Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro |
Mbuyu Twite (kati) na Msuva wakimpongeza Cannavaro katika moja ya mechi ya timu yao ya Yanga. |
Yanga na Azam zinatarajiwa kuvaana Agosti 17 katika pambano la Ngao ya Hisani kufungulia pazia la msimu mpya wa ligi nchini, litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kuanza kwa kipute cha ligi hiyo wiki moja baadaye.
Akizungumza na MICHARAZO mapema asubuhi hii, Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro alisema kurejea dimbani kwa nyota hao kumewapa faraja na kuamini kuwa watavaana na wapinzani wao wakiwa wamekamilika.
Minziro alisema benchi lao la ufundi linaamini wachezaji hao watakuwa fiti kabla ya pambano hilo na mchezo wao wa kufungua dimba ya Ligi Kuu dhidi ya Ashanti United.
"Kurejea kwa wachewzaji wetu waliokuwa majeruhi kumetufa faraja kubwa kwa kuamini kuwa watakuwa fiti kabla ya mechi yetu ya Ngao ya Hisani na ile ya Ligi dhidi ya Ashanti United," alisema Minziro.
Aidha kocha huyo alisema anafurahishwa na namna wachezaji wao wanavyozidi kushika maelekezo yao kiasi cha kufanya vyema kwenye michezo yao ya kirafiki ya kujipima nguvu wakiamini wataendelea hivyo hata ligi itapoanza Agosti 24.
Minziro alisema pamoja na kikosi chaao kuifanya vyema bado wanazidi kuendelea kuwanoa kuhakikisha wanakuwa wakali zaidi ili kurejea mafanikio ya msimu uliopita wa kunyakua tena taji la Ligi Kuu kwa mara ya 25.
Alisema katika kujiweka fiti zaidi kesho wanatarajiwa kushuka dimbani tena kuvaana na Bandari Mombasa, mchezo aliodai huenda ukawa wa mwisho kwao kabla ya kujichimbia kambini kusibiri Azam na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kikisi hicho juzi liliifumua timu isiyojulikana ya 3 Pillars inayodaiwa kutoka Lagos, Nigeria kwa bao 1-0 siku chache baada ya kuilaza Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1.
No comments:
Post a Comment