STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, November 27, 2014

Waziri wa Nishati ajitetea bungeni kuhusu jinamizi la Tegeta Escrow


profmuhongoWAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewasilisha utetezi kwenye Bunge la Jamhuri kuhusiana na kutajwa kwake kuhusika na sakata ya wizi wa mabilioni ya fedha la Tegete Escrow.
Awali Waziri huyo alianza kwa kuomba radhi kama jana kulikuwa na usumbufu wa umeme na anawaagiza mameneja wote wa TANESCO wasikate umeme.
Anatoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow, mengi yamesemwa na ni wakati wa kuanza mjadala kujua ukweli, Shukrani kwa CAG, TAKUKURU kwa uchunguzi. Pia nawashukuru PAC, jana tulitulia kuwasikiliza PAC na leo tutulie tusikilize utetezi wangu.
Miaka ya 1990 tulikuwa tuna upungufu wa umeme kutokana na maji, 1994 serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa inamilikiwa na VIP ya Tanzania iliyokuwa na 30% na Mechmar ya Malaysia 70%.

Kulingana na mkataba, majukumu ya IPTL yalikuwa kujenga, kumiliki na kuendesha hivyo utaifishaji utaiingiza serikali katika matatizo makubwa ikiwemo kushtakiwa kimataifa pia itafukuza wawekezaji binafsi. TANESCO na IPTL walisainiana mkataba wa miaka 20, hata hivyo uzalishaji haukuanza mara moja kutokana na mgogoro ulioibuka baina ya TANESCO na IPTL
IPTL ilianza kuzalisha umeme 2002 hivyo mkataba ukaanza kuhesabiwa hapo, kutokana na mgogoro ikafunguliwa Escrow Account na Escrow ilizungumziwa toka mkataba wa 1995.Kusoma zaidi bofya

2004 TANESCO ilifungua shauri kupinga tozo la capacity charge

Taarifa hii sio ya kweli kwani TANESCO haijawahi kufungua kesi yoyote dhidi ya Standard Charted kama ilivyosemwa na PAC. Kesi hiyo ilifunguliwa na Standard Charted na ilikuwa haihusu capacity charge. Hamna kokote mkataba kati ya Standard Charted na TANESCO.
Makinda ameingilia na kusema ripoti itatolewa baada ya wabunge kudai ripoti hiyo.
Muhongo anaendelea
Uwiano wa mtaji ni 70 kwa 30, na uamuzi haujabadilishwa na mahakama yoyote. 2004 kampuni ya Mkono and CO Advocates iliishauri TANESCO iendelee kupinga capacity charge London. Hata hivyo, haikuishauri TANESCO kufungua kesi za TANZANIA wala mahakama ya kimataifa. Hadi 2013 Jaji Utamwa anatoa hukumu ya mgogoro wa wanahisa wa IPTL kulikuwa hamna kesi yoyote kuhusu tozo ya IPTL.
UUZAJI WA HISA ZA VIP
Kutokana na kutokubaliana Mechmar iliishauri VIP ifungue shauri. VIP ilifungua shauri Tanzania ikiomba IPTL ifilisiwe. Uamuzi ulitolewa kwa shauri la VIP. Chini ya Kimario, alpewa mfilisi wa muda kulinda mali za IPTL, kufanya uchunguzi ili mahakama iweze kutoa uamuzi. Uamuzi ulitoka IPTL iweke kwenye ufilisi kamili chini ya RITA. Hukumu ilipingwa mahakama ya rufaa ikianisha dosari katika uamuzi wa mahakama kuu na Standard Charted Hong Kong. Mahakama ya rufaa ilikubaliana na hoja hiyo na ilipelekwa tena kwa mfilisi wa muda kukusanya madeni, kusuluhisha mogogoro na kuendesha mitambo ya IPTL kwa niaba ya IPTL.

Serikali haiwajibiki kuingilia hisa za makampuni binafsi, mauzo ya hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu endapo yatatambuliwa na BRELA. Uhamishaji wa hisa 7 ulisajiliwa hapa nchini. Kamati katika uthibitisho huo inakubali hisa za Mechmarr unamilikiwa na PAP.
Hisa saba za IPTL zinatambuliwa pia na Standard Charted, Kama PAP haimiliki asilimia sabini kwa nini wana makubaliano na Standard Charted ya Uingereza?
Ilifilisiwa Malaysia na sio Tanzania, madai ya Standard Charted dhidi ya TANESCO ni kwa sababu IPTL waliweka dhamana mtambo wa kuzalishia umeme, Lakini benki ya Hong Kong ilikosa sifa ya kufungua shauri Tanzania hivyo ilifungulia Uingereza.
VIP chini ya usuluhishi wa RITA iliuza hisa zake PAP kwa dola milioni 70 na ndivyo ilivyomaliza mgogoro wa IPTL. Mimi sio dalali wa hii biashara bali ni dalali wa (anasema mambo mazuri aliyoyafanya)
Makinda amekuwa mkali kidogo kwa Muhongo asome taarifa na asiseme ambayo hayamo.

AKAUNTI YA ESCROW
TANESCO kwa ushauri wa Mkono walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme na makadirio ya mtaji walitoa notisi (Invoice disputes notice) ya kupinga usahihi wa malipo. Alietoa ushauri ni kampuni ya Mkono, 2006 serikali ulisaini mkataba wa kufungua Akaunti ya Escrow.

MMILIKI WA FEDHA YA ESCROW
Akaunti ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa na TANESCO. PAC walitoa mapendekezo kuwa imethibitisha kuwa mchakato wa kutoa pesa Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kutakatishwa na benki mbili

TAHADHARI ZILIZOCHUKULIWA
Serikali ilichukua kinga kutoka IPTL, kwa mujibu wa kinga IPTL itawajibika yakitokea madai yoyote na ilipitiwa na mwanasheria mkuu wa serikali. (Yoyote anaedai chochote aende IPTL)

PAC wameeleza serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha juu ya madai mapya kama yangejitokeza kitu ambacho sio kweli.
DHANA YA MADAI YA BILIONI 321
Madai kwamba IPTL inaidai 321 Bilioni, bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG hakionyeshi madai haya.

Madai yaliyowasilishwa na mufilisi, yalitakiwa kuhakikiwa lakini hayakuhakikiwa na hayakuwa na uhalali wowote.
Kamati ya PAC, wamesema yana uhalali japo uhalali wake unategemea maamuzi.
MADENI TANESCO
Wazri Muhongo amesema Tanesco haijaanza kutengeneza pesa kwa manufaa ya Umma ina madeni. Hivyo hamna fedha za umma popote kuna madeni tu.

MWANASHERIA WA TANESCO

Prof. Muhongo amesema Mwanasheria wa Tanesco anayedaiwa kufukuzwa kazi taarifa hiyo si ya kweli na bwana huyo amedanganya umma.
Ukweli ni kwamba Mwanasheria huyo alileta ombi la kusafiri kwenda Malaysia kwa kumdanganya mwajiri wake kwa kuandika barua kuwa anakwenda na Mwanasheria Mwandamizi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Hivyo hakufukuzwa kazi bali aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa kumwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco mwezi Februari mwaka huu#TegetaEscrow
BUNGE LAAHIRISHWA

Spika wa Bunge, Anne Makinda ameahirisha kikao cha bunge mpaka jioni saa 11 baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo kumaliza kutoa utetezi wa serikali.
Chanzo:Mwananchi.

Newz Alert! Watu 11 wapoteza maisha katika ajali mjini Tanga


Taswira kutoka eneo la Mkanyageni baada ya ajali hiyo mbaya iliyoua watu 11.

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa watu 11 wamefariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali mbaya eneo la Mkanyageni mkoani Tanga.
Inadaiwa kuwa ajali hiyo ilisababishwa na gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 410 BJD kugongana na Scania namba T 605 ABJ asubuhi hii.
Katika ajali hiyo, Coaster lilikuwa likitoka mkoani Tanga kwenda Lushoto na madereva wa magari yote mawili hawajulikani walipo baada ya ajali.
Miili ya marehemu katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, Tanga.

Taarifa zaidi zitawajia baadaye ila MICHARAZO inatoa pole kwa wote walioguswa na ajali hiyo na kuwaombea waliitangulia mbele ya Haki Roho zao ziweke mahali Pema na majeruhi wapone haraka.

Arsenal yasonga mbele, Liverpool yabanwa Ulaya, Real yaua

The Arsenal players celebrates the French youngster's early goal in the Champions League Group D clash

Alexis Sanchez runs towards the Arsenal fans in celebration of his second-half strike against Borussia DortmundGerrard wins a tussle for the ball with Marcelinho (left) of  Ludogerets at the Vasil Levski StadiumLambert celebrates with Joe Allen as his goal made it 1-1 at the at Vassil Levski StadiumIt wasn't just fans Ronaldo had to watch out for as he is tackled hard by Basle's Fabian Schar during the gameBale gets in front of his man from a corner but is unable to find the back of the net for RealRonaldo wheels away after bundling home from close range to give Real the 1-0 lead at St Jakob ParkWAKATI Arsenal wakitinga hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata ushindi nyumbani, Liverpool imejikuta ikibanwa ugenini kwa kuambulia sare.
Arsenal walipata ushindi muhimu nyumbani dhidi ya Borussia Dortmund kwa kuwalaza mabao 2-0 wakati Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogorets .
Mabao ya Yaya Sanogo na jingine la Alexis Sanchez yalitosha kuivusha Arsenal hatua hiyo katika mechi kali iliyochezwa uwanja wa Emirates.
Arsenal imeungana na Wajerumani hao kutinga hatua ya 16 Bora kutoka kundi D baada ya kufikisha pointi 10, tatu nyuma ya Dortmund inayoongoza kileleni.
Nao Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogoretsna kuzidi kujiweka pabaya katika azma yao ya kucheza hatua ya mtoano.
Ludogorets waliwashtukiza wageni wao kwa kupata bao la mapema la dakika tatu kupitia Dani Abalo kabla ya Liverpool kusawazisha dakika tano baadaye kupitia Rickie Lambert na baadaye Jordan Henderson kuwapa uongozi wa 2-1 wageni.
Hata hivyo Vijogoo vya England walishindwa kulinda bao lao baada ya kuruhusu wenyeji kusawazisha dakika mbili kabla ya mchezo huo kumalizika baada ya Georgi Teziev kuifuingia Lodogorets.
Sare hiyo imeifanya Liverpool kufikisha pointi nne na kushika nafasi ya tatu ikitanguliwa na Basel iliyolazwa  bao 1-0 na Real Madrid iliyotangulia 16 Bora ikiongoza kundi B.
Bao la Real lilifungwa na Ronaldo na kumfanya Mreno huyo kumfikia Raul katika orodha ya waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo wakishika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi anayeongoza kwa mabao 74 dhidi ya 71 na wakali hao.
Katika mechi nyingine Zenit iliitambia Benfica kwa kuilaza bao 1-0, huku Atlético Madrid ikiendeleza rekodi yao ya kutofungwa uwanja wa nyumbani kwa kuicharaza Olympiakos Pirates kwa mabao 4-0 na kufuzu 16 Bora.
Wakali wa Italia, Juventus wakipata ushindi muhimu ugenini dhidi ya Malmo, huku Monaco ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya   Bayer Leverkusen, huku Anderlecht ikiinyoa Galatasaray kwa mabao 2-0.
Mpaka sasa wakati michuano hiyo ikisaliwa na raundi moja kabla ya kufikia tamati hatua ya makundi timu nane ndizo zimejihakikisha hatua inayofuata zitakazochezwa mwezi ujao.
Timu hizo ni pamoja na Atletico Madrid, Real Madrid na  Barcelona zote za Hispania, Chelsea na Arsenal za England, Bayern Munich na Borussia Dortmund za Ujerumani, PSG ya Ufaransa, POrto ya Ureno na Shakhtar Donetsk ya Uturuki.

Real Madrid, Bayern waongoza tuzo za Kikosi Bora Ulaya

http://english.ahram.org.eg/Media/News/2014/4/24/2014-635339446265357238-535.jpgKLABU ya Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wamethibitisha ubora na thamani yao baada ya kutoa wachezaji nane katika uwaniaji wa tuzo ya kikosi bora cha Ulaya.
Tuzo hiyo ya Uefa ya mwaka 2014 itakayotolewa hivi karibuni inajumuisha pia wachezaji wanne kutoka AtleticoMadrid ambao pia wanaiwania.
Wanaowania kuingia kwenye 1st Eleven ya mwaka ya Uefa ni kama ifuatavyo;
Kutoka Madrid : Carvajal, Ramos, Kroos, Modric, James, Bale, Benzema na Cristiano Ronaldo.
Bayern wenyewe wametoa wachezaji sawa kama Real Madrid nao ni Neuer, Alaba, Benatia, Boateng, Lahm, Xabi Alonso, Müller na Lewandowski.
Upande wa Atletico Madrid iliyotoa wachezaji wanne ambao ni Koke, Arda, Godín na Miranda.
Wengine waliopo kwenye kinyang'anyiro hicho ni Xabi Alonso (Bayern Munich) na Di María (Manchester United), Courtois (Chelsea), Diego Costa (Chelsea).
Kwa upande wa Barcelona imetoa wachezaji watatu ambao ni Rakitic, Neymar na Messi. Pia mchezaji wa Red Bull Salzburg Jonathan Soriano naye yupo kwenye mbio hizo za kuwepo kwenye First Eleven.