STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 10, 2012

Kazi: 'Konda' aliyeamua kuvunja watu mbavu


Kazi Ukushoto) akiwa na Man BizoKatika pozi zake

Kazi (kulia) akiwa na TabithaKUVUTIWA kwake kisanii na mchekeshaji Amri Athuman 'King Majuto' tangu utotoni, ndiko kulikomfanya msanii Kazi Suleiman 'Kazi' kuamua kuacha kazi ya ukondakta wa daladala awe muigizaji.
Aliingia rasmi katika fani hiyo mwaka 1993 kupitia kundi la Mzimuni Arts kabla ya baadae kuibukia kundi la Africando, ambapo baada ya kuona hajapata kile anachokipata alihamia Al Riyamy Production.
Filamu ya kwanza kumtangaza katika ulimwengu wa sanaa ni 'Olopong' kabla ya kufuatiwa na nyingine zipatazo 20 kwa sasa.
Baadhi ya kazi zake nyingine za mchekeshaji huyo mwenye umbile fupi na anayechekelea kuigiza na wasanii wenye majina makubwa nchini kama Mzee Majuto, Sharo Milionea, Kitale, Senga, Pembe, Man Bizo na wengine ni 'Harusi ya Mwanangu', 'Pedeshee', 'Choo cha Kike' na vichekesho vya 'Vituko Show' vinavyorushwa kwenye runinga.
Kazi ambaye bado hajaoa ingawa anaye mtoto mmoja, anasema sanaa kwa kiasi fulani imemsaidia kwa mengi ikiwemo kufahamika na kujipatia kipato cha kila siku, licha ya kwamba bado hajaridhika.
Matarajio ya mkali huyo aliyezaliwa mwaka 1980 Kawe jijini Dar es Salaam akiwa mtoto wa nne kati ya sita wa familia yake ni kufika mbali kisanii na kuja kumiliki miradi yake binafsi ya kibiashara.
Msanii huyo anayependa kula ugali kwa nyama na mchicha na kunywa Pepsi, anasema sanaa Bongo inalipa ingawa bado wasanii wanashindwa kunufaika na jasho lao kutokana na kukithiri kwa uharamia.
Akaiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia wasanii, sambamba na kuiwekea mipango mizuri fani hiyo ili kuwainua wadau wake sawia na nchi kuvuna pato kubwa linaloendelea kupotea kwa sasa.
Shabiki huyo wa Yanga na Manchester United, naasema hakuna tukio la furaha kwake kama kukubalika kwa mashabiki na anahuzunishwa na vitendo vinavyofanywa na wasanii wenzake hasa suala la skendo.
Anawataka wasanii wenzake kupendana, kushikimana na kujiepusha na yote yanayowachafua wao na familia zao pamoja na fani nzima ya sanaa mbele ya jamii.
Kazi anadai ukiacha Mungu aliyemuumba na kumjalia kipaji cha uigizaji shukrani zake nyingine zinaenda kwa wazazi wake, Mzee Majuto,mkurugenzi wake wa Al Riyamy Production na wasanii wenzake.


TFF YAMPA 'SHAVU' RIDHIWANI KIKWETE

Ridhiwani Kikwete
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys itakayopambana na Congo (Brazaville) katika mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.Uteuzi huo umefanywa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana ya TFF kufanya kikao chake kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na kupeleka mapendekezo yake kwa rais huyo wa shirikisho.
Kutokana na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:

1. Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo

2. Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.

Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
1. Ridhiwani Kikwete                                    Mwenyekiti
2. Ahmed Seif (Magari)                                 Mjumbe
3. Nassoro Bin Slum                                      Mjumbe
4. Henry Tandau                                            Katibu
5. Ahmed Mgoyi                                            Mjumbe
6. Aboubakar Bakhresa                                 Mjumbe
7. Angetile Osiah                                           Mjumbe
8. Kassim Dewji                                             Mjumbe
9. Abdallah Bin Kleb                                     Mjumbe
10. Salim Said                                                Mjumbe

Baada ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Mechi za kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012.


AGGREY MORRIS NAYE ATIMULIWA AZAM 

Aggrey Morris (kushoto) aliyesimamishwa na timu yake ya Azam


BEKI wa Azam FC, Aggrey Morris Ambroce amefukuzwa kwenye kambi ya timu hiyo leo mjini Tanga, baada ya kuthibitika naye alipokea rushwa kutoka klabu ya Simba ili kuihujumu timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Aggrey ameondolewa kambini leo, siku moja tu baada ya kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Said Mourad na Erasto Nyoni nao kusimamishwa kwa tuhuma hizo.
Azam ilifungwa na Simba mabao 3-1 Oktoba 27, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi za Ligi Kuu na baada ya hapo ikamfukuza kocha wake Mserbia, Boris Bunjak na kumrejesha Muingereza, Stewart Hall.
Habari kutoka ndani ya Azam zimesema kwamba baada ya kupata taarifa hizo, uongozi ulizifanyia kazi taratibu na kujiridhisha kabisa wachezaji hao watatu walikula njama za kuihujumu timu katika mechi hiyo.
Kwa sababu hiyo, uongozi kwanza umewasimamisha wachezaji hao na hatua zaidi zitafuatia baadaye.
Hata hivyo, Dida hakucheza mechi hiyo, kwani Oktoba 27, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Ibrahim Shikanda, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz aliyempisha Abdi Kassim, Himid Mao aliyempisha Kipre Balou, John Bocco ‘Adebayor’ aliyempisha Khamis Mcha ‘Vialli’, Kipre Herman Tcheche na Salum Abubakar.
Siku hiyo, Azam walitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka beki Mkenya Paschal Ochieng na kumchambua Juma Kaseja, kabla ya Felix Mumba Sunzu Jr., kuisawazishia Simba dakika mbili baadaye, akiunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.
Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni mwa timu hiyo na Mwinyi Kazimoto na dakika tano tu tangu kuanza kipindi cha pili, Mganda huyo tena akawainua vitini mashabiki wa Simba, akifumua shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Azam.
Habari zaidi zinasema kwamba, uchunguzi unaendelea kufanywa juu ya wachezaji wengine wanaotuhumiwa kuwa katika mkumbo huo wa kuihujumu timu na ikithibitika ni ukweli, watachukuliwa hatua pia bila kujali majina yao.
Azam tayari iko Tanga tangu jana saa 8:00 mchana wa kwa ajili yao ya mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani.

MSONDO NGOMA YAKABIDHIWA VYOMBO VIPYASAID MABELA AKIPOKEA  KUTOKA KWA David Mgwasa


BENDI kongwe nchini ya Msondo Ngoma music band  imekabidhiwa vifaa vya muziki na kampuni ya Konyagi Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Konyagi nchini, David Mgwasa alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania na kuifanya msondo kuwa imara katika kutoa burudani kwa watanzania.

"Msondo ni bendi kongwe tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 imesimama imara katika kutoa burudani ya uhakika kwa watanzania sanjari na kutumia nyimbo zake katika kuelimisha, kufunza jamii ya watanzania walio wengi," alisema Mgwasa.

Alisema watu wengi kwa kuwepo bedndi ya msondo wamewezakupata mafunzo mengio kupitia nyimbo zao ambazo nyingi zimekuwa zikitoa mafunzo kwa watanzania.


Hivyo alisema kuwa kwa kuwapatia vifaa hivyo, Msondo itakuwa moto wa kuotea mbali katika kutoa burudani ya uhakika hali itakayofanya bendi nyingine kwa wasindikizaji katika tasnia ya muziki wa dansi nc?hini.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Maalim Gurumo alisema kuwa kwa sasa wanadeni kwa Watanzania na kampuni ya Konyagi katika kutoa burudani ya uhakika baada ya kupatiwa vifaa hivyo.

"Tunaamini baada ya leo kupata vifaa hivyo tutatoa burudani ya uhakika sanjari na kukijenga vyema kikosi chetu kwa lengo la kukiimarisha," alisema Gurumo.

Kiongozi wa bendi hiyo Said Mabela alitoa shukrani wa kampuni ya konyagi kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kutoa burudani safi kwa Watanzania na Afrika kwa ujumla.

"Tunashukuru kampuni ya Konyagi kutupatia vifaa vya muziki ambavyo kwetu ilikuwa ni vigumu kwa kipindi hiki kuvipata, hivyo tunaamini tutafanya tutaendela kuwa vinara katika kutoa burudani nchini," alisema Mabela.

Ofisa Habari wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa amefurahishwa na kampuni hiyo kutoa vifaa hivyo akiamini kuwa vijana wake watafanya vizuri zaidi katika ushindanio wa muziki huo nchini.

Pia aliwaomba wadau wengine wa muziki nchini kujitokeza  kuisaidia Msondo ili kuijengea uimara katika ushindi wa muziki huo nchini ili kuendelea kuwa bendi bora na ya kuigwa nchini. 

WANAMZIKI WA BENDI YA MSONDO NGOMA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KONYA

WALTER NDIYE MKALI WA EBSS 2012 AZOA MILIONI 50

Walter Chilambo ameibuka mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Sesrch 2012 usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam baada ya kuwabwaga washiriki wenzake wanne alioingia fanali, hivyo kuzawadiwa papo hapo kitita cha Sh. Milioni 50.
Salma Yussuf Abushir amekuwa wa pili na Wababa Mtuka amekuwa wa tatu, wakati ndugu wawili, Nsami Nkwabi na Nshoma Nghangasamala hawakuingia tatu  bora.
Walter akikabidhiwa begi lake la Milioni 50

Walter akiwapungia mashabiki baada ya kushinda

Walter akifanya vitu vilivyompa ushindi

Walter akikusanya fedha alizotuzwa na mashabiki

Walter ze Milione

Richa Mavocal akitumbuiza

Mashabiki wakicheza

Richa Mavocal akitumbuiza

Majaji wakibangua bongo zao. Kutoka kulia Master Jay, Ritha Poulsen na salama Jabir

Mzee Yussuf mwenye suti akitumbuiza

Mzee Yussuf

Ben Pol akitumbuiza

Majaji wakielekezwa kuhusu kura za mashabiki na Ofisa wa Push Mobile

Linah na Amani wakitumbuiza

Lina na Amani

Furaha ya ushindi. walter akiwa amekaa chini ya miguu ya bosi wa Zantel, wadhamini wa shindano hilo

Linah na Amani jana ilikuwa mhhh!

Mshindi wa BSS mwaka jana, akitumbuiza

Keysha alikuwepo

Mashabiki

Emillian Rwejuna alikuwepo

Ephraim Mafuru wa SBL kulia akiwa na mkewe
Wababa akifanya vitu vilivyompa nafasi ya tatu

Salma akifanya vitu vilivyompa nafasi y

Ras Six akitumbuiza

Wazee wa kukesha

Dito akitumbuiza na Walter

Jaji Mkuu, Ritha akitangaza matokeo. Kulia ni bosi wa Zantel

Linex akitumbuiza na Salma

Mihela

Nsima

Walter na Salma kabla ya matokeo kutangazwa

Ommy Dimpoz akitumbuiza

Dimpoz akipagawisha

Achana na Dimpoz

Rich MavocalCHANZO:Bongostaz