STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 1, 2014

Wanachama MHCS Ltd wakabidhiwa vyeti vya hisa, viwanja Kibiki

Dk Rutabazibwa akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya MHCS Ltd, Ndesumbuka Merinyo Cheti cha Hisa katika sherehe hizo zilizofanyika Kibiki-Chalinze mkoani Pwani.
Dk Rutabazibwa akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya MHCS Ltd, Hellen Khamsini Cheti cha Hisa katika hafla hizo za Kibiki-Chalinze.
Dk Rutabazibwa akimabidhi chet cha Hisa mmoja wa wanachama wa MHCS Ltd, Zahir Mshana.

Dk Rutabazibwa akimkabidhi Cheti cha Hisa, Mwanachama wa MHCS Ltd, Mwanahawa Gambo katika sherehe hizo za Kibiki
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania, Dk Audax Rutabazibwa akikata utepe kuzindua ofisi mpya ya Chjama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge, zilizopo Kibiki-Chalinze
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo kutoka kushoto Diwani wa Bwilingu, Hamad Nassa, DC Ahmed Kipozi, Dk Audax Rutabazibwa aliyekuwa mgeni rasmi.
Mgeni ramsi akirudisha mkasi baada ya kuzindua ofisi mpya za MHCS Ltd Kibiki-Chalinze
Sehemu ya waliohudhuria sherehe hizo akiwamo mchekeshaji Erick Ivyoivyo
Mchekeshaji Mkono wa Mkonole akiwa na wanachama wa MHCS Ltd kwenye hafla hizo za Kibiki
Mgeni rasmi Dk Audax Rutabazibwa akitoka kwenye jengo la ofisi mpya ya MHCS baada ya kuzifungua rasmi
Viongozi waalikwa, Dk Rutabazibwa, Dc Kipozi na Diwani Nassa wakipata maelezo kwa mmoja wa viongozi wa MHCS Ltd baada ya kukagua vyumba vya jengo la ofisi mpya za MHCS Ltd-Kibiki
Mwenyekiti wa MHCS Ltd, Jonas Mwangomango (kushoto) pamoja na Mjumbe wa Bodi ya MHCS, Ndesumbuka Merinyo (rasta) wakiwaongoza viongozi wenzaop kutoka ndani ya jengo la ofisi yao mpya iliyopo Kibiki-Chalinze mkoani Pwani
Jengo la ofisi mpya ya MHCS Ltd baada ya kuzinduliwa rasmi na aliyekuwa mgeni rasmi Dk Audax Rutabazibwa
Safari ya kwenda kugawa viwanja kwa wanachama ikaanza ikiongozwa na MC Kiswaga
MC Kiswaga akimtambulisha mmoja wa wanachama aliyekabidhiwa kiwanja, Seleka Sanga (wa pili kulia) kwa Mgeni Rasmi, Dk Audax Rutabazibwa.
Mwanachama Seleka Sanga (Kushoto aliyeipa kamera mgongo) akikabidhiwa kiwanja chake
Zoezi limemaliza na msafara ukirudi eneo la mkutano kuendelea na mengine
Wanachama Seleka Sanga na Marieta Urassa (wa pili na tatu toka kulia) walipokabidhiwa viwanja vyao
Viwanja mlivyopewa mhakikishe mnaviendeleza au vipi?
Wakati wa Maakuli kila mtu na lunch box yake
Mwili haujengwi kwa matofali na simenti bali msosi wageni wakipata mlo
Mwanachama Dionis Mushi akihojiwa na wanahabari kuelezea faida alizopata kama mwanachama wa MHCS Ltd baada ya kupewa kiwanja chake Kibiki
Bi Hellen Mwanachama na Mjumbe wa Bodi ya MHCS Ltd naye akihojiwa kuelezea faida na matarajio yake ndani ya chama chao.
Mwanachama Zahir Mshana baadaya kukabidhiwa kiwanja chake na kuhojiwa alipozi kwa picha ya kumbukumbu
CHAMA cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge (MHCS Ltd) kimewakabidhi baadhi ya wanachama wake Vyeti vya Hisa.
Makabidhiano hayo yalifanyika juzi wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya ya chama hicho iliyopo Kibiki-Chalinze, mkoani Pwani ambapo wanachama wanne kati ya 385 walikabidhiwa aliyekuwa mgeni Rasmi Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk Audax Rutabazibwa.
Wanachama waliokabidhiwa vueti hivyio vya hisa ni pamoja na wajumbe wawili wa Bodi wa Uongozi wa chama hicho, Ndesumbuka Merinyo na Hellen Khamsini na wanachama wengine wawili, Mwanahawa Gambo na Zahir Mshana.
Pia katika hafla hiyo wanachama wengine wawili, Seleka Mshana na Marieta Urassa kwa niaba ya mumewe walikabidhiwa viwanja vyao kati ya viwanja zaidi ya 300 walivyokabidhiwa wanachama wa MHCS Ltd ikiwa ni mwanzo wa kuanza kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa na bora za wanachama wa chama hicho katika eneo hilo la Kibiki.
Katika hafla hizo zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kiposi, Diwani wa Bwilingu, Hamad Karama Nassa na viongozi wengine ambapo mgeni huyo kabla ya hapo alizindua ofisi hiyo mpya ya MHCS kwa kukata utepe na kuonyesha ndani kuliko kabla ya baada ya kujumuika na waalikwa eengine kupata chakula cha mchana.


No comments:

Post a Comment