STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 3, 2013

Tottenham yashindwa kufurukuta kwa Everton

Everton v Tottenham Hotspur
TOTTENHAM Hotspur jioni hii imeshindwa kukwea kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa suluhu na wenyeji wao Everton.
Spurs walikuwa na nafasi ya kushika nafasi ya pili kama ingeifunga Everton kwani ingefikisha pointi 22 ambazo zinepita pointi 20 ilizonazo timu za Liverpool na Chelsea ambazo jana zilichezea vichapo katika mechi zao za Ligi hiyo.
Kwa suluhu hiyo timu hizo zimegawana pointi ambapo Spurs imepanda hadi nafasi ya nne nyuma ya Chelsea na Liverpool zote zikiw na pointi 20, lakini zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Ratiba ya ligi hiyo inaendelea hivi kwa pambano jingine jioni hii kati ya Cardiff City dhidi ya Swansea City.

No comments:

Post a Comment