri kwa msimu uliopita, Ernie Brandts wa Yanga aliyeiongoza Yanga kwa mechi zaidi ya 24 bila kufungwa tangu walipolala bao 1-0 toka kwa Kagera Sugar msimu uliopita.
Kocha wa Azam, Muingereza, Stewart John Hall, yeye naye atataka kulipa kisasi kwa mpinzani wake ambaye amemtambia kwa msimu uliopita katika mechi zote za ligi na majuzi kwenye ngao ya Hisani.
Je ni Yanga au Azam itakayocheka au Kipre Tchetche atakayemtambia Didier Kavumbagu ama ni kocha Brandts kuendelea kumfunika Stewart? Tusubuiri tuone.
Rekodi za Yanga na Azam katika Ligi tangu 2008:
Oktoba 15, 2008
Yanga 3-1 Azam
Aprili 8, 2009
Azam 3-2 Yanga
Oktoba 17, 2009
Azam 1-1 Yanga
Machi 7, 2010
Yanga 2-1 Azam
Oktoba 24, 2010
Yanga 0-0 Azam
Machi 30, 2011
Yanga 2-1 Azam
Septemba 18, 2011
Azam 1-0 Yanga
Machi 10, 2012
Azam 3-1 Yanga
Novemba 4, 2012
Yanga 2-0 Azam
Februari 23, 2013
Yanga 1-0 Azam
Sept 22, 2013?

Masogange, Melisa waachiwa huru hatimaye

http://api.ning.com/files/It3-odgnrfRW80PWalq53lRwVSPptJtp*DOsLRl-yTPt24Tlnfb-fOv0Dzh6ppWTIjHud9Q--mi-9R3wu5ArUT7KY4Lt9FlD/MASOGANGE.jpg?width=450
Masogange
WATANZANIA wawili Agness Gerard ‘Masogange’ na Melissa Edward wameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg baada ya kutakiwa kulipa faini ya Sh 4.8 milioni (Randi 30,000) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumiwa kutengeneza dawa za kulevya.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini (hawk) Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo mahakama ilibaini kuwa Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana amemsindikiza Masogange, aliyemuomba amsaidie kubeba mzigo huo.
Mosagange alilipa faini ya Shilingi 2.5 milioni (R15, 000), huku akiahidi kumaliza nusu yake ambayo juhudi zilikuwa zinafanyika amalize kulipa jana Ijumaa.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kusaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini haikuwa mizigo yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Masogange na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimuomba amsaidie mizigo hiyo kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela miezi 30 (miaka miwili na miezi sita) au alipe faini ya R30, 000(Sh 4.8 milioni).
Hata hivyo alilipa faini na nusu ya fedha hizo ilishalipwa na nyingine ilikuwa inakaribia kulipwa.
Ingawa Kamishana Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi Alhamisi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS) Marika Muller, alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5, mwaka huu ni methamphetamine.

MWANASPOTI

Amani Simba aanza tambo Ashanti United

Amani Simba
KIPA mpya wa Ashanti United, Amani Simba ametamba kwamba bado muda mfupi tu kabla ya mashabiki wa soka kuikubali timu yao ambayo imeanza vibaya Ligi Kuu Tanzania Bara kiasi cha kuruza mkia katika msimamo wa ligi hiyo.
Aidha kipa huyo alisema ni mapema mno kuanza kuitabiria ligi ya msimu huu kwa sababu anaamini lolote linaweza kubadilika kwa sasa kutpkana na ukweli ligi ndivyo kwanza ipo raundi ya nne kwa sasa.
Simba aliyeidhinishwa hivi karibuni na TFF kuidakia timu hiyo baada ya kuitema timu aliyoipandisha daraja ya Mbeya City, alisema Ashanti inasumbuliwa na ugeni wa ligi, ila kadri siku zinavyosonga mbele wachezaji wataizoea na kutisha.
Kipa huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Moro United, Simba na Taifa Stars alisema ni mapema mno kuanza kuihukumu Ashanti na matokeo iliyopata kwa sasa kwa sababu ligi bado mbichi na wachezaji wao wanaendelea kuizoea ligi hiyo.
"Ni mapema mno kuijadili Ashanti, naamini muda mfupi ujao wanayoibeza wataikubali baada ya kuanza kupata matokeo mazuri, unajua ugeni wa ligi ndiyo tatizo lakini kadri siku zinavyoenda mbele wachezaji wanaondoa woga," alisema.
Simba, aliyewahi pia kuzidakia Lipuli Iringa, Prisons Mbeya na JKT Ruvu, alisema akishirikiana na wenzake watahakikisha Ashanti inafanya vyema katika mechi zilizopo mbele yake.
Ashanti United inayoburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa pointi moja ni kati ya timu tatu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu, nyingine zikiwa ni Mbeya City na Rhino Rangers ya Tabora.

Gaucho bado aliota soka la kulipwa

http://api.ning.com/files/Z311HW*8BLsTaHW*p4y9dVjDgbR8cx2tskdyBtk0ZluRwicT9*Nf2fkCQ3unhX6sg*ce5TuwMHaY4TPmDCzkUwHTqR41EqDZ/GLOBALHUMUD.jpg?width=351
Gaucho
KIUNGO nyota wa klabu ya Simba, Abduhalim Humud 'Gaucho' amesema bado hajakata tamaa na mipango ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi hata baada ya mipango ya kwenda nchini Afrika Kusini kukwama.
Akizungumza na MICHARAZO, Gaucho, aliyerejea tena Simba akitokea Azam aliyoichezea msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema japo ametuliza akili zake kuitumia kikamilifu Simba, bado analiwaza soka la kulipwa.
Gaucho, alisema bado ana kiu kubwa ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na imani yake siku yoyote ataenda nje ksa kuamini ana kipaji na uwezo wa kucheza soka kokote akipata fursa hiyo.
"Sijakata tamaa na soka la kulipwa, bado naamini ipo siku nitaenda nje kwa uwezo wa Muingu kwani yeye ni Muweza na Mpangaji wa kila jambo," alisema Gaucho nyota wa zamani wa Mtibwa Sugar na Taifa Stars.
Hata hivyo Gaucho aliwataka viongozi swa soka nchini kuepukana hali ya kibabaishaji na tabia za kuwawekea kauzibe wachezaji wanapopata nafasi ya kwenda nje ya nchi kusakata kandanda akidai ni faifa kwa taifa.
Mapema mwaka huu Gaucho alifaulu majaribio yake ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini, lakini wakati akiwa katika maandalizi ya kuondoka alitangaza ghafla kutua klabu ya Simba.
Hata hivyo alinukuliwa katika mahojiano na kituo kimoja cha redio kwamba klabu yake ya zamani ya Azam ndiyo iliyomwekea vikwazo kabla ya uongozi wa Azam kukanusha taarifa hizo na kutangaza kuachana naye.

Ile Ile atoa Wazazi akijipanga upya

Msani Ile Ile katika pozi
MSANII anayekuja juu kwenye muziki wa kizazi kipya, Maishani Ndee 'Ile Ile' ameachia kibao kipya kiitwacho 'Wazazi' ukiwa ni wimbo wake wa tatu tangu atumbukie kwenye fani hiyo miaka minne iliyopita.
Wimbo huo na video yake umeanza kuwa gumzo kwenye vituo vya redio na runinga kutokana na maudhui wake na Ile Ile alisema amefarijika na anajipanga kuandaa kazi nyinginje mbili kwa mpigo.
Ile Ile aliyewahi kukimbiza na nyimbo za 'Ileile' alioutoa mwaka 2010 na 'Bora Twende' wa mwaka jana alisema nyimbo ambazo zitafuata baada ya 'Wazazi' ni 'Amani na Upendo' na 'Sheila'.
"Hizi zimeshakamilika kila kitu na wakati wowote naziingiza studio kuzirekodi ili kuendelea kuwapa burudani mashabiki wangu na muziki kwa ujumla," alisema Ileile anayejishughulisha na biashara za nguo na hasa lebo yake ya Ile Ile Wears.
Msanii huyo mwenyeji wa Kondoa, alisema angetamani kutoa albamu yake ya kwanza, lakini soko la muziki kwa sasa nchini linamtisha na hivyo anaona bora aendelee kurtoa 'singo' moja moja na video zake ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kupata shoo zitakazomuingiza pato la kutosha.

Steve Nyerere 'ala shavu' kifo cha Baba wa Taifa


MSANII wa filamu nchini, Steve Mangendela 'Steve Nyerere' amepata shavu la kutangaza kwa kutoa hotuba mbalimbali za baba wa taifa zitakazokuwa zikirushwa hewani na  Luninga ya TBC mpaka siku ya kilele cha kifo cha hayati Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Hotuba hizo ambazo zilikuwa zikitolewa na baba wa Taifa sasa Steve Nyerere atakuwa akizitoa kwa kuiga sauti hile hile
Msanii huyo aliyejizolea umaarufu kwa kuiga sauti za viongozi mbalimbali nchini na Duniani kwa ujumla amekuwa akipendwa na wengi kutokana na kuiga sauti ya hayati Baba wa Taifa na kufanya kuchukua jina lake moja kwa moja ambapo kwa sasa popote uendapo uwezi kumwita kwa jina la Steve bali lazima useme Steve Nyerere
Kwa sasa ameingiza kazi yake mpya mtaani inayojulikana kwa jina la Before Wedding ambayo ipo mtaani ikisambazwa na kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dae rs salaam

Bendera 'akiuma' sikio' chama cha Pool kuhusu TBL



 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera(wa pili kushoto), Meneja wa wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa(TAPA), Fred Mushi na Katibu wa chama cha Pool Taifa , Amos Kafwinga wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari National Pool Championships.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (wa tatu kushoto) akipigiwa makofi mara baada kufungua rasmi fainali za mashindano ya Safari National Pool Championship 2013 Mkoani Morogoro. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga, Makamu Mwenyekiti wa chama cha Pool, Fred Mushin a Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.


 Baadhi ya wachezaji wa Pool kutoka mikoa 17 ikiwakilisha na vilabu 17 nchini wakiwa katika maandamano kuelekea katika Ukumbi wa Tanzanite Morogoro wakati wa ufinguzi wa fainali za kitaifa za Safari National Pool Championships.
 Top Land- Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni Dar es Salaam






 Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Safari National Pool Championships, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa tatu kushoto), Mwakilishi wa TBL Morogoro, Julius Ngaga(wa nne kushoto), Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Iringa, Salum Kisaku (wa pili kushoto) na Mwamuzi wa kike pekee, Vaileth Mrema (kushoto)  na baadhi ya wachezaji wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa fainali za Pool Taifa Mkoani Morogoro.
 Na Mwandishi Wetu.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, amewaasa chama cha Pool Taifa(TAPA), kumkumbatia mdhamini mkuu  wa mhezo wa Pool Taifa, “Safari Lager” kupitia Kampuni kubwa nchini Tanzania Breweries(TBL).
Bendera aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano hayo yanayoyofanyika kitaifa Mkoani Morogoro ambapo yeye alialikwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema Bendera, vipo vyama vya michezo vingi vinashindwa hata kufanya mashindano kwa mwaka lakini Pool ni mwaka wa sita sasa mnafanya, vipo vyama vingi vya michezo vinalia kwanini mpira wa miguu peke yake ndio unapata udhamini lakini Pool ni mwaka wa sita sasa mnaye mdhamini na bado mnaendelea nae na baada ya hapa anaipeleka timu ya Taifa kwenye mashindano ya Afrika ya mchezo wa Pool.
Mchezo wowote  ili ukue na kutambulika nchini na Duniani unaanza na mchezaji mwenyewe kuupenda na kuufanya kutoka moyoni kwa kujiheshimu kwanza mwenyewe na kuuheshimu mchezo ndipo hata jamii huudhamini (Self displine and Tactical displine).
Alisema Bendera yeye kama mdao na mzoefu kwenye tasnia ya michezo na mpaka sasa anashikiria sifa kemkem ambazo hazijawahi kutolewa kwenye rekori anauzoefu wa kutosha na maswala ya michezo, siri ya maendeleo katika michezo ni nidhamu pekee na si vinginevyo.
Mtazamo wa mchezo wa Pool katika jamii siku kadhaa hapo nyuma ulionekana kama mchezo wa kihuni lakini leo mmebadilisha taswira hiyo na sasa mko kwenye mikoa 17 ikiwakilisha na vilabu 17 mkiunganisha na mchezo wa Pool mkiwa mkoani Morogoro katika fainali za kitaifa, hongereni sana TAPA.
Mkuu wa Mkoa pia aliipongeza TBL kupita bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mchezo wa Pool na sasa ni mwaka wa sita ambapo aliomba waendelee kudhamini kwani mchezo huu unaunganisha vijana wengi Tanzania kwa hapo walipofikia kwenye mikoa 17,unaepusha mambo mengi maovu ambayo wangekumbana nayo hawa vijana ni zaidi ya vijana 300 wamekutana Mkoa wa Morogoro na kilicho wakutanisha ni mchezo wa Pool.Endeleeni kudhmini mchezo wa Pool kwani kwa sasa michezo ni afya, michezo ni upendo,michezo ni urafiki,michezo ni matangazo na michezo ni afya.
Bendela aliwakaribisha wote Mkoani Morogoro na kuwaomba wawe na amani kwani Morogoro ni shwari kabisa hewa nzuri baridi kiasi.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kujitokeza kufungua fainali hizo na kuahidi lengo la Safari Lager na kuufanya mchezo wa Pool kuwa mchezo namba moja kama ilivyo Safari Lager bia namba moja Afrika hivyo wataenelea kudhamini mashindano ya Pool daima.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi alimsukuru mdhamini Safari Lager kuendelea kuwadhamini na pia kumshukuru Mkuu wa mkoa kwa changamoto alizozieleza za kumlinda mdhamini na kuahidi wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuwaweka sawa vijana kuhakikisha mchezo wa Pool unakuwa chezo namba moja nchini na Afrika kama bia ya Safari Lager.


 Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga akizungumza.
 Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. akizungumza
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool, Fred Mushi akizungumza
 Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akizungumza