STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 3, 2013

Orlando yabanwa nyumbani na Al Ahly Fainali Afrika

Wachezaji wa Al Ahly na Orlando walipokutana katika hatua ya makundi
BAO la mapema la mkongwe wa Misri, Mohammed Aboutrika limeweka kuiweka katika nafasi nzuri klabu ya Al Ahly katika mbio zake za kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini nchini Afrika Kusini dhidi ya wenyeji wao Orlando Pirates.'
Aboutrika alifunga bao hilo katika pambano la kwanza la Fainali za ligi hiyo kwenye dakika ya 14 na kudumu hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Hata hivyo wenyeji walikuja kuchomoa bao hilo kwenye dakika za nyongeza za pambano hilo (90+3) kupitia kwa Thabo Matlaba na kuwaokoa Orlando na kipigo nyumbani, ingawa sare hiyo inawapa wakati mgumu kuwawavua taji Al Ahly.
Timu hizo zitarudiana mwishoni mwa wiki ambapo Al Ahly itakuwa katikka nafasi nzuri ya kutetea taji hilo iwapo itapata hata suluhu tu, ingawa soka huwa halitabiriki.

No comments:

Post a Comment