STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 3, 2013

Angetile nje TFF, Wambura akaimu nafasi yake


Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura

SAFU mpya ya uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyokutana jana kwa mara ya kwanza tangu waingie madarakani Oktoba 27, wamemtupa nje aliyekuwa Katibu Mkuu, Angetile Osiah na nafasi yake kukaimiwa na Afisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani za kikao hicho kilichoendeshwa na Rais Jamal Malinzi ni kwamba Angetile amepewa likizo ya muda usiojulikana na wakati anasubiri hatima yake, Wambura ataendelea kusimamia kazi zake zote.
Hata hivyo TFF inatarajiwa kutoa taarifa rasmi juu ya suala hilo kutokana na ukweli kwa sasa safu hiyo 'inasafisha' shirikisho hilo ili kuanza upya chini ya uongozi wa Malinzi kwani tayari kamati zote zilizokuwepo enzi za rais aliyepita, Leodger Tenga zimevunjwa pia.

No comments:

Post a Comment