STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 9, 2013

Francis Cheka, Chiotcha Chimwemwe patachimbika kesho Moro

Franci Cheka (kushoto) na Chiotcha Chimwemwe wakiutunishiana misuli
BINGWA wa IBF Afrika, Francis Cheka ameapa kutorudia makosa yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya na bondia Chiotcha Chimwemwe kutoka Malawi, huku akitamba amepania kumtwanga kwa KO ili kuondoa lawama kwamba katika pambano la kwanza alibebwa kwa kupewa ushindi jijini Arusha.
Cheka na Mmalawi huyo watavaana kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri katika pambano lisilo la ubingwa lililoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) likiwa ni maandalizi ya pambano lake la kuwania ubingwa wa WBF dhidi ya Mmarekani, Phil Williams badala ya Findley Derrick aliyetangazwa awali ambao mchezo huo utachezwa Agosti 30 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo kutoka Morogogo, Cheka alisema anamfahamu vilivyo mpinzani wake huyo ambaye licha ya kumshinda kwa pointi walipokuwa akitetea taji la IBF Desemba mwaka jana, alimjeruhi vibaya kiasi cha kuwa nje ya ulingoni mwa miezi miwioli akijiuguza.
Cheka alisema atapanda kwenye ulingo leo katika pambano hilo hilo la uzani wa Super Middle la raundi 10 akiwa na tahadhari kubwa dhidi ya mpizani wake ili kuhakikisha anamtwanga kwa KO, lakini pia asiumizwe kwa ajili ya pambano lijalo la kimataifa dhidi ya Mmarekani.
"Nashukuru naendelea vyema na mazoezi baada ya kurejea toka Kenya na nimejiandaa kumkabili Chimwemwe na kama mambo yataenda nilivyoanga nitampiga kwa KO kuondoa utata wa pambano letu la IBF ambapo nilimshinda kwa pointi lakini kukawa na lawama kwamba nilibebwa," alisema.
"Jingine ni kwamba Mmalawi huyu ana ngumi nzito hivyo nitakuwa na kazi kubwa ya kujihami ili asije akanijeruhi kama ilivyokuwa jijini Arusha kwa sababu nina pambano muhimu zaidi la kuwania mkanda wa WBF dhidi ya bondia toka Marekani," alisema Cheka ambaye tangu mwaka Agosti 2003 hajapoteza pambano lolote katika ardhi ya Tanzania akiwapiga mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Pambano pekee lililotibua rekodi ya kushinda mfululizo katika kipindi chote hicho lilikuwa ni la Machi mwaka huu alipopigwa nchini Ujerumani na Uensal Arik aliyemtwanga kitatanishi kwa TKO ya raundi ya 7 kati ya 12.