STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 31, 2014

Shi....Shilole achia ngoma mpya iitwayo Chuna Buzi

Shilole
BAADA ya kutamba na kibao chake cha 'Nakomaa na Jiji', msanii Zuwena Mohammed 'Shilole' ameachia kazi mpya iitwayo 'Chuna Buzi' na kuwataka mashabiki wake kumuunga mkono kama walivyofanya katika kazi zake za nyuma kuanzia 'Lawama', 'Dume Dada' hadi 'Paka la Baa'.
Wimbo ni utunzi wa Barnaba Boy ambaye ameutendea haki kwa kum back-up mkali huyo anayekimbiza katika filamu pia.

AZAM kukipiga na Ferreviario de Beira Chamazi


* CAF yaruhusu uwanja wake wa Chamazi

chamazi_2
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindanoya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanzaunaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki  kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana Khaled Nassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote vinavyohitajika na CAF kuchezewa mashindano ya kimataifa hivyo kuanzia tarehe ya leo, uwanja huu unaruhusiwa “kuchezewa mechi za CAF
Bwana Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguziwake toka nchini Zimbabwe Bwana Wilfried Mukuna kuja kukagua uwanja huu. Bwana Mukuna aliwasilisha ripoti CAF iliyopelekea shirikisho hilo kutoa kibali kwa Azam FC na TFF kuruhusiwa kuutumia uwanja huu kwa mechi zinazoandaliwa na CAF
Uongozi wa Azam FC umetoa shukrani kwa mkaguzi wa CAF Bwana Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya Rais Jamal Malinzi, na uongozi wa CAF Cairo Misri hasa Bwana Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa uwazi na uweledi wa hali ya juu uliopelekea uwanja wetu kupata kibali cha kutumika kwenye michezo ya kimataifa.
Azam FC sasa imewatangazi
wapenzi wake kuwa kuanzia msimu huu mechi zake za  CAF zitachezwa Azam Complex Chamazi

Yanga yakanusha Cannavaro, Niyonzima kuzichapa Mkwakwani

Niyonzima (kulia) na Cannavaro (kati) wakiwa na Chuji (24)

BENCHI la Ufundi la klabu ya Young Africans limekanusha taarifa kwamba nyota wawili wa timu yao, nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' na Haruna Niyonzima 'Fabregas' walipigana katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliochezwa juzi jijini Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa klabu hiyo wa www.youngafricans.co.tz , umemnukuu Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa 'Master' akisemataarifa hizo hazina ukweli wowote bali ni katika kutaka kuharibu twasira ya timu.
Mkwasa amesema benchi la ufundi wameshangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona na kuzisoma leo na kusisitiza walioandika wamefanya hivyo kwa ajili ya maslahi yao tu.
Kila mtu alikuwepo uwanjani na aliweza kushuhudia mchezo huo, hakuna aliyeona Cannavaro na Niyonzima wakipigana katika kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, nashikwa wasi wasi na waandishi waliokuwepo uwanjani kama walikua makini kufuatilia mchezo na kuandika kitu tofauti na walichokiona.
"Sheria za soka zipo wazi, mchezaji au wachezaji wapigana ndani ya uwanja mwamuzi anawatoa nje ya uwanja kwa kuwapa kadi nyekundu, sasa tumeshangazwa na taarifa hizo zilioripotiwa leo kuwa kuwa kuna wachezaji wetu walipigana ili wachezaji wote walicheza kwa dakika 90 "alisema Mkwasa.
Nadhani imefika wakati tuisaidie jamii kuelewa uhalisia wa jambo husika liliotokea, kwani kuandika tofauti na kilichotokea kunasababisha jamii kuamini/kuelewa jambo ambalo silo lililotokea.
Katika mchezo wowote wachezaji kuelekezana/kukumbushana majukumu ni jambo la kawaida na ndicho kilichotokea katika mchezo dhidi ya Coastal kati ya Cananavaro na Yondani na Niyonzima na Cannavaro na si kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Hata mara baada ya mchezo wachezaji wote walikuwa pamoja na kupeana pole kutokana na ugumu wa mechi, kisha wote kuondoka kuelekea hotelini kupumzika, na sisi kama viongozi hatujaona wachezaji kutofautiana kitu chochote hata kufikia hatua ya kusuruhishwa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari " aliongeza Mkwasa .
Kuhusu maandalizi ya mchezo wa jumapili Mkwasa amesema vijana wake leo wamefanya mazoezi asubuhi kujiandaa na mchezo huo, na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kwani Hamis Kiiza, Hassana Dilunga waliokuwa wagonjwa wameshaungana wenzao kambini na Athuman Idd "Chuji"  aliyekua amesimamishwa kurejeshwa kundini.

Bodi ya Ligi Kuu yazipiga jeki klabu za FDL

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa sh. milioni 1.5 kwa kila klabu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Uamuzi wa kuzisaidia timu hizo ulifanywa katika kikao cha TPLB kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo fedha hizo zitalipwa kupitia kwenye akaunti za klabu husika. 

Hivyo klabu ambazo hazijawasilisha akaunti zao TPLB zinatakiwa kuwasilisha haraka.
Klabu za FDL ni African Lyon, Burkina Moro, Friends Rangers, Green Warriors, Kanembwa JKT, Kimondo, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mkamba Rangers, Mlale JKT na Mwadui.
Nyingine ni Ndanda, Pamba, Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Morogoro, Polisi Tabora, Stand United, Tessema, Toto Africans, Trans Camp na Villa Squad.

TFF mpya yatimiza siku 100 madarakani, Rais Malinzi kuteta Ijumaa

Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Na Boniface Wambura
KAMATI mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi, Februari 4 mwaka huu inatimiza siku 100 tangu iingie madarakani katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28 mwaka jana.
Hivyo, Rais Malinzi atazungumza na waandishi wa habari Februari 7 mwaka huu kuelezea utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi. Muda na mahali utakapofanyika mkutano huo mtaarifiwa baadaye.


Serengeti Boys kuanza na Afrika Kusini mchujo wa Afrika

Na Boniface Wambura
TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) itacheza na Afrika Kusini katika mechi za mchujo kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Niger.
Serengeti Boys ambayo pamoja na nchi nyingine 17 zimeingia moja kwa moja katika raundi ya pili itaanzia mechi hiyo nyumbani kati ya Julai 18-20 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika nchini Afrika Kusini kati ya Agosti 1-3 mwaka huu.
Ikifanikiwa kuitoa Afrika Kusini, Serengeti Boys itacheza mechi ya raundi ya tatu na ya mwisho na mshindi wa mechi kati ya Misri/Sudan vs Congo Brazzaville.
Nchi nyingine ambazo zimeingia moja kwa moja raundi ya pili ni Afrika Kusini, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Mali, Morocco, Nigeria, Rwanda, Senegal, Tunisia na Zambia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kutangaza benchi la ufundi litakaloiongoza Serengeti Boys hivi karibuni.

Simba, Oljoro kesho hapatoshi, Ashanti Utd kutoka vipi Chamazi

Simba
Oljoro JKT
Na Boniface Wambura
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuwania ubingwa wa Tanzania inaingia raundi ya 16 wikiendi hii kwa mechi nne ambapo kesho (Februari 1 mwaka huu) Simba itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Refa atakuwa Nathan Lazaro kutoka mkoani Kilimanjaro wakati Kamishna ni Hakim Byemba wa Dodoma.

Uwanja wa Azam uliopo Mbagala siku hiyo kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Ashanti United na Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga kwa viingilio vya sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Jumapili (Februari 2 mwaka huu) ni Yanga vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, saa 10 kamili jioni), na Azam vs Kagera Sugar (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 10 kamili jioni).
Ligi hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi).