STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 9, 2013

Nizar aipaisha Yanga, Azam yabanwa na Polisi

 
Mfungaji wa bao la Yanga leo dhidi ya Toto African
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuinyuka Toto African ya Mwanza bao 1-0 katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo.
Yanga ikiicheza kwenye uwanja wa Taifa ilishindwa kuonyesha makeke yake licha ya kupata bao katika kipindi cha kwanza lililofungwa na Hamis Kiiza na kukataliwa na mwamuzi akidai mfungaji alimchezea rafu kipa wa Toto kabla ya kutumbukiza mpira wavuni kwa kichwa na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe 0-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kosa kosa za hapa na pale baina ya timu zote huku Hamis Kiiza, Simon Msuva na Jerryson Tegete wakiongoza kwa kukosa mabao.
Hata hivyo mabadiliko ya kocha wa Yanga ya kumtoa Tegete na kumuingiza Nizar Khalfan yaliisaidia Yanga kupata bao lililofungwa na Nizar katika dakika ya 78 na kuipa ushindi huo muhimu ambao ulionekana kutowekwa katika pambano la leo.
Toto ilimpoteza mchezaji wake, Eric Mlilo, huku Kiiza akifunga bao katika kipindi hicho cha pili lililokataliwa tena na mwamuzi kwa madai alikuwa ameotea kabla ya kutumbuiza wavuni.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha jumla ya pointi 45 kutokana na mechi 19 ilizocheza na kuiacha Azam waliopo nafasi ya pili kwa pointi nane baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Polisi Morogoro.
Sare hiyo imeifanya Azam kufikisha pointi 37 kwa michezo 19 iliyocheza huku kukisaliwa mechi saba kabla ligi hiyo msimu huu haijamalizika.
Kwenye uwanja wa Chamazi, Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya tano kupitia kwa John Bocco 'Adebayor' bao lililodumu hadi mapumziko.
Bao la kusawazisha na Polisi lilifungwa kwenye kipindi cha pili katika dakika ya 54 na Mokili Rambo na kuifanya timu hiyo iambulie pointi moja na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi katika duru la pili.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa pambano moja tu litkalokutanisha 'ndugu' wawili, Simba ya jijini Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga pambano litakalochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Msimamo kamili wa Ligi Kuu baada ya mechi ya leo:
                             P  W  D  L  GF GA  GD Pts
1 Yanga               19 14  3   2   36  12   24  45
2 Azam                19 11  4   4   32  16  16   37
3 Simba SC          18  8   7   3   26  15  11   31
4 Coastal U          19  8   7   4   21  16   5    31
5 Mtibwa             20  8    7   5   22  18   4   31
6
Kagera Sugar    20  8    7   5   21  17   4   31
7 Ruvu Shooting  18  8    5   5   21  17   4   29
8 JKT Oljoro       19   6   6   7   20  22  -2   24
9 Mgambo JKT    20  7   3   10  14  19  -5  24
10 TZ Prisons      20   4   8   8   11  17  -6   20
11 JKT Ruvu       19   5   4  10  16  30 -14  19
12 Polisi Moro    19   3   7   9    10  19  -9  16
13 Toto African  20   2   8   10  15  28  -13 14
14 African Lyon  20  3   4  13 13  32  -19  13



Coastal 'kuchochea' moto Msimbazi kesho au...!

Kikosi cha Coastal Union

Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi kuu Simba
MABINGWA wa zamani wa kandanda nchini, Coastal Union ya Tanga kesho inatarajiwa kushuka dimba la Taifa kupambana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ambayo ipo katika taharuki kubwa kufuatia baadhi ya vibopa wake kuachia ngazi ghafla kabla ya kutangazwa kamati maalum ya ushindi.
Simba na Coastal zitapambana katika pambano pekee la ligi kwa kesho, huku timu zote ziliwa zimelingana kwa pointi kila moja ikiwa na pointi 31 sawa na timu 'ndugu' za Mtibwa Sugar na Kagera Sugar na kulifanya pambano hilo la kesho kushindwa kutabirika mapema.
Mwenendo mbovu iliyonayo Simba ambayo katika mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ilinyukwa bao 1-0, itashuka keshi dimbani ikiwa na matumaini makubwa ya kurekebisha makosa baada ya kuunda kamai ya ushindi inayoongozwa na Malkia wa Nyuki, Rahma Al Kharoos.
Hata hivyo kuundwa kwa kamati hiyo iliyotangazwa na Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are 'Mzee Kines' huenda isiwe dawa ya kutetereka kwa timu hiyo, iwapo wataingia uwanjani wakiamini ushindi bila kuifikiria Coastal yenyewe ikiwa ina shinikizo la mashabiki wake baada ya 'kuyumba' katia duru la pili.
Timu hiyo ililazimishwa suluhu na Ruvu Shooting katika mechi yao ya mwisho na kusababisha mashabiki hao kulalamika, japo blog ya klabu hiyo imemnukuu Mwenyekiti wao, Ahmed Hilal 'Aurora' akitamba kuwa kesho ni kesho katika mechi yao ya Simba.
Coastal katika duru la pili imeambulia pointi tisa tu kati ya 18 zilizotokana na mechi sita walizocheza wakipoteza moja kwa Kagera Sugar, kushinda mbili dhidi ya maafande wa Mgambo na JKT Oljoro, huku wakiambulia sare tatu mbele ya Prisons-Mbeya, Toto Afrika na Ruvu Shooting katika mechi yao iliyopita.
Hata hivyo Aurora alidai wangependa kushinda mechi hiyo licha ya kutambua ugumu wake mbele ya Simba huku akiahidi kufanya vema kwa mechi zao zitakazosalia kabla ya kufunga msimu ili kuzipiku timu wanazofukuzana nao kwenye kuwania nafasi ya tatu na nne katika ligi hiyo zikiwemo Mtibwa na Kagera.
na nyingine zilizosalia kabla ya ligi kwisha ili kuweza kuziacha mbali Mtibwa na Kagera Sugar wanaoifukuzia nafasi ya nne.
Alisema mechi hiyo ya kesho ndiyo itakayoamua timu ipi ishike nafasi ya tatu kati yao na Simba waliowazidi uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika pambano lao duru la kwanza lililochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga Oktoba 13, mwaka jana timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu ya 0-0.
Je, ni Coastal itakayotuliza munkari wa mashabiki na kuchochea kuni Msimbazi, au itatoa faraja kwa Simba? Tusubiri tuone hiyo kesho.

Changamoto, NSSF zaanza kwa kishindo NSSF CUP

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akipa mpira wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NSSF leo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akikagua timu ya Changamoto kabla ya pambano lao na timu ya Habari Zanzibar. Changamoto iliwavua ubingwa wa michuano hiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Habari Zanzibar kwa kuitandika 3-0.
 Waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wakisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kabla ya mchezo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na wachezaji wa Habari Zanzibar.
 Golikipa wa Habari Zanzibar akipatiwa matibabu baada ya kuumia.
 Kocha wa timu ya Changamoto, Mawazo Lusonza akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (katikati) akifuatilia mchezo wa netiboli kati ya NSSF na Mlimani Tv, katika mchezo huo NSSF ilishinda 46-1 Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.
 Meneja Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu akitoa maelekezo kwa Ofisa Uhusiano Kinongozi wa NSSF, Eunice Chiume wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo.
 Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa wa ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup dhidi ya NSSF uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Changamoto imeshinda 3-0
 Mshambuliaji wa timya Habari Zanzibar, Amour Mohamed akimtoka beki wa Changamoto, John Robert 
 Kiungo wa timu ya Changamoto, Andrew Faustin akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa Habari Zanzibar, Thani Mfamau.
 Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.
 Timu za Nertiboli za NSSF na Mlimani Tv zikichuana ambapo NSSF imeshinda 46-1
 
 
IMEHAMISHWA HABARI MSETO: