STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 7, 2013

Mark Band, Pembe wafyatua nne wakienda kurudia za zamani Ulaya

Rashid Pembe akionyesha makeke yake kwa mashabiki ughaibuni
Rashid Pembe (kulia)
 BENDI iliyojikita kwenye muziki wa asilia ya Mark Band, imekamilisha nyimbo nne kwa ajili ya albamu yao ya pili mpya walioyopanga kuitoa Desemba mwaka huu, wakati wakiwa katika maandalizi ya kurudia nyimbo za albamu yao ya kwanza barani Ulaya.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Rashid Pembe 'Professa', aliiambia MICHARAZO kuwa, nyimbo mbili za mwisho za albamu hiyo mpya zinatarajiwa kutenmgenezwa nchini Chile na kurekodiwa Ufaransa kabla ya kufanyiwa uzinduzi jijini Dar.
Pembe, nyopta wa zamani wa bendi ya Vijana Jazz, alizitaja nyimbo hizo nne zilizokamilika kuwa ni Tanzania Yetu na Kibule zilizotungwa na yeye (Pembe), Amani wa Balusi Kitembo na Nasoma Namba wa Noel Msuya.
"Nyimbo mbili za mwisho tutaenda kuzimalizia tukiwa kwenye ziara yetu nchini Chile na kuzirekodia Ufaransa, lakini pia tumepanga kurudia upya nyimbo za albamu yetu ya kwanza ambayo imechangia kutupatia mialiko Ulaya na Amerika," alisema.
Alisema wamelazimika kuzirudia upya nyimbo hizo kwa ushauri wa wadhamini wao barani Ulaya ili kuzifanya ziwe na kiwango za kimataifa na kuzidi kujizolea soko nje ya nchi.
Pembe, mkali wa kupuliza 'domo la bata' alizitaja nyimbo zitakazorudiwa Ulaya ambazo ziliitambulisha bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 ni 'Matukio', 'Baba Kaleta Panya', 'Slow Puncture', 'The Girl from Tanzania', 'Amani Tanzania' na 'Angela'.

Zola D 'kuparii in da house' Mombasa

Mkali Zola D katika pozi
NYOTA wa muziki wa Hip hop nchini, David Mlope 'Zola D' amekamilisha wimbo wake mpya uitwao 'Party in da House' na kwa sasa amekimbilia Mombasa Kenya kwa ajili ya kurekodi video yake.
Akizungumza na MICHARAZO, Zola D staa wa nyimbo za 'Moto wa Tipper', 'Rap Gangester', 'Msela Sana' na Jana Siyo Leo', alisema ameamua kwenda kurekodi video hiyo Mombasa kwa lengo la kuipa mandhari tofauti.
Alisema, ndani ya wimbo huo ameimba na 'dogo' aitwaye Man DVD ambaye pia ndiye mzalishaji wa wimbo huo ambao alidai video yake itaachiwa hadharani ndani ya mwezi mmoja ujao baada ya kukamilika kwake.
"Natarajia kuachia 'ngoma' yangu mpya ya 'Party in da House' ambayo nimpigiwa 'chorus' (kibwagizo) na Man DVD na video yake naenda kuirekodia Mombasa Kenya kwa nia ya kuipa ladha na mandhari tofauti na kazi zangu za nyuma," alisema Zola D.
Msanii huyo mwenye 'mwili jumba' na anayejishughulisha pia na mchezo wa ngumi, alisema kazi hiyo mpya ni kati nyimbo zitakazokuwa katika albamu yake ijyao itakayofahamiaka kama 'Swahili Hip Hop'.