STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 3, 2013

Arsenal yaizima Liverpool, Man City yaua EPL

Raha ya ushindi bana ni mabao

Ramsey akitumbukiza wavuni bao la pili la Arsenal

ASRENE Wenger kocha wa Arsenal ameendelea kudhihirisha huu ni msimu wake baada ya 'babu' mwenzake, Sir Alex Ferguson kustaafu kufundisha soka baada ya vijana wake kuwafumua wenzao wa Liverpool na kuimarisha uongozi wao wa Ligi Kuu ya England.
Mabao mawili ya kila kipindi yaliyotosha kuwapa ushindi muhimu Arsenal kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Emirates.
Bao la kwanza liliwekwa kimiani na Santi Carzola katika dakika ya 19 kabla ya Aaron Ramsey kuongeza la pili kwenye kipindi cha pili na kuifanya Arsenal kuimarisha uongozi wake kwa kufikisha pointi 25, pointi tano zaidi ya wapinzani wao na Chelsea ambayo mapema jana ilinyukwa mabao 2-0 na Newcastle United.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Manchester City ikiwa nyumbani iliifumua Norwich City kwa mabao 7-0, huku Manchester United wakipata ushindi muhimu ugenini dhidi ya Fulham walipowatungua mabao 3-1, huku West Ham United na Aston Villa silishindw akutambiana kwa kutoka suluhu.
Sunderland iliendelea kuwa mtepeto baada ya kunyukwa bao 1-0 na Hull City, West Bromwich iliipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Crystal Palace na Stoke City na Southampton walishindwa kupata mbabe baina yao kwa kutoka sare ya baoa 1-1.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa michezo miwili, Everton watakuwa nyumbani kuikaribisha Tottenham ambapo mshindi wowote wa pambano hilo atakwea hadi nafasi ya pili baada ya Chelsea na Liverpool jana kuangukia pua katika mechi zao. Pambano jingine la leo litakuwa kati ya Cardiff City dhidi ya Swansea City.

No comments:

Post a Comment