STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 23, 2014

Burundi yahitimisha aibu ya CECAFA CHAN 2014


 * DR Congo yaiduwaza, robo fainali kuchezwa wikiendi
* Nigeria v Morocco, Ghana v DR Congo, Gabon vs Libya, Mali v Zimbabwe
http://cdn.spyghana.com/wp-content/uploads/2013/09/wpid-CHAN.jpg
Mwali anayegombewa Afrika Kusini
http://www.tellng.com/sites/default/files/styles/large/public/field/image/Nigeria-South-Africa-CHAN-2014.jpg
Nigeria
BURUNDI imehitimisha aibu kwa timu za CACAFA kwenye michuano ya Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) baada ya usiku wa jana kunyukwa mabao 2-1 na DR Congo.
Burundi wameungana na Uganda na Ethiopia kuondoka patupu kwenye michuano hiyo na kuziacha timu za ukanda wa Afrika Magharibi na Kaskazini zikiendelea kutamba baada ya kuingia timu sita kati ya nane zilifuzu robo fainali zinazotarajiwa kuanza wikiendi hii.
Timu hiyo iliyokuwa ikiongoza kundi hilo mpaka jana kabla ya mechi za mwisho za kundi D waliporomoka hadi nafasi ya tatu na kuzipisha Gabon na DR Congo kuhitimisha timu za mwisho za kucheza hatua hiyo.
Gabon waliitandika Mauritania mabao 4-2 na kuongoza msimamo wa kundi hilo ikiwa na pointi saba na kufuatiwa na DR Congo ikikamata nafasi ya pili na poonti zake sita.
Kwa matokeo hayo robo fainali itakayoanza Jumamosi kwa mechi mbili itashuhudia Nigeria iliyoshika nafasi ya pili kundi A ikicheza na Morocco walioongoza kundi B katika pambano litakalochezwa uwanja wa Cape Town na mshindi wa kundi A kabla ya usiku kufuatiwa na pambano la Mali dhidi ya Zimbabwe uwanja huo.
Jumapili Gabon watakwaruzana na Libya kwenye uwanja wa Peter Mokaba ambao usiku utashuhudia pia pambano jingine la kuhitimisha hatua hiyo kwa Ghana kupepetana na DR Congo.

No comments:

Post a Comment