STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 23, 2014

Hivi ndivyo roho za madenti watano zilivyopotea Mtwara

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen, akiwa ndandi ya  wodi namba moja katika Hospitali ya mkoa ya Ligula, alipokwenda kuwaona majeruhi wa ajali  ya  wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mustafa Sabodo, iliyotokea jana katika barabara ya Mtwara Lindi wakati wanafunzi wa shule hiyo wakikimbia mchakamchaka asubuhi. Kushoto Kaimu Katibu tawala wa Mkoa Smythies Pangisa. Katika ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili T174 AEB imesababisha vifo vya wanafunzi wanne na wengine 47 kujeruhiwa
 Mmoja wa majeruhi akipelekwa wodini baada ya kupokewa katika hospitali hiyo
 Kamanda wa Polisi, Zelothe Steven akizungumzia ajali hiyo
Kamanda Zelote akikagua gari lililohusika katika ajali hiyo 
 
Wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari ya Mustapha Sabodo iliyoko katika kijiji cha Msijute Halmashauri ya Mtwara Vijijini, mkoani Mtwara wamekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari wakati wakikimbia mchakamchaka jana alfajiri.

Wanafunzi hao walikufa baada ya kugongwa na gari aina ya Mercedes-benz namba T174 AED jirani na eneo la shule.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea alfajiri saa 11:40 katika maeneo ya shule hiyo barabara kuu ya Dar es Salaam-Lindi na kwamba gari hilo lililokuwa katika mwendo wa kasi, lilikuwa linaendeshwa na Baraka Mgengwe (50) wakati likitokea Mtwara kwenda Lindi.

Kamanda Stephen hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na mazingira ya ajali hiyo, mbali ya kusema kuwa wanafunzi hao walipatwa na mkasa huo wakati wakigeuka kurejea shuleni.
Alisema kuwa wanafunzi 21 walijeruhiwa huku wengine 26 waliopata mshtuko, walitibiwa kisha kuruhusiwa.
 

CCM yaonya watendaji wa serikali 'mizigo'


Mara baada ya kuundwa kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg. Abdulrahman Kinana mwanzoni mwaka mwaka jana, Sekretarieti hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya ziara mikoani kukutana na wananchi kusikiliza kero zao,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha Chama mikoani. Utaratibu huu ni agizo la mkutano mkuu wa Taifa wa nane wa CCM uliofanyika Novemba 2012 mjini Dodoma. Nanukuu azimio hilo;
 
“ Chama Cha Mapinduzi lazima kiwe karibu na wananchi, kisikilize changamoto zao na kiwasemee wananchi na hasa wanyonge” Moja ya maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa CCM 2012.
 
Kwa hiyo msingi wa kwanza wa ziara hizo ni maagizo ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambacho ndicho kikao cha juu kabisa cha Chama. Msingi wa pili ni ukweli kuwa CCM ndio iliyopewa dhamana na kuingia mkataba na wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015, hivyo inayowajibu wa kukagua utekelezaji wa ilani hiyo.
 
Na bila shaka wote tumeshuhudia jinsi ziara hizo zilivyoinua uhai wa Chama nchi nzima na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwenye maeneo yao, kiasi cha kuongeza imani ya wananchi kwa CCM.
 
Tumeshuhudia makundi mbalimbali ndani ya jamii yakija kueleza changamoto zao ndani ya Chama. Makundi hayo ni pamoja na makundi ya wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wanafunzi na wafanyakazi hasa walimu. Huu ni uthibitisho wa kuongezeka kwa imani yao kwa CCM.
 
Katika mwendelezo wa ziara hizo mwishoni mwa mwaka jana Katibu Mkuu wa CCM na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti walifanya ziara ya siku 26 katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Njombe. Pamoja na mambo mengine wananchi walilalamikia baadhi ya watendaji wa serikali hasa baadhi ya mawaziri wakiamini kuwa yapo mapungufu kadhaa yanayotokea kwenye wizara zao.
 
CCM kama lilivyo agizo la Mkutano mkuu la kuwasemea wananchi tulisikiliza kilio chao na kwa kufuata utaratibu, baadhi ya mawaziri hao waliitwa na kuhojiwa kwenye Kamati Kuu ya CCM mwezi Disemba 2013.

 Utaratibu wa watendaji wa serikali kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye vikao vya Chama sio mgeni na wala haujaanza jana. Wakuu wa wilaya hutoa kwenye wilaya, wakuu wa mikoa hutoa mikoani kwao,hivyo sio utaratibu mpya.
 
Baada ya mahojiano hayo Kamati Kuu ya CCM ilitoa ushauri kwa serikali wa namna ya kurekebisha mapungufu yaliyoelezwa na wananchi. Kwakuwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi mwenye mamlaka na mawaziri ni Rais mwenyewe, CCM ililiacha suala hili kwake aangalie njia ipi bora ya kuondoa mapungufu tuliyoyaeleza.
 
Na kwenye taarifa yetu kwa vyombo vya habari baada ya kikao hicho tulisisitiza kuwa sio lazima awafukuze mawaziri husika isipokuwa wanaweza kufanya mabadiliko katika mfumo,sheria nk ili mradi kuwepo na mabadiliko katika kushughulikia mambo yaliyolalamikiwa na wananchi.
 
Hivi karibuni Rais amefanya mabadiliko kidogo kwenye baraza lake la mawaziri na kuwarudisha baadhi ya mawaziri waliolalamikiwa na wananchi na wabunge, ambao malalamiko hayo yaliungwa mkono na CCM. Ni kupitia malalamiko hayo ndipo lilipozaliwa jina la mawaziri mizigo. Baada ya uteuzi huo kukaibuka mjadala mkubwa nchini wakihoji kulikoni Rais kaamua kutowatimua mawaziri hao.
 
Kwanza haikua hoja ya CCM kuwafukuza mawaziri hao bali kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu husika. Kufukuza inaweza kuwa ni njia ya kutatua tatizo lakini sio njia pekee. Hivyo basi CCM tunaamini kuwa kurudishwa kwao wamepewa fursa ya kurekebisha mapungufu tuliyoyasema kwa niaba ya wananchi. Tunaamini mawaziri wote hawatabweteka bali watatimiza wajibu wao na kuhakikisha wanawatumikia wananchi ambao ndio waajiri wa serikali.
 
Ifahamike kuwa Chama Cha Mapinduzi hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri na watendaji wengine watakaoshindwa kurekebisha mapungufu na watakaoshindwa kutimiza wajibu wao vizuri. Wakumbuke kushindwa kwao kutimiza majukumu yao ni hujuma kwa Ilani ya uchaguzi ya CCM, CCM haitavumilia usaliti huo. Kukaa kimya kwa CCM itakua ni kujinyonga yenyewe jambo ambalo hatutaruhusu kabisa.
 
Tunajua wapo baadhi ya watendaji wa serikali wasiopenda kuhojiwa utendaji wao, tunawasihi kwa moyo safi wasiotaka kuulizwa juu ya utendaji wao waondoke serikalini wenyewe kwani CCM tutakuwa wakali sana kwenye mapungufu,kwani tukikaa kimya tutakua tunajihujumu wenyewe.
 
Tutatumia vizuri wingi wa wabunge wetu bungeni na wingi wa madiwani wetu kwenye halmashauri kuisimamia vizuri serikali. Hivyo kuanzia sasa kasi ya CCM kuisimamia serikali, kuisifu itakapofanya vizuri na kukosoa itakapofanya vibaya itaongezeka mara dufu kwa kila ngazi.
 
Tunawaomba watanzania kwa ujumla tuwape muda wateule hawa wa Rais watimize wajibu wao, lakini tusisite kusema pale tutakapoona mambo hayaendi kama tunavyotarajia. Uwajibikaji wa kweli ndio msingi wa mafanikio na maendeleo yetu.
 
CCM inawatakia kila lakheri kwenye kutimiza wajibu wao. Tuna matumaini makubwa kuwa wote kwa pamoja hawataisaliti ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba hawatayaangusha matumaini ya wananchi kwa serikali yao.
 
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
 
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
23/01/2014

Burundi yahitimisha aibu ya CECAFA CHAN 2014


 * DR Congo yaiduwaza, robo fainali kuchezwa wikiendi
* Nigeria v Morocco, Ghana v DR Congo, Gabon vs Libya, Mali v Zimbabwe
http://cdn.spyghana.com/wp-content/uploads/2013/09/wpid-CHAN.jpg
Mwali anayegombewa Afrika Kusini
http://www.tellng.com/sites/default/files/styles/large/public/field/image/Nigeria-South-Africa-CHAN-2014.jpg
Nigeria
BURUNDI imehitimisha aibu kwa timu za CACAFA kwenye michuano ya Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) baada ya usiku wa jana kunyukwa mabao 2-1 na DR Congo.
Burundi wameungana na Uganda na Ethiopia kuondoka patupu kwenye michuano hiyo na kuziacha timu za ukanda wa Afrika Magharibi na Kaskazini zikiendelea kutamba baada ya kuingia timu sita kati ya nane zilifuzu robo fainali zinazotarajiwa kuanza wikiendi hii.
Timu hiyo iliyokuwa ikiongoza kundi hilo mpaka jana kabla ya mechi za mwisho za kundi D waliporomoka hadi nafasi ya tatu na kuzipisha Gabon na DR Congo kuhitimisha timu za mwisho za kucheza hatua hiyo.
Gabon waliitandika Mauritania mabao 4-2 na kuongoza msimamo wa kundi hilo ikiwa na pointi saba na kufuatiwa na DR Congo ikikamata nafasi ya pili na poonti zake sita.
Kwa matokeo hayo robo fainali itakayoanza Jumamosi kwa mechi mbili itashuhudia Nigeria iliyoshika nafasi ya pili kundi A ikicheza na Morocco walioongoza kundi B katika pambano litakalochezwa uwanja wa Cape Town na mshindi wa kundi A kabla ya usiku kufuatiwa na pambano la Mali dhidi ya Zimbabwe uwanja huo.
Jumapili Gabon watakwaruzana na Libya kwenye uwanja wa Peter Mokaba ambao usiku utashuhudia pia pambano jingine la kuhitimisha hatua hiyo kwa Ghana kupepetana na DR Congo.

Ezekiel Kamwaga, Asha Muhaji waula Simba

Msemaji mpya wa Simba, Asha Muhaji
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/10/IMG_14351.jpg
Katibu Mkuu mpya wa Simba, Ezekiel Kamwaga

https://scontent-a-lhr.xx.fbcdn.net/hphotos-prn1/t1/1535732_594844153918068_212668818_n.jpg
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akiwa na viongozi wapya a klabu hiyo
 KLABU ya Soka ya Simba imefanya mabadiliko ya sekretarieti yake pamoja na kutangaza tarehe ya kufanya Mkutano Mkuu maalumu. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kufanyika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji. 
Rage amesema nafasi ya Katibu Mkuu wa klabu sasa itashikiliwa na aliyekuwa ofisa habari wake Ezekiel Kamwaga akisaidiwa na Stanley Philipo, nafasi ya mhasibu ikibakia kwa Eric Sekiete akisaidiwa na Amina Kimwambi. 

Nafasi ya ofisa habari sasa itashikiliwa na Asha Muhaji huku meneja wa timu akiwa Hussein Mbozi na Issa Mathayo atakuwa msimamizi. 

Rage pia amesema katika kikao hicho wamepanga Machi 23 mwaka huu kuwa tarehe ya Mkutano Mkuu Maalumu ambao utakuwa na ajenda moja ya kuhusu mabadiliko ya katiba. 

Wakati huohuo Rage amesema wamepokea barua kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Kamati ya Hadhi za Wachezaji wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA ambayo inawataka klabu ya Etoul du Sahel hadi Januari 27 mwaka huu wawe wametoa maelezo kuhusiana na hela ya mshambuliaji Emmanuel Okwi.

Man Utd yakubali 'kuvunja' benki kumnyakua Mata


MANCHESTER United ambayo inauguza maumivu wa kung'olewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi (Capital One) usiku wa kuamkia leo, imekubali kulipa ada ya pauni milioni 37 ambayo ni rekodi kwa klabu ili kumnasa Juan Mata kutoka Chelsea.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho ameidhinisha dili hilo baada ya mazungumzo na maofisa wa klabu na sasa Mata anatarajiwa kufanyia vipimo leo na kusaini mkataba wa miaka minne na nusu.


Mtendaji mkuu wa Manchester United amekubali kuvunja rekodi ya klabu ya usajili kwa ajili ya Mata ili kuokoa msimu unaokwenda kombo kwao.
Vipigo saba katika Ligi Kuu ya England vimeiacha United ikiwa nyuma kwa pointi 6 kutoka nafasi ya nne kwanye msimamo wa Ligi ambayo ingewawezesha kushiriki Champions League msimu ujao – lakini kuongezeka kwa Mata kunatarajiwa kuleta uhai mkubwa.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi jana walitolewa na Sunderland kwenye michuano ya Kombe la Ligi kwa kufungwa mikwaju ya penati 2-1 baada ya kumaliza dakika 120 wakishinda 2-1 nyumbani na kulingana na Sunderland waliowafungwa kwao idadi kama hiyo.
Kitu kilichosikitisha ni kwamba katika penati tano walizopiga Man Utd walipata moja tu huku tatu zikishindwa kuingia kimiani.

TAFCA-Moro kuwanoa makocha wake


http://api.ning.com/files/E-3hkOytmSiV1f0RrlVwYA3qSUb*OfUU5gpbgURYDkApBKGPGI1oQQb0PulIlS105IT2f18yz8zvda5Tx7AMt6HQKDDNk2Hb/soka.jpg
Na Daud Julian
CHAMA  cha makocha wa mpira wa miguu Tanzania (TAFCA) mkoa wa Morogoro kimeandaa kozi ya kati kwa makocha wa mchezo huo inayotarajiwa kuanza kufanyika Februari 26, mwaka huu, mkoani hapa.

Akizungumza na mtandao huu, katibu  mkuu wa chama hicho, Hemed Mumba alisema maandalizi kwa ajili ya kozi hiyo itakayochukua siku kumi yanakwenda vizuri na kwamba tayari baadhi ya makocha wameshajiandikisha.

Mumba alisema lengo la kozi hiyo ni kuwaendeleza makocha wa mpira wa miguu mkoani Morogoro na mikoa mingine ili kuhakikisha mchezo wa soka unapiga hatua kubwa.

Alisema ada ya ushiriki katika kozi hiyo ni Sh.60,000 na mwisho wa kulipa ada hiyo ni Februari 16.

Katibu huyo alisema ada inatakiwa kulipwa kwa mweka hazina wa chama au katibu mkuu katka ofisi za chama hicho zilizopo ndani ya ofisi za chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) na mshiriki ahakikishe anapewa risiti.

“Maandalizi kwa ajili ya kozi hii yanakwenda vizuri na makocha wameanza kujitokeza lakini pia milango ipo wazi hata kwa makocha walio nje ya Morogoro kuja kuchukua mafunzo haya”, alisema.

Kozi hiyo ni ya kwanza kutolewa na chama hicho chini ya uongozi mpya ulioingia madarakani hivi karibuni chini ya mwenyekiti wake, John Simkoko.

Malinzi mgeni rasmi tuzo za Makocha

Rais wa TFF Jamal Malinzi
Na Daud Julian
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya tuzo ya makocha wa mpira wa miguu Tanzania inayotarajia kufanyika Machi 8, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu jijini Dar, Afisa Mtendaji wa tuzo hiyo, Fredrick Luunga alisema kamati ya maandalizi ya tuzo iliyokutana hivi karibuni ndiyo iliyopitisha jina la Malinzi kuwa mgeni rasmi siku hiyo.

Luunga alisema lengo la kumwalika kiongozi huyo wa juu wa soka ni kuthamini mchango wake katika kuendeleza mchezo huo hapa nchini na pia kumpa fursa ya kukutana na kuzungumza na makocha wa mpira wa miguu Tanzania na wadau wengine kupitia hafla hiyo.

Kuhusu maandalizi ya tuzo hiyo kiujumla, afisa huyo alisema yanakwenda vizuri na kwamba wapo katika mchakato wa kutafuta wadhamini zaidi.

“Maandalizi yanakwenda vizuri na kamati imekuwa ikikutana mara kwa mara kwa lengo la kupanga mikakati mbalimbali”, alisema.

Hata hivyo, Luunga ametoa wito kwa wafadhili wa michezo nchini kujitokeza na kudhamini tuzo hiyo itakayokuwa ikitolewa kila mwaka.

“Bado tunahitaji wafadhili zaidi ili kufanikisha utoaji wa tuzo hizo kwani lengo ni kuhakikisha makocha wa soka nchini wanathaminiwa kutokana na kazi zao wanazofanya katika taaluma ya ukocha”, alisema.

Wakati huo huo, afisa huyo alisema zoezi la kuwapigia kura makocha wanaostahili kupata tuzo hizo linaendelea kwa kuandika katika simu neno sokafasta acha nafasi kisha jina la kocha yeyote na tuzo anayostahili kupata kisha itumwe kwenda 15678.

Tuzo zinazotarajiwa kutolewa siku hiyo ni kocha bora wa mwaka 2013, kocha bora wa makipa, kocha bora mkongwe mwenye mafanikio makubwa, kocha bora chipukizi, kocha bora wa kike, kocha bora wa kigeni, kocha bora wa kigeni aliyewahi kupata mafanikio makubwa nchini na kocha bora Mtanzania anayefundisha soka nje ya nchi kwa sasa.