STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 1, 2014

Real Madrid yapiga mtu 4-0, Atletico yatakata pia

Karim Benzema
Benzema akiwajibika
Real Madrid
Ronaldo akipongezwa na wenzake
CHRISTIANO Ronaldo ameendeleza rekodi yake ya mabao baada ya usiku huu kuifungia timu yake ya Real Madrid bao moja wakati wakipata ushindi wa mabao 4-0 ugenini dhidi ya Granada.
Ronaldo alifunga bao lake la 17 katika mechi 10 na kutimiza mabao 23 katika mechi 12 za michuano yote ya msimu huu mpaka sasa 9 katika dakika ya pili ya mchezo kabla ya James Rodriguez kufunga mengine mawili na Karim Benzema kumaliza udhia na kuipa madrid ushindi huo mnono.
Majirani na wapinzani wa jadi wa Real, Atletico Madrid wakiwa nyumbani walipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Cordoba.
Mabao ya washindi yalifungwa na Delgado Pacheco aliyejifunga dakika ya 43 kabla ya wageni kusawazisha kupitia kwa Ghilas dakika ya 53 na Griezmann kuongezea wenyeji bao dakika tano baadaye na Mario Mandzukic kufunga bao la tatu na Raul Garcia kuhitimisha bao la nne kabla ya Ghilas kufunga bao la pili la Cordoba.
Hivi Barcelona wapo uwanja wa nyumbani kuumana na Celta Virgo na matokeo bao 0-0.

Yanga yazamishwa Kaitaba, Simba bado sana

http://3.bp.blogspot.com/-kvyq9j_cUf0/VC5oK7s0DII/AAAAAAAARPs/1fj3HZWqogE/s1600/Simba%2B1.jpg
Simba walioendeleza sare zao katika ligi
http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2014/10/YANGA-MPYA-2014.jpg
Yanga waliolala Kaitaba
http://4.bp.blogspot.com/-wPbMKQIh7Ro/VBlv3SF4NOI/AAAAAAAAMDk/MTl9WBo8abU/s1600/DSC_0805.JPG
JKT Ruvu walioshindwa kulicheza gwaride la Polisi Moro
WAKATI klabu ya Simba ikiendeleza wimbo lake la sare, watani zao Yanga wamezamishwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kulazwa bao 1-0 na Kagera Sugar, huku maafande wa JKT Ruvu wakilala uwanja wa Chamazi ikiwa ni wiki moja tangu wavunje rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam.
Simba ikiwa kwenye uwanja wa Jamhuri ililazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar na kuendeleza rekodi yao ya kutoshinda katika michezo 12.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Joseph Owino, Nahodha wa vijana wa Msimbazi, kabla ya wenyeji kuchomoa bao kupitia kwa Mussa Hassan Mgosi, huku beki wa zamani wa Yanga, David Luhende akikosa penati ambayo ingeweza kuisaidia Mtibwa kuibuka na ushindi.
Mjini Bukoba, Yanga ikiwa na furaha ya kushinda 3-0 dhidi yha Stand United, ilijikuta ikichezea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar huku nahodha wake, Nadir Haroub Cannavaro akilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya dhidi ya mfungaji wa bao pekee la wenyeji, Paul Ngwai.
Kipigo hicho kimepokewa kwa masikitiko na kocha Marcio Maximo aliyelallamikia wachezaji wa Kagera kujaingusha na mwamuzi kutokuwa makini katika mchezo huo mbali na kulalamikia ubovu wa uwanja wa Kaitaba ambao umekuwa ukiisumbua Yanga kila mara kwa kuchezea kichapo.
Katika pambano jingine lililochezwa uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu ilizimwa na maafande wenzao wa Polisi baada ya kulala mabao 2-1.
Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Danny Mrwanda aliyefunga yote mawili na lile la wenyeji waliokuwa wametoka kushinda mechi mbili mfululizo likiweka wavuni na Jaffar Kisoki kabla ya Polisi kusawazisha na kuata la ushindi.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa pambano moja tu kati ya Mgambo JKT itakayokuwa wenyeji wa Mbeya City.

Chelsea, Arsenal, Southampton zaua England

Arsenal's Alexis Sanchez celebrates
Sanchez akishangilia moja ya mabao yake mawili leo
Oscar celebrates scoring for Chelsea against QPR
Oscar akiifungia Chelsea bao la kwanza
Victor Wanyama
Wanyama akiwa na wachezaji wenzake wakishangilia bao lake pekee la mapema lililotokana na shuti kali la umbali kama mita 40 na kuipa Soputhampton ushindi wa bao1-0 ugenini
VINARA wa Ligi Kuu ya England imezidi kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuizamisha QPR kwa mabao 2-1 na Arsenal kuifanyia mauaji Burnley kwa kuinyuka mabao 3-0.
Chelsea ikiwa uwanja wa nyumbani wa Stanford Bridge ilipata mabao yake kupitia kwa Oscar dakika ya 32 na mkwaju wa penati ya dakika ya 75 kupitia Eden Hazard na bao la wageni lilifungwa na Carlie Austin. Ushindi huo umeifanya Chelsea kufikisha mechi ya 10 ila kupoteza katika ligi hiyo.
Katika mechi nyingine Arsenal ilipata ushindi nyumbani wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley kupitia mabao mawili ya Alexis Sanchez na jingine la Alex Oxlade-Chamberlain.
Nayo timu ya Southampton imeendeleza wimbi lake la ushindi na kuifukuza Chelsea ikiwa nafasi ya pili baada ya kupata ushindi ugenini dhidi ya Hully City bao pekee likifungwa na Vincent Wanyama.
Everton ikiwa nyumbani iling'ang'aniwa na Swansea City na kutoka suluhu bila ya kufungana, huku West Brom wakipata ushindi mwembemba ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, huku West Ham United ikiwa ugenini ililazlmisha sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City.

Ndanda yaizamisha Azam, Ruvu yafa Tanga

Azam
http://3.bp.blogspot.com/-nY3zScmEEkY/VBSVhvCwAWI/AAAAAAABIus/bNF4CbtixRE/s1600/IMG-20140913-WA0029.jpg
Ndanda Fc
BAO pekee lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Toto Africans na African Lyon, Jacob Massawe lilitosha kuipa ushindi wa kwanza Ndanda ikiwa uwanja wake wa nyumbani kwa kuilaza mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam kwa bao 1-0.
Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa Azam baada ya mechi iliyopita mabingwa hao kufungwa bao 1-0 na JKT Ruvu na kuwaacha 'Matajiri' hao kusalia na pointi zao 10 baada ya kucheza mechi 7.
Ushindi huo umeipa faraja wenyeji Ndanda ambao walikuwa hawajapa ushindi wowote kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kufungfwa mechi mbili mfululizo na Ruvu Shooting na Mgambo Fc.
Katika mechi nyingine Prisons-Mbeya ikiwa ugenini mjini Shinyanga ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Stand United.
Prisons walianza kuandika bao mapema kupitia kwa Ibrahim Mamba kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Heri Mohammed.
Nayo timu ya Ruvu Shooting wamejikuta wakizimwa wimbi lake la ushindi baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.
Bao pekee la Wagosi wa Kaya liliwekwa kimiani na Itubu Imbem dakika ya 54,
Stand Utd-Heri Mohammed
Prisons-Ibrajim Mamba

Newcastle yaendeleza maajabu, yaizamisha Liverpool


Mario Balotelli akichezwa vibaya na mchezaji wa Newcastle Un ited leo
BAO pekee lililowekwa kimiani na Ayonze Perez limeifanya Newcastle United kuendeleza maajabu baada ya jioni ya leo kuilaza Liverpool bao 1-0.
Perez alifunga bao hilo dakika ya 73 na kuifanya timu hiyo ya Newcastle imepata ushindi wa tatu mfululizo baada ya kuinyuka Spurs na kisha kuivua taji la Capital One League, Manchester City.
Kipigo hicho kimezidi kuiweka pabaya Liverpool ambayo imeshindwa kuonyesha makali yake kama ilivyokuwa msimu uliopita ilipoonekana kama ingetwaa taji la Ligi ya England kabla ya kuzidiwa na Man City.

SINEMA YA TFF V NDUMBARO YAENDELEA


http://www.mwanaspoti.co.tz/image/view/-/2474914/highRes/843598/-/maxw/600/-/nj9aqaz/-/klabu.jpg
Jamal Malinzi Rais wa TFF
“OKTOBA 31 mwaka huu kupitia vyombo vya habari Wakili Damas Ndumbaro alitoa shutuma mbalimbali dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Tunapenda kuuleza umma wa Watanzania yafuatayo;
1.Hukumu dhidi ya Wakili Ndumbaro ilitolewa na chombo halali kwa mujibu wa Katiba ya TFF. Hivyo, TFF inatoa tahadhari kwa wanafamilia wa mpira wa miguu kutomhusisha Wakili Ndumbaro katika masuala ya mpira wa miguu katika kipindi hiki anachotumikia adhabu.
2.Hadi sasa TFF haijapokea rufani yoyote kutoka kwa Wakili Ndumbaro. Hii ni kwa kuwa kupitia barua yake kwa TFF aliagiza asikabidhiwe nyaraka yoyote kutoka TFF hadi Oktoba 30 mwaka huu, hivyo hukumu ya Kamati ya Nidhamu dhidi yake alikabidhiwa Oktoba 30 mwaka huu. Alichokifanya Wakili Ndumbaro ni kuleta TFF barua ya kusudio la kukata rufani.
3.Tuhuma za ubadhirifu wa TFF zilizotolewa na Wakili Ndumbaro si za kweli. TFF inatafakari hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua dhidi ya tuhuma hizi.
4.Mkataba wa TFF na TBL:
TFF inapenda kuwahakikishia wadau wa mpira wa miguu kuwa hakuna ubadhirifu wa aina yoyote katika matumizi ya fedha za mkataba wa TFF/TBL. TFF ingependa itoe kwa umma ufafanuzi wa vipengele vya mkataba huo na jinsi unavyoendeshwa lakini masharti ya mkataba huo (confidentiality clause) yanatuzuia kufanya hivyo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikutana na klabu za Ligi Kuu na kuzielekeza zikae na kujadili kanuni za Ligi, kisha zipendekeze maboresho ili yajadiliwe katika kikao kijacho cha Kamati ya Utendaji.
TFF inapenda kuchukue fursa hii kusisitiza umuhimu wa kufuata mifumo tuliyojiwekea katika kutatua matatizo/kero zetu mbalimbali, utulivu ni muhimu katika kuendeleza mpira wa miguu,”.
(IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MASHINDANO WA TFF, BONIFACE WAMBURA MGOYO)

Rasmi sasa! Rooney kuivaa Man City kesho

http://cdn.images.express.co.uk/img/dynamic/67/590x/Rooney-Lampard-goals-498076.jpg
Rooney na Lampard
IMETHIBITISHWA kuwa nahodha wa Man United, Wayne Rooney ataanza mechi ya kesho Jumapili dhidi ya Man City katika pambano la watani wa jadi wa jiji la Manchester.
Rooney amemaliza adhabu ya kadi nyekundu na imethibitika kuwa yupo fiti kwa pambano hilo, ingawa mkali mwingine Radamel Falcao hatacheza kwa sasa bado yu majeruhi.
Man Utd ikimkosa Falcon wenzao Man City watakaokuwa nyumbani uwanja wa Etihad watawakosa David Silva, Frank Lampard na Yaya Toure walio majeruhi, lakini samir Nasir atakuwapo dimbani.
Timu hizo zinakutana kesho katika pambano la Ligi Kuu ya England sambamba na mechi nyingine ya Aston Villa dhidi ya Spurs huku matokeo baina yao yakisomeka hivi:
2013-14 - Utd 0-3 City, City 4-1 Utd
2012-13 - Utd 1-2 City, City 2-3 Utd 
2011-12 - City 1-0 Utd, City 2-3 Utd (FA Cup), Utd 1-6 City
2010-11 - City 1-0 Utd (FA Cup), Utd 2-1 City, City 0-0 Utd,
2009-10 - City 0-1 Utd, Utd 3-1 City (FA Cup), City 2-1 Utd (League Cup), Utd 4-3 City

Kiemba, Chanongo wakacha 'Kitimoto' Msimbazi, Kisiga naye...!

Kiemba akichuana na Coutinho wakatia wa pambano la Simba na Yanga hivi karibuni
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/10/46.png
Haruna Chanongo (kushoto)
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/07/IMG_9835.jpg
Shabaan Kisiga
WACHEZAJI Amri Kiemba na Haroun Chanongo wameshindwa kutokea kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Simba SC kilichokua kifanyike jana ili kujitetea kutokana na kupewa adhabu ya kusimamishwa kusikojulikana huku wakiwa hawataoa udhuru wowote kama Shaaban Kisiga waliyesimamiwa naye.
Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva alisema kuwa Kiemba na Chanongo hawakutokea licha ya kutakiwa kufanya hivyo na wala hawajatoa taarifa yoyote, huku Kisiga akitoa udhuru.
“Tuliwaagiza wafike makao makuu ya klabu Saa 4:00 asubuhi (jana), lakini hadi saa 6:00 mchana walikuwa hawajafika na hawakutoa taarifa yoyote, kwa hivyo ikabidi Wajumbe wa Kamati ya Nidhamu watawanyike,”alisema.
Hata hivyo, Aveva alisema baadaye Kisiga alipiga simu kujieleza kwamba amekwama kwenye foleni na waakamuambia hana sababu ya kufika tena, kwa sababu kikao kimeahirishwa.
Alipoulizwa ni hatua gani watachukuliwa wachezaji hao, Aveva alisema; “Kwanza Kamati ya Nidhamu ilete ripoti ya maandishi kwa Kamati ya Utendaji juu ya kikao chao, baada ya hapo Kamati ya Utendaji itatoa uamuzi,”alisema.
Watatu hao, Shaaban Kisiga ‘Malone’, Amri Kiemba na Haroun Chanongo waliondolewa kwenye kambi ya Simba SC mapema wiki hii kwa sababu mbalimbali.
Kisiga alirejeshwa Dar es Salaam kutoka Mbeya kwa tuhuma za kutoa majibu ya kifedhuli kwa uongozi kabla ya mchezo na Prisons Jumamosi, wakati Kiemba na Chanongo wanatuhumiwa kucheza kwa kiwango cha chini.