STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 3, 2013

Tottenham yashindwa kufurukuta kwa Everton

Everton v Tottenham Hotspur
TOTTENHAM Hotspur jioni hii imeshindwa kukwea kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa suluhu na wenyeji wao Everton.
Spurs walikuwa na nafasi ya kushika nafasi ya pili kama ingeifunga Everton kwani ingefikisha pointi 22 ambazo zinepita pointi 20 ilizonazo timu za Liverpool na Chelsea ambazo jana zilichezea vichapo katika mechi zao za Ligi hiyo.
Kwa suluhu hiyo timu hizo zimegawana pointi ambapo Spurs imepanda hadi nafasi ya nne nyuma ya Chelsea na Liverpool zote zikiw na pointi 20, lakini zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Ratiba ya ligi hiyo inaendelea hivi kwa pambano jingine jioni hii kati ya Cardiff City dhidi ya Swansea City.

Inatisha! Hivi ndivyo alivyojeruhiwa Dk Mvungi

Mtoto wa Dk. Sengodo Mvungi, Deogratius Mwarabu (kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku (katikati), na Prof. Paragamba Kabudi walipofika MOI kumjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye amefikishwa MOI baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga.  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengodo Mvungi akitolewa katika chumba cha huduma za dharura MOI na kupelekwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa.

Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa. 

Dk. Sengodo Mvungi akipata matibabu ndani ya gari la kubeba wagonjwa wakati akipelekwa hospitali ya Aga Khan.Dk. Sengodo Mvungi akiwa na majeraha kichwani na sehemu za paji la uso.
Na Hapiness Katabazi

MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk. Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi, Dk. Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku alimdhibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye aliwahi kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa alivamiwa na kujeruhiwa na mapanga na watu wasiyojulikana.

Dk. Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alisema kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwa ajili ya kuanza kupewa matibabu.

HABARI MSETO

Yanga ni balaa Ligi Kuu, Mgambo mmh!

Amissi Tambwe (kulia) Kinara wa mabao Ligi Kuu akiwa na bao 9

Hamis Kiiza 'Diego' anayefuata kwa magoli mengi
PAMOJA na kuporomoshwa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka nafasi ya tatu, mabingwa watetezi Yanga ndiyo timu yenye safu 'wembe' ya ushambuliaji katika ligi hiyo ikiwa imefunga mabao 28.
Mabao 10 kati hayo mabingwa hao walipata katika mechi zao tatu mfululizo zilizochezwa hivi karibuni dhidi ya timu za maafande.
Yanga ikiwa na magoli 28 ya kufunga yenyewe imeruhusu mabao 11 na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa 17 ikizizidi timu nyingine 13 zinazoshiriki ligi hiyo inayomaliza duru la kwanza wiki ijayo.
Simba walio kwenye nafasi ya nne katika msimamo huo ndiyo inayowafuata Yanga kwa kufumania nyavu mara nyingi ikiwa na mabao22 na kufuatiwa na Azam kisha Mtibwa Sugar zenye mabao 20 na 17.
Mabingwa wa zamani wa soka Tanzania, Coastal Union ndiyo timu yenye safu ngumu katika ligi hiyo ikiwa imeruhusu mabao sita mpaka sasa ikifuatiwa na timu za Azam na Mbeya City zenye kufungwa mabao 7 kila moja.
Timu yenye ukuta mwepesi katika ligi hiyo ni Mgambo JKT iliyofungwa mabao 21 na kufuatiwa na Ashanti United iliyoruhusu mabao 20.
Safu butu ya ushambuliaji katika ligi hiyo ni Mgambo yenye mabao matatu tu ikifuatiwa na Prisons Mbeya ambayo jioni hii inashuka dimbani kuwakaribisha Oljoro JKT katika mechi ya mwisho ya raundi ya 12.
Mpaka sasa ligi ikiwa imebakiza mzungumko mmoja kabla ya kumaliza duru la kwanza jumla ya mabao 182 yamefungwa na timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Azam yenye pointi 26 sawa na Mbeya City zinazotofautishwa na uwiano wa mabao iliyonayo.
Mshambuliaji Amissi Tambwe wa Simba akiendelea kuongoza akiwa na mabao 9 akifuatiwa na Hamis Kiiza 'Diego' wa Yanga mwenye magoli 8.
Yanga iliyokuwa kileleni imerejea nafasi ya tatu ikiwa na pointi 25 kisha Simba wakifuatia na pointi zao 21,  wakifuatiwa na Mtibwa Sugar ambayo ushindi wa jana dhidi ya Rhino Rangers umewafanya wafikishe pointi 19.
Kagera Sugar yenye ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 17 na Ruvu Shooting iliyofungwa na Azam jana imeporomoka toka nafasi ya sita hadi ya nane ikiwa na pointi 16 sawa na Coastal ambayo sare yake ya jana dhidi ya Mgambo imechupa hadi nafasi ya saba.
Mgambo imeendelea kuburuza mkia ikiwa na pointi sita ikifuatiwa na Oljoro yenye pointi 7 na Prisons yenye pointi 8, japo yoyote kati ya timu hizo inaweza kuchupa toka nafasi ilizopo kama moja wapo itashinda kwqenye uwanja wa Sokoine-Mbeya watakapoumana jioni hii.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014
    
                                  P    W   D   L    F    A   GD   PTS
01.Azam                    12   7    5    0   20    7    13    26
02.Mbeya City           12   7    5    0   16    7     9     26
03.Yanga                    12   7    4    1   28   11   17    25
04.Simba                    12   5    6    1   22   11   11    21
05.Mtibwa Sugar        12   5    4    3   17   15    2     19
06.Kagera Sugar         12   4    5    3   12    9     3    17
07.Coastal Union        12    3    7    2   10    6     4    16
08.Ruvu Shooting        12   4    4    4   13   13     0    16
09.JKT Ruvu              12    4    0    8    9    16   -7    12
10.Rhino Rangers        12    2    4    6    9   16    -5   10
11.Ashanti                   12    2    4    6   10  20   -10  10
12.Prisons                   11    1    5    5     5   14   -9    8
13.Oljoro                    11    1    4    6     8    16  -8    7
14.Mgambo                12    1    3    8     3    21 -18   6

Wafungaji:
9- Tambwe Amisi (Simba)
8- Hamis Kiiza (Yanga)
7- Elias Maguri (Ruvu Shooting), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Kipre Tchetche (Azam)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Themi Felix (Kagera), Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa (Yanga)
4-Peter Michael (Prisons), Jerry Santo (Coastal Union), Jerry Tegete (Yanga)
3- Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union),  Mcha Khamis (Azam)
2-
Haruna Moshi, Crispian Odulla (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John, Peter Mapunda,(Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary (JKT Oljoro), Joseph Kimwaga (Azam), Shaaban Nditti (Mtibwa Sugar), Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
1- Abdi Banda, Danny Lyanga (Coastal Union), Henry Joseph, Joseph Owino, Gilbert Kazze (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Frank Dumayo, Mbuyi Twitte, Oscar Joshua (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah, Abbas Mohammed (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah,  Aggrey Morris,  John Bocco, Faridi Maliki, Hamphrey Mieno, Salum Abubakar, Erasto Nyoni (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Deo Deus  (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader  (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Shaaban Kisiga, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG), Samir Luhava (OG), John Matei, Mwinyi Ally (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas, Salum Kanoni (Kagera Sugar), Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)

Ratiba ya kufungia duru la kwanza:
Nov 06, 2013
JKT Ruvu vs Coastal Union
Ashanti Utd vs Simba
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar
Kagera Sugar vs Mgambo JKT

Nov 07, 2013
Azam vs Mbeya City
Rhino Rangers vs Prisons
Yanga vs Oljoro JKT 

Orlando yabanwa nyumbani na Al Ahly Fainali Afrika

Wachezaji wa Al Ahly na Orlando walipokutana katika hatua ya makundi
BAO la mapema la mkongwe wa Misri, Mohammed Aboutrika limeweka kuiweka katika nafasi nzuri klabu ya Al Ahly katika mbio zake za kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini nchini Afrika Kusini dhidi ya wenyeji wao Orlando Pirates.'
Aboutrika alifunga bao hilo katika pambano la kwanza la Fainali za ligi hiyo kwenye dakika ya 14 na kudumu hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Hata hivyo wenyeji walikuja kuchomoa bao hilo kwenye dakika za nyongeza za pambano hilo (90+3) kupitia kwa Thabo Matlaba na kuwaokoa Orlando na kipigo nyumbani, ingawa sare hiyo inawapa wakati mgumu kuwawavua taji Al Ahly.
Timu hizo zitarudiana mwishoni mwa wiki ambapo Al Ahly itakuwa katikka nafasi nzuri ya kutetea taji hilo iwapo itapata hata suluhu tu, ingawa soka huwa halitabiriki.

Hawa ndiyo wanamichezo wenye wafuasi wengi katika Twitter

WAPO wanamichezo na mastaa kibao waliojiunga kwenye mitandao ya kijamii ambao huwa na Followers, wakishindana wenyewe kwa wenyewe.
Hapa chini ni orodha ya wanamichezo watano (Top 5) wenye followers wengi kwenye mtandao wa Twitter.

No.5- Shaquille O'neal-Milioni 8
Shaquille O'Neal
No. 4- Neymar- Milioni 9
Neymar
No.3- Lebron James-Milioni 10
Lebron James
No.2- Ricardo Kaka- Milioni 17
 
Ricardo Kaka
 No.1-Cristiano Ronaldo-Milioni 22
Cristiano Ronaldo

Binti wa Carren Mgonja apata Kipaimara cheki party yake


 

Carrenflora Mgonja wa kundi la wajasiliamali wa kikundi cha Habari Group akiwa na mumewe Patson Mlandali wakati wa kumfanyia part ya kipaimara bint yao Elizabet iliyofanyika katika ukumbi wa Abiola Buza Dar es salaam jana
Washereheshaji wa shughuli hiyo Anti Latifa kushoto na Sakina Lioka wakiwa na CArren Mgonja wakati wa sherehe ya mwanae
Elizabet
kutoka kushoto Hellen Mwango na Somoe N,gitu wafanyakazi wenzie
WAZAZI WAKICHEZA MZIKII
WAZAZI WAKITOA NENO LA KUWAKARIBISHA WAGENI

Carrenflora Mgonja

Angetile nje TFF, Wambura akaimu nafasi yake


Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura

SAFU mpya ya uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyokutana jana kwa mara ya kwanza tangu waingie madarakani Oktoba 27, wamemtupa nje aliyekuwa Katibu Mkuu, Angetile Osiah na nafasi yake kukaimiwa na Afisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani za kikao hicho kilichoendeshwa na Rais Jamal Malinzi ni kwamba Angetile amepewa likizo ya muda usiojulikana na wakati anasubiri hatima yake, Wambura ataendelea kusimamia kazi zake zote.
Hata hivyo TFF inatarajiwa kutoa taarifa rasmi juu ya suala hilo kutokana na ukweli kwa sasa safu hiyo 'inasafisha' shirikisho hilo ili kuanza upya chini ya uongozi wa Malinzi kwani tayari kamati zote zilizokuwepo enzi za rais aliyepita, Leodger Tenga zimevunjwa pia.

Hawa ndiyo Top 10 ya waigizaji visura- 2013

1. Elizabeth Michael Lulu(18)

Lulu is sexy and she knows it, she is confident with her natural beauty that is why we have seen this diva many times with no wigs or weaving, may be because she grew up onscreen. She is talented and very popular in the Tanzanian Swahili movie industry.
Elizabeth Michael
2.Omotola Jalade(35). 
The mother of four children is already known as Omosexy, she is very popular in Nollywood. She is an ageless beauty.
http://informationng.com/wp-content/uploads/2013/04/omotola1.jpg

3.Jackie Appiah(29) 
Born in Canada but got huge popularity in the Ghananian movie industry, Jackie is sexy and talented.
She has appeared in many movies both in Ghana and Nigeria.
http://www.newstimeafrica.com/wp-content/uploads/2013/03/Jackie-Appiah-Best-Actress-Award.jpg
Jackie Appiah

4.Jackline Wolper(25)
Tanzanian Swahiliwood screen goddess, Wolper once said she makes sure she eats green vegetables, fruits and drinks lots of water every day to maintain her beauty. Wolper is a top actress in the Tanzanian movie industry and she has appeared in many movies this year.
http://3.bp.blogspot.com/-Ux4H_aAgxR0/UcmxrsknF2I/AAAAAAAAAcc/OfmuodRsgC4/s400/jack.jpg
Jacklyen Wolper

5.Genevieve Nnaji(34)
“Referred to as Julia Roberts of Africa” this Nollywood queen has maintained her beauty over years. She is simply beautiful and sexy.
Genevieve Nnaji
6.Nadia Buari(30)
Another Ghananian actress,Nadia is simply hot
http://www.etesenghana.com/wp-content/uploads/2013/01/Nadia-Buari.jpg
Nadia Buari
 7.Yobnesh Yusuph “Batuli”(27)
Mother of two but she still looks hot leaving behind many of her contemporaries in the Tanzanian Swahili movie industry.
http://1.bp.blogspot.com/-W4x4az_lGso/Ug9azXcKiSI/AAAAAAAAkzk/BiCmbmBSF0k/s1600/batuli.jpg
Batuli
8.Julieth Ibrahim(27)
Julieth is another Ghananian famous actress, early this year the bombshell actress said “The fact is and will always remain I, Juliet Ibrahim is 100 times hotter, prettier than Kim kardashian! I have every right to say so Coz I am an African woman without any surgeries and natural beauty is what I brag of”
Juliet
9.Ini Edo(31)
Edo is one of the hottest female stars in Nollywood whom their beauty can’t be hidden.
http://sweetmilliesinfo.webs.com/photos/Ma-fav-nigerian-picts/ini.jpg
Ini Edo
10.Yvonne Cherryl”Monalisa”(32)
Despite being a mother of two Yvonne Cheryl popularly know as Monalisa has kept herself in shape over years. She is a true black beauty in Tanzanian Swahili movies.
Monalisa
source;djsekblog

Azam, Mbeya City yaziporomosha Yanga, Mtibwa yazinduka

Azam wakishangilia moja ya mabao yao ya jana

Mbeya City
BAO la kujifunga la beki wa Ashanti United, Samir Luhava, lilitosha kuifanya Mbeya City kuendeleza rekodi ya kushinda mechi mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara inayoicheza kwa mara ya kwanza na kurejea kwenye nafasi ya pili nyuma ya Azam waliorejea kileleni baada na wao kupata ushindi wa mabao 3-0.
Mbeya City, iliyokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Sokoine inadaiwa haikuonyesha soka lake lilizoeleka kutokana na kubanwa na Watoto wa Jiji, Ashanti ambao walioinyesha walienda Mbeya kufuata ushindi.
Hata hivyo dakika ya 30 ya pambano hilo, Samir katika harakati za kuokoa mpira langoni kwake alijikuta akijifunga bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Ashanti kurejea Dar kinyonge kusubiri kuumana na Simba siku ya JUmatano.
Nao Azam waliendelea kuonyesha dhamira yao ya kuwa mabingwa wapya nchini baada ya kuinyoa Ruvu Shooting mabao 3-0 na kuiporomosha Yanga hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu kwa kurejea kileleni ikifikisha pointi 26.
Mabao ya Azam iliyokuwa uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi yalifungwa na Kipre Tchetche, Joseph Kimwaga na Mcha Khamis 'Vialli'.
Mtibwa Sugar baada ya kukumbana na kipigo cha mbwa mwizi uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mechi iliyopita jana ilizinduka na kuinyoa Rhino Rangers kwa bao la Salim Mbonde huku, Coastal Union na Mgambo JKT zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu.
Ligi hiyo itaendelea tena kwa pambano moja tu la kukamilisha mechi za raundi ya 12 kwa timu ya Prisons Mbeya kuialika Oljoro JKT kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Dk Mvungi avamiwa, acharangwa mapanga

Dk Sengondo Mvungi
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Dk. Sengondo Mvungi, usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana na kukatwa mapanga maeneo mbalimbali mwilini ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai ya kutaka wapatie fedha. 
Watu hao walitimiza lengo lao hilo baada ya Dk. Mvungi kuwaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.
Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi aitwaye Dk. Natujwa Mvungi ameeleza kuwa baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani ambapo amepatiwa huduma ya kwanza kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baadaye alipelekwa kwenye wodi katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi

Arsenal yaizima Liverpool, Man City yaua EPL

Raha ya ushindi bana ni mabao

Ramsey akitumbukiza wavuni bao la pili la Arsenal

ASRENE Wenger kocha wa Arsenal ameendelea kudhihirisha huu ni msimu wake baada ya 'babu' mwenzake, Sir Alex Ferguson kustaafu kufundisha soka baada ya vijana wake kuwafumua wenzao wa Liverpool na kuimarisha uongozi wao wa Ligi Kuu ya England.
Mabao mawili ya kila kipindi yaliyotosha kuwapa ushindi muhimu Arsenal kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Emirates.
Bao la kwanza liliwekwa kimiani na Santi Carzola katika dakika ya 19 kabla ya Aaron Ramsey kuongeza la pili kwenye kipindi cha pili na kuifanya Arsenal kuimarisha uongozi wake kwa kufikisha pointi 25, pointi tano zaidi ya wapinzani wao na Chelsea ambayo mapema jana ilinyukwa mabao 2-0 na Newcastle United.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Manchester City ikiwa nyumbani iliifumua Norwich City kwa mabao 7-0, huku Manchester United wakipata ushindi muhimu ugenini dhidi ya Fulham walipowatungua mabao 3-1, huku West Ham United na Aston Villa silishindw akutambiana kwa kutoka suluhu.
Sunderland iliendelea kuwa mtepeto baada ya kunyukwa bao 1-0 na Hull City, West Bromwich iliipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Crystal Palace na Stoke City na Southampton walishindwa kupata mbabe baina yao kwa kutoka sare ya baoa 1-1.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa michezo miwili, Everton watakuwa nyumbani kuikaribisha Tottenham ambapo mshindi wowote wa pambano hilo atakwea hadi nafasi ya pili baada ya Chelsea na Liverpool jana kuangukia pua katika mechi zao. Pambano jingine la leo litakuwa kati ya Cardiff City dhidi ya Swansea City.

MATOKEO MITIHANI DARASA LA SABA YATOKA...SOMA HAPA

Dar es salaam, Tanzania
MATOKEO ya Darasa la Saba yametangazwa  na mwaka huu huku ufaulu ukiwa umeongezeka kutoka asilimia 30.72 mwaka jana mpaka asilimia 50.61 mwaka huu kutokana na wanafunzi walio fanya mtihani mwaka huu wa darasa la saba wamefaulu zaidi ukilinganisha na wanafunzi wa mwaka jana Kaimu mtendaji wa Baraza la Mtihani Charles Msonda amesema ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 6.01 na 28.06 ukilinganisha na mwaka 2012.
Mwaka huu watahiniwa wamefahulu zaidi katika somo la Kiswahili kwa asilimia 69.06 na somo walilio faulu kwa kiwango kidogo zaidi ni somo la Hisabati wamefaulu kwa asilimia 28.62.
 Msonda amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya 844,938 walio fanya mtihani huo wamepata alama ya 100 kati ya alama ya 250 idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61