STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 21, 2013

Mbeya City yapunguza kasi Msimbazi, Tambwe aendelee kufumania nyavu, Ashanti yaendelea kuwa mdebwedo


Mbeya City wakiomba dua
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi003q9axgmcyEwn769yPSk0p-qvp7iBWnxb70zu3q8AEvcVy2CrW_ALBPLt_ui4VS13-PzWbTpfaDxDBACnTatNnxlIyckN4u5SXDOATdaTiRtWevZ5goB1IekVocBA9ddoiZP-GkDw90/s400/kikosi1.JPG
Kikosi cha Simba

LILE 'fupa' lililowashinda Yanga kulitafuta, Mbeya City imedhihirisha wapo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kikazi baada ya jioni ya leo kuibana mbavu Simba na kwenda nao sare ya mabao 2-2 kwenye uwanja wa Taifa, huku mshambuliaji nyota toka Burundi, Tambwe Amissi akiendeleza libeneke lake kwa kufumania nyavu.
Simba ambayo hata hivyo inaendelea kukalia uongozi wa msimamo wa ligi hiyo ilishindwa kulinda mabao yake mawili yaliyofungwa na Tambwe katika kipindi cha kwanza na kuwapa mwanya 'wageni' Mbeya City kuyarejesha na kupata ponti yake ya pili ugenini.
Tambwe alifunga bao la kwanza dakika ya 22 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 33 na kumfganya afikishe jumla ya mabao sita na kuwaacha mbali wafungaji wenzake wanaomfukuzia kwenye orodha ya wafumania nyavu.
Hata hivyo Mbeya inayonolewa na kocha mzoefu, Juma Mwambusi ilijipatia bao la kwanza dakika nne baada ya kufungwa bao la pili na Simba kupitia Paul Nonga na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe 2-1.
Kipindi cha pili kilishuhudiwa kosa za hapa na pale kwa timu zote na hasa Mbeya kuonyesha kucharuka na katika dakika ya 69, Richard Peter aliisawazishia timu yake bao la pili na kuifanya Simba ipoteze umakini wake na kama siyo papara za washambuliaji wa Mbeya huenda wangeweza kuibuka na ushindi leo Taifa.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Mgambo JKT ikiwa uwanja wa Mkwakwani ililazimishwa sare ya bao 1-1 na maafande wenzao wa Rhino Rangers ya Tabora. Bao la wenyeji lilifungwa na Mwalimu Musuku dakika ya 60 kabla ya Rhino kuchomoa dakika za jioni kupitia Hamis Msafiri.
Nayo timu ya Prisons Mbeya imeendelea kujikongoja baada ya kuambulia sare ya pili mfululizo dhidi ya Mtibwa Sugar, mechi iliyochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya, wageni wakianza kupata bao kupitia nahodha Shaaban Nditti aliyefunga kwa kichwa dakika ya 26 akiiunganisha mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa na Said Mkopi kabla ya wenyeji kuchomoa bao dakika ya 58 kupityia kwa Peter Michael.
Kagera Sugar ikiwa uwanja wake wa Kaitaba, Bukoba iliishindilia bila huruma 'vibonde' wa ligi hiyo Ashanti United ya Dar kwa mabao 3-0. Mabao ya washindi yalitupiwa kimiani na Daud Jumanne, Seleman Kibuta na Clement Douglas.
 Kivumbi cha ligi hiyo kitaendelea kesho kwa mechi tatu zitakzaochezwa viwanja vitatu tofauti jijini Dar mabingwa watetezi watapimana ubavu na Azam watakaokuwa wenyeji, huku mjini Tanga Coastal Union itapepetana na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mkwakwani na JKT Ruvu itawalika Oljoro JKT.

No comments:

Post a Comment