STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 4, 2013

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa jana huko Tunduma Mbeya kwevye vurugu zinazotokana na kugombea kuchinja kati ya Waislam na Wakristo sijui wapi tunakwenda Watz!

Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma janaMatairi yanachomwa katikati ya barabaraMambo hayo 
Mwandishi wa Mbeya Yetu na waandishi wenzake walipata shida sana kufika mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate habariKamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Afande  Diwani  Athuman akiongea na waandishi wa habari

Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao


Polisi wakiendelea kazi yao katika mitaa ya Tunduma


Baadhi ya magati ya IT yaendayo nchini Zambia yakiwa yamepakiwa nnje kidogo ya mji wa Tunduma kuogopa kuharibiwa kwa magari hayo


DIWANI wa Kata ya Tunduma Ndugu Frank Mwaijoka (Chadema) na Mchungaji wa Kanisa la KKT katika eneo hilo la Tunduma wilayani mkoani Mbeya wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa vurugu  katika eneo hilo.
Vurugu hizo zimeanza majira ya saa 3:asubuhi katika eneo hilo la Tunduma mara baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.
Akizungumza kuhusiana na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi ya 40 tayari wamekwisha kamatwa .
Amesema mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya Tunduma Ndugu John Mwaijoka pamoja na mchungaji huyo wa kanisa la kkt ndugu Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Amesema suala hilo limegubikwa  na siasa kwani tayari viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi Apri 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini .
Amesema kwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.
Amesema shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika eneo hilo hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka mpakani mwa Tanzania.
Hata hivyo Diwani amesema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja  pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.
Kufuatia hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imerejea katika hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu wakati jeshi hiulo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta wahalifu wengine.

Picha na Mbeya yetu 

Hivi ndivyo uwanja wa Yanga utakavyokuwa
Ramani ya uwanja mpya wa klabu ya Yanga - Kaunda Stadium unavyoekana kwa ndani


Kampuni ya Beinjing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi akinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG  Zhang Chengwei David amesema upembuzi akinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.
Zhang alisema kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 201o.
Aidha Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000.
Katika uwasilishaji huo wa makadirio ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe alisema wanafurahishwa na kampuni ya BCEG kwa kukamilisha zoezi la upembuzi akinfu mapema ambapo leo wamepata fursa ya kujionea na kujua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.


Ramani ya mchoro wa Uwanja mpya wa Kaunda unavyoonekana kwa njeKifukwe alisema wamepewa nafasi ya kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa klabu ya Yanga utakaa na kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha kwa kampuni ya BCEG na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda. 
Akijibu swali la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za ujenzi wa uwanja, Kifukwe alisema ujenzi wa uwanja wa mpya utajengwa na wanachama, wapenzi na washambiki wa klabu ya Yanga.
Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.
Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maaalumu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.

SOURCE:http://www.youngafricans.co.tz

TFF YAZINDUA MPANGO WA MAENDELEO 2013-2016

Viongozi wakuu wa TFF, Rais Leodger Tenga na Katibu Mkuu, Angetile Osiah

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezindua rasmi Mpango wa Maendeleo wa Mpira wa Miguu (Technical Development Plan- TDP) wa 2013-2016 ambao pamoja na mambo mengine unahusisha kutazama upya mfumo wa mashindano na kuunda kanda kwa ajili ya kusimamia maendeleo.

Uzinduzi huo umefanywa leo (Aprili 4 mwaka huu) na Rais wa TFF, Leodegar Tenga katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washirika mbalimbali wakiwemo wachezaji, viongozi wa mpira wa miguu, Serikali, klabu na Wahariri wa Michezo.

Rais Tenga amesema mpango huo unafuatia ule wa 2004-2007, na 2008-2012 ambayo ilitengenezwa kwa msaada wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Mpango wa sasa umetengenezwa na TFF kwa kufuata mpango mfano (standard plan) wa FIFA.

Amesema mpango wa sasa ni wa kiufundi zaidi kwa vile umelenga kuendeleza mpira wa miguu, kwani iliyotangulia ilihusisha zaidi kutengeneza muundo wa TFF, kazi ambayo imekamilika kwani sasa shirikisho lina vyombo mbalimbali vya kusimamia mchezo huo.

“Wakati ule tulikuwa na Ligi Kuu tu, lakini tumeongeza mashindano ya aina mbalimbali kama U17, U20, Kombe la Taifa na sasa michuano ya Copa Coca-Cola itakuwa ya U15. Pia tukatengeneza Kanuni za Fedha, kilichomo katika mpango wa sasa ni kujenga mpira. Chombo (TFF) tayari kipo,” amesema.

Rais Tenga amesema TFF imefika hapa kutokana na watu kujitolea ambapo ametaka moyo huo uendelezwe, lakini akasisitiza washirika wote kuwa na mpango huo na kuusoma kwani umetokana na maoni yao ambapo kila mmoja ana kazi ya kufanya katika mpango huo.

“Naomba washirika wote wasome mpango huu. Kama mtu una mawazo zaidi baada ya kusoma, toa maoni yako. Mpango huu si Msahafu, utabadilika kutokana na maoni ya watu. Kama una mawazo zaidi, toa maoni yako kwa lengo la kujenga, isiwe kazi ya kulaumu tu kuwa mpango una upungufu. Mabadiliko yanafanyika kutokana na mawazo mapya,” amesema.

Amesema maendeleo ya mpira wa miguu ni mchakato mrefu, kwa hiyo unahitaji ushiriki wa watu kutokana na ukweli kuwa uongozi wa mpira wa miguu Tanzania bado ni wa kujitolea.

Rais Tenga amesema ahadi ya TFF ni kushirikiana na washirika mbalimbali kuhakikisha kuna maendeleo kwa faida ya mpira wa miguu wenyewe na nchi kwa ujumla.

Amewashukuru wote waliotoa maoni kwa ajili ya mpango huo wenye kurasa 76. Mpango huo ulioandaliwa na Mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni na Ofisa Maendeleo wa TFF, Salum Madadi unapatikana kwenye CD na nakala laini (soft copy).

Mheshimiwa Temba ebu Toroka Uje

Mhe Temba


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Aman Temba 'Mheshimiwa Temba' amevunja ukimya kwa kufyatua wimbo wake mpya uitwao 'Toroka Uje'.
Katika wimbo huo Mhe Temba ameimba akishirikiana na wasanii  Aslay Is'haka 'Dogo Aslay' na Yessaya Ambikile 'YP'.
Huo ni wimbo wa kwanza kwa Temba tangu alipotoa kazi yake ya mwisho mwaka jana iitwayo Mariyo alioimba pamoja na Cheka Hija 'Bibi Cheka'.
Meneja wa kundi la TMK, Said  Fella alisema wimbo huo wa Temba unaozungumzia kijana anayemsihi mpenzi wake atoroke ili wakajirushe umetoka sambamba na video ya Aslay iitwayo 'Wahenga'.
Fella alisema kama zilivyo kazi za nyuma ya Temba wimbo huo ni moja na nyimbo kali ikizingiatiwa vichwa alivyoimba navyo ambavyo vimeutendea haki.
"Baada ya kimya kirefu tangu atoe ngoma yake ya Mariyo aliyoimba na Bibi Cheka, Mheshimiwa Temba amechia wimbo mpya uitwao 'Toroka Uje', " alisema Fella.
Fella alisema video ya wimbo huo ipo njiani ikiendelea kurekodiwa, huku video ya wimbo wa 'Maneno ya Wahenga' ya msanii Dogo Aslay imeshatoka rasmi.

MAZISHI YA WAKILI NYAGA MAWALA KATIKA PICHA NCHINI KENYA


Mwili wa marehemu Nyaga poul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa 
SHUKRANI FATHER KIDEVU
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Chadema ni miongoni mwa waombolezaji waliokuwa kanisani nchini Kenya.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro Nyarandu na Sir George kahama wakiwa kanisani wakishiriki misa ya maziko ya marehemu Nyaga Mawalla.
****
Mazishi ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Makampuni ya Mawalla ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi Kenya katia Makaburi ya Jumuia ya Langata.

Mapema kabla ya Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika Kanisa la KKKK, Uhuru Highway. 

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria Mazishi hayo ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama, Mwemyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria mabalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Marehemu Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwaa amelazwa kwa matibabu  Hospitali ya Nairobi.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Buriani akiwa na mwanasheria maarufu Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya uwakili ya Law /Access Advocates Mosses Mahuna wakiwa nje ya kanisa la Lutherani nchini Kenya.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro wilani Simanjiro mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Laurence Marsha wakiwa kanisani nchini Kenya maziko ya marehemu Poul Mawalla

Kiongozi wa Dini wa Kanila la Kilutheri Kenya la Uhuru Highway akiongoza Mazishi.
 Sir George Kahama na mkewe wakiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Nyaga Mawalla.

 Familia ya Marehemu Nyaga Mawalla wakiwa wenye simanzi nzito wakati wa Mazishi hayo.
 Jaji Mark bomani nae alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki mazishi hayo.
 Baadhi ya jamaa wa karibu wa Marehemu Nyaga ambao ni wabunge wakiweka Shada la Maua
 Mwenyejiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mkewe wakiweka shada la maua
 Wabunge na Mawaziri mbalimbali wa serikali ya Jamhurti ya Muungano wa Tanzania, wakiweka mashada ya maua.
 Wanafamilia wakiweka mashada ya maua
 Watoto wa Marehemu Nyaga wakiwa na ndugu zao.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, dk. Batilda Buriani akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Nyaga.