STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 21, 2013

Gaucho bado aliota soka la kulipwa

http://api.ning.com/files/Z311HW*8BLsTaHW*p4y9dVjDgbR8cx2tskdyBtk0ZluRwicT9*Nf2fkCQ3unhX6sg*ce5TuwMHaY4TPmDCzkUwHTqR41EqDZ/GLOBALHUMUD.jpg?width=351
Gaucho
KIUNGO nyota wa klabu ya Simba, Abduhalim Humud 'Gaucho' amesema bado hajakata tamaa na mipango ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi hata baada ya mipango ya kwenda nchini Afrika Kusini kukwama.
Akizungumza na MICHARAZO, Gaucho, aliyerejea tena Simba akitokea Azam aliyoichezea msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema japo ametuliza akili zake kuitumia kikamilifu Simba, bado analiwaza soka la kulipwa.
Gaucho, alisema bado ana kiu kubwa ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na imani yake siku yoyote ataenda nje ksa kuamini ana kipaji na uwezo wa kucheza soka kokote akipata fursa hiyo.
"Sijakata tamaa na soka la kulipwa, bado naamini ipo siku nitaenda nje kwa uwezo wa Muingu kwani yeye ni Muweza na Mpangaji wa kila jambo," alisema Gaucho nyota wa zamani wa Mtibwa Sugar na Taifa Stars.
Hata hivyo Gaucho aliwataka viongozi swa soka nchini kuepukana hali ya kibabaishaji na tabia za kuwawekea kauzibe wachezaji wanapopata nafasi ya kwenda nje ya nchi kusakata kandanda akidai ni faifa kwa taifa.
Mapema mwaka huu Gaucho alifaulu majaribio yake ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini, lakini wakati akiwa katika maandalizi ya kuondoka alitangaza ghafla kutua klabu ya Simba.
Hata hivyo alinukuliwa katika mahojiano na kituo kimoja cha redio kwamba klabu yake ya zamani ya Azam ndiyo iliyomwekea vikwazo kabla ya uongozi wa Azam kukanusha taarifa hizo na kutangaza kuachana naye.

No comments:

Post a Comment