STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 28, 2014

Ronaldo ndiye Mchezaji Bora Barani Ulaya

http://www.free-top10.com/Data/Sites/1/Free/Free%20Video/Free-Video-Ronaldo-European-Football-Player-Of-The-Year.jpg 
http://www.sokkaa.com/wp-content/uploads/Neuer-Christiano-and-Robben.jpg
Waliokuwa kwenye Tatu Bora Ulaya
MSHAMBULIAJI nyota wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Ulaya.
Mkali huyo alipata tuzo hiyo baada ya kuwaangusha wachezaji wenzake wawili wanaoichezea Bayern Munich ya Ujerumani.
Ronaldo alitangazwa jioni hii kushinda tuzo hiyo mbele ya Arjen Robben na kipa Manuel Neuer wa Bayern Munich.

Haya ndiyo makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2014

MAKUNDI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yametangazwa jioni hii ambapo Mabingwa wa Engand, Manchester City wamejikuta wakiangukia kundi moja na Bayern Munich huku Liverpool ikiangukia kundi B lenye vigogo Real Madrid.
Kwa mara nyingine Arsenal wameangukia kundi gumu, safari hii wakiwa D lenye timu za Arsenal, 
Borussia Dortmund, 
Galatasaray na Anderlecht.
Chelsea wao wako kundi G lenye timu za 
Schalke, 
Sporting
 na Maribor.
Yacheki makundi yote hapo chini:
Kundi A


Atletico Madrid, Juventus,
 Olympiacos na 
Malmo
Kundi B
Real Madrid, 
Basle, 
Liverpool,
 Ludogorets
Kundi C
Benfica, 
Zenit St. Petersburg,
 Bayer Leverkusen na Monaco
Kundi D
Arsenal, 
Borussia Dortmund,
 Galatasaray na Anderlecht
Kundi E
Bayern Munich,
 Man City, 
CSKA Moscow na 
Roma
Kundi F
Barcelona, 
PSG, 
Ajax, 
Apoel Nicosia
Kundi G
Chelsea,
Schalke, 
Sporting
 na Maribor
Kundi H
FC Porto,
 Shakhtar Donetsk,
 Athletic Bilbao 
na BATE

Michel Platin achomoa kuwania Urais FIFA

KATIKA kinachoonekana kama kumgwaya Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, Sepp Blatter, Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya,UEFA, Michel Platini amesema hatagomea nafasi hiyo ya dunia kama ilivyokuwa ikivumishwa.
Platin amesea ni vyema kutilia mkazo kibarua chake cha sasa kuliko UEFA badala ya kushiriki uchaguzi huo wa FIFA.
http://static.guim.co.uk/sys-images/Football/Pix/pictures/2011/5/31/1306848649705/Michel-Platini-and-Sepp-B-007.jpg
Platin (kushoto) na Blatter
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa akiaminika kuwa anafikiria kugombea nafasi nhiyo lakini alifafanua katika mkutano wa vyama 54 vya soka barani Ulaya uliofanyika huko Monte Carlo kuwa atabakia katika nafasi yake hiyo.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA, Michel D’Hooge alikaririwa akidai kuwa ni ujumbe chanya uliotolewa na Platini na amefurahi kwani inamaanisha kuwa safari hii hakutakuwa na ushindani kati FIFA na UEFA. 
Platini amekuwa akimkosoa vikali Blatter kwa zaidi ya mara moja na mapema mwaka huu alieleza kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 amekwisha kama mtu sahihi wa kuiongoza FIFA. 
Blatter aliwahi kudai kuwa ataachia ngazi mwishoni mwa muhula wake huu wa nne lakini alibadili mawazo na uamuzi wake baadae na kuweka wazi kuwa atatetea tena kiti chake katika uchaguzi ujao. 
Blatter amekuwa akifanya kazi FIFA toka mwaka 1975 na alichaguliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi ya urais mwaka 1998.

Alexis Sanchez amkuna Wenger Arsenal

http://pbs.twimg.com/media/BuDK8W3IIAAy0Qv.jpgKIWANGO alichokionyesha mshambuliaji Alexis Sanchez kimemkuna Kocha wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger.
Meneja huyo wa Ze Gunners amesema kiwango cha Alexis Sanchez alichoonyesha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas imeinyesha kuwa ana ubora wa kumfanya afanikiwe katika Ligi Kuu nchini Uingereza.
Nyota huo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 35 akitokea Barcelona alifunga bao pekee katika mchezo huo na kuipa Arsenal ushindi mwembamba wa 1-0 katika Uwanja wa Emirates na kuwafanya kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Akihojiwa Wenger amesema Sanchez alionyesha mchezo mzuri kwani alikuwa akielewana vyema na wenzake na alikuwa akionyesha ari ya kupambana huku akiwa hatari anapokuwa katika lango la adui. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ubora huo ndio unaotakiwa katika ligi. Bao hilo la kwanza kwa mchezaji huyo toka ajiunge na timu hiyo alilifunga muda mchache kabla ya mapumziko na kuingiza Arsenal katika ratiba ya makundi yaliyopangwa leo.
Hata hivyo Wenger amekiri kuwa aliingiwa na woga kidogo wakati beki wake Mathieu Debuchy alipotolewa nje kwa baada ya kupewa kadi ya pili ya njano zikiwa zimebaki dakika 14 mpira kumalizika.

Kocha Mexime awakuna wachezaji Mtibwa Sugar

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVzufGN29F3EQO9M7DaKGF8TdIspdiztoQgVTGD8zWO2W1YB8ab9wJMCTc5-pqvYnHKlB2JLmq-wB7XAxld2-4Kh7Xb9sz0CVRFZKAKfjnWABu_wB-VYdQ1hq18g8-TqWULxVQIjQbjic/s1600/IMG_0621.JPG
Benchi la ufundi la Mtibwa Sugar
MSHAMBULIAJI nyota wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma amemwagia sifa kocha wake, Mecky Mexime huku akiitabiria Mtibwa kufanya vema kwenye msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Abdallah maarufu kama 'AJ' aliyeifungia Mtibwa mabao manne msimu uliopita ikiwamo hat trick wakati wakiizamisha JKT Oljoro, alisema tangu kocha wao amerejee toka masomoni amekuwa akiwapa mbinu ambazo zinawafanya kuzidi kuwa wakali na kufufua ari zao.
Nyota huyo wa zamani wa AFC Arusha, Kagera Sugar na Simba, alisema kwa namna kocha wao anavyowapa mbinu za kinazohusu mikasa aliyokutana nayo katika maisha yake.
"Kocha wetu ni kama 'amezaliwa' upya, yupo tofauti na msimu uliopita kwa jinsi anavyotupa mbinu mpya ambazo tunaamini zitaifanya Mtibwa Sugar itishe kwenye ligi ya msimu huu," alisema.
Abdallah alisema mpaka Septemba 20 ligi itakapoanza kwa wao kuwakaribisha Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri watakuwa wameiva na kuanza mbio zao za kurejesha heshima yao baada ya kushindwa kufanya vema ligi iliyopita.
Mshambuliaji huyo alisema anaamini msimu wa 2014-2015 utakuwa wa Mtibwa Sugar licha ya kwamba wadau wa soka wanaziangalia Simba, Yanga, Azam na pengine Mbeya City baada ya msimu uliopita kupanda Ligi Kuu na kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Misri yaongeza idadi inayowania AFCON 2017

CHAMA cha Soka nchini Misri kiomeongeza idadi ya nchi zinazowania uaandaaji wa Fainali za Afrika 2017 baada ya kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho Tanzania nacho imeingia tangu juzi.
Misiri ilianda mara ya mwisho fainali hizo mwaka 2006 na inawania nafasi hiyo na nchi nyingine baada ya waliokuwa wawe wenyeji, Libya kutangaza kujitoa.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini Libya viwalazimisha kujitoa kwa mara ya pili baada ya mwaka jana kushindwa na kuiachia Afrika Kusini kuandaa.
Kutokana na hali hiyo ambayo imeikwaza nchi hiyo kutekeleza mikakati ya ujenzi wa viwanja na kuifanya Shirikisho la Soka Barani Afrika-CAF kutafuta mwenyeji mwingine wa michuano hiyo. 
Chanzo kimoja cha habari kutoka ndani ya EFA kimebainisha nia ya kutaka kuwa mwenyeji wa michuano hiyo lakini bado hawajafanya uamuzi wa mwisho kuhusiana na suala hilo. 
Makamu wa rais wa EFA Hassan Farid naye alithibitisha nia yao hiyo lakini amesema bado wanataka kuzungumza na baadhi ya wizara serikalini ili kupata ushirikiano wao. 
Misri ni mojawpao ya nchi chake barani Afrika zenye miundo mbinu mizuri ya kuandaa michuano mikubwa kama Afcon.

Rooney nahodha mpya England Hodgson atangaza kikosi

http://static.guim.co.uk/sys-images/SPORT/Pix/pictures/2012/6/27/1340795627494/Roy-Hodgson-008.jpg
Sasa wewe ni nahodha wa kikosi usiniangushe, Kocha Hodgson akifurahia jambo na Rooney
NYOTA wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney ametajwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Uingereza Three Stars na kocha Roy Hodgson. 
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amechukua kitambaa hicho akimrithi kiungo wa Liverpool Steven Gerrard aliyestaafu rasmi soka la kimataifa baada ya nchi hiyo kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia. 
Mshambuliaji huyo nyota amefunga mabao 40 katika mechi 95 za kimataifa na alitajwa kuwa nahodha wa United na kocha Louis van Gaal mapema mwezi huu. 
Rooney alithibitisha uteuzi huo katika mtandao wake na kudai kuwa ataitumikia nafasi hiyo kwa bidii na kujivunia huku akidai kuwa zilikuwa ndoto zake za muda mrefu. 
Rooney ataanza kuvaa beji rasmi akiwa na timu ya taifa Septemba 3 mwaka huu wakati Uingereza watakapoikaribisha Norway katika Uwanja wa Wembley kwa ajili ya mchezao wa kirafiki wa kimataifa.
Kocha huyo amekitangaza kikosi cha wachezaji wake watakaocheza mechi hiyo na ile ya kuwania kufuzu EURO 2016 dhidi ya Uswisi akiwajumuisha wachezaji wanne ambao hawajawahi kabisa kuichezea timu hiyo.
Makinda hao waliotwa katika timu hiyo ni Jack Colback, Calum Chambers, Danny Rose na Fabian Delph, huku Andros Townsend akirejeshwa kikosini tena.
 
Kikosi kamili ni kama ifuatavyo; MAKIPA: Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)
MABEKI: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Everton)
VIUNGO: Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)
WASHAMBULIAJI: Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).

Eto'o, Xabi Alonso kama Lampard soka la kimataifa

http://www.tiemporeal.mx/files/image/0/416/5117b02d5f66c.jpg
Samuel Eto'o
frank-lampard-volley
Lampard
http://www1.pictures.zimbio.com/gi/Xabi+Alonso+Portugal+v+Spain+UEFA+EURO+2012+3JngxodQREjl.jpg
Xabi Alonso

SIKU chache baada ya Frank Lampard kutangaza kustaafu soka la kimataifa – jana ilikuwa siku nyingine kwa wanasoka wawili wa kimataifa barani nao walitangaza uamuzi wa kuachana na soka la kimataifa.

Samuel Eto’o na Xabi Alonso kwa wakati tofauti jana walitumia mitandao ya kijamii kutangaza uamuzi wao wa kuachana na soka la kimataifa.
Alianza Xabi Alonso kupitia mtandao wa Twitter kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Spain.
Kiungo huyo wa Real Madrid ameshaitumikia Spain kwa muda wa miaka 11 na ameifungia nchi hiyo magoli 16 katika mechi 114.
Wakati huo huo mfungaji mabao mengi zaidi wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu soka la kimataifa.
Mshambuliaji huyo ambaye ameifungia Cameroon mabao 56 amejiunga na Everton ya Uingereza juzi .
Kufuatia kauli hiyo mshambuliaji huyo sasa hatakuwepo katika kipindi chote cha cha kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari mwakani.
“Nataka kuwajuza kuwa nimestaafu mashindano yote ya kimataifa ”aliandika Etoo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram .

Bosi wa zamani wa TBS atupwa jela miaka mitatu

Charles Ekelege akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo ambapo alihukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kulipa faini ya sh.milioni 68.
Ekelege akiteta jambo na kijana aliyedaiwa kuwa ni mtoto wake.


 Ekelege akiteta jambo na familia yake akiwa Mahakamani hapo.

Hapa Ekelege akiwa amekaa nje ya Mahakama hiyo na familia yake  kabla ya kuhukumiwa.

 Askari polisi akiwa na familia ya Ekelege (wa pili kulia), wakati akitoka kwenye mahakama hiyo ----
Aaliye kuwa Mkurugenzi wa Shirika la viwango Tanzania TBS Bw Charles Hekelege, ametiwa hatiani na kufungwa miaka mitatu jela baada ya kukutwa na kosa la kuhujumu uchumi. Hekelege amefungwa jumla ya miaka mitatu jela kwa makosa matatu kila kosa moja mwaka mmoja kwa maana hiyo atatumikia mwaka moja gerezani.
www.habariza jamii.com

Afande Bright aachia mpya za Injili

Kava la albamu ya Afande Bright linavyoonekana kwa wanayoitaka wanaweza kuwasiliana kwa namba zinazoonekana chini kushoto kwenye kava hilo
Afande Bright katika pozi
MSANII aliyekuwa anakuja juu kwenye muziki wa kizazi kipya aliyejitosa kwenye muziki wa Injili baada ya kuponea chupuchupu kufa ajalini, Bright Mbwilo 'Afande Bright' ameachia albamu yake ya kwanza ya miondoko hiyo mipya iitwayo 'Ahsante Bwana'.
Akizungumza na MICHARAZO, Bright alisema albamu hiyo ambayo kwa sasa ipo sokoni wakati akijipanga kuitengenezea video yake, ina nyimbo nane.
Bright alizitaja nyimbo hizo ni 'Ahsante Bwana', 'Upendo', 'Vita', 'Hamjui', 'Itakuwaje', 'Twakuheshimu', 'Jinsi Gani' na 'Vita Remix', huku akisema karibu nyimbo zote ni simulizi la kweli zilizowahi kumpata au kuwapata watu wake wa karibu.
"Baada ya kunusurika katika ajali mjini Morogoro, nimeamua kumgeukia Mungu na sasa naimba muziki wa Injili nikiwa nimeachia albamu inayofanya vyema sokoni na kwenye vituo vya redio iitwayo 'Ahsante Bwana' yenye nyimbo nane," alisem Bright.
Aliongeza kabla ya kutumbukia kwenye muziki huo wa kumtukuza MUNGU alikuwa kiimba muziki wa kizazi kipya na aliwahi kutoa albamu moja iliyofanya vyema sokoni iitwayo 'Tanzania' iliyokuwa na nyimbo nane.
Baadhi ya nyimbo hizo ni 'Tanzania', 'Ndani ya Dancehall', 'Zako Style', 'Kiza Kinene', 'Jakaya', 'Nimedata', 'Hawapendi', 'Watanzania', 'Nikiachwa leo' na 'Leave Me Alone'.

TFF yaongeza usajili kwa saa 48

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNvkecPaytXUwsqfpHaifVRHqmPmJ_u0TP-5BxX76mv8bd84h44qP-FTYcfR-aTLu6MK4XJBsNnW1KVuBppUBi8WNFTZvzyTzC278WST8a4X69WDeqN5-BrLV3HnOv5-7VjeVRKHwumMds/s1600/DSC_0428.JPG
Viongozi wakuu wa TFF
DIRISHA la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa wachezaji wazalendo limesogezwa mbele kwa Saa 48 kuanzia jana, kutokana na timu kushindwa kukamilisha usajili katika muda husika jana.
Akizungumza leo jijini Dar Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa alisema sababu za kusogeza mbele ni klabu zote za Ligi Kuu kushindwa kukamilisha usajili jana.
“Nadhani wameshindwa kuutumia huu mfumo wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa 48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo hakuna nafasi tena, tunasonga mbele,” amesema Mwesigwa. 

Amesema kwamba hadi muda wa kufunga usajili jana Saa 6:00 usiku, ni timu moja tu, Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake katika mfumo huo. 
“Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili wao ndani ya muda,” amesema. 
Aidha, Mwesigwa amesema kwamba dirisha la usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 6, mwaka huu. 
“Hili dirisha la wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA, likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe hawafanyi makoasa,”amesema.  

Twiga Stars kwenda Bondeni kirafiki

http://api.ning.com/files/STHDuz-8NrUpchIxJtAG7Yhc*bs7v9f6guq0lMwxNXrwwbY8mQyceglvUwtFfk9Y9Lg8A7-*-yAlwpgOnTx01kmvHI749vQs/TWIGA.JPGKIKOSI cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya nchi hiyo (Banyana Banyana). Twiga Stars inakwenda huko kwa mwaliko wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) katika mji wa Polokwane.
Msafara wa timu hiyo utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Saloum ambapo utajumuisha wachezaji 18 na benchi la ufundi lenye watu watano.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Amina Bilali, Anastaz Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Fatuma Jawadu, Fatuma Makusanya, Fatuma Maonya, Fatuma Swaleh, Happiness Mwaipaja, Maimuna Said, Mwajuma Abdillahi, Mwanahamis Shurua, Shelda Mafuru, Sophia Mwasikili, Therese Yona na Zena Rashid.
Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Rogasian Kaijage, na msaidizi wake Nasra Mohamed. Wengine ni Christine Luambano (daktari), Furaha Mnele (Meneja) na Mwanahamisi Nyomi (mtunza vifaa). Timu hiyo inatarajia kurejea nchini Septemba 2 mwaka huu kwa ndege ya Fastjet.

Breaking News: Okwii arejea Simba kama utani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi30ecePnhZEckX89NHVLlKiHlv20Jo1JaBMTfcadNELgBqw6SY-HjetDd8JGlpJezz8znqtCdwiBagxQUz85BaW2fhh9X271wkFUhuDo05NLnVd2-N6uMfJ9eE6k8-5Iz-5Jt9REAwWNI/s1600/EMMANUEL+OKWI.JPG
Emmanuel Okwi karudi nyumbani Msimbazi
WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiongeza muda wa usajili kwa saa 48, klabu ya Simba imemrudisha kundini kiungo wao mshambuliaji, Mganda Emmanuel Okwi.
Okwi aliyekuwa akiichezea Yanga imedaiwa amekamilisha usajili wake wa kukipiga Simba na tayari jina lake ni miongoni mwa majina 29 yaliyopelekwa TFF kwa ajili ya kuombewa usajili kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza Septemba 20.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hanspope amethibitisha kumsainisha miaka miwili mshambuliaji huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Uganda The Cranes.
Kurejea kwa Okwi ndani ya Msimbazi ni kama imeirahisishia kazi Yanga iliyokuwa njia panda kuamua nani ikate jina lake kati ya nyota wake wa kigeni sita waliokuwa wapo kwenyue kikosi chao.
"Ni kweli Okwi tumemsajili kwa miaka miwili na atakuwa kwenye kikosi cha Simba kwa msimu ujao," Hanspope amenukulia akisema kwa kujiamini.
Yanga ilikuwa katika sintofahamu ya kuamua imuache nani kati ya Okwi na Jaja Brazil aliyepigiwa debe na kocha Marcio Maximo, ambaye hata hivyo uongozi ya Jangwani ulikuwa haujaridhika naye.
Hayo yakijiri TFF imeongeza siku mbili zaidi za usajili wa wachezaji wa ndani ingawa zoezi hilo lililikuwa limekamilika usiku wa jana.
Kwa usajili wa Mapro zoezi litaendelea hadi Jumamosi ijayo yaani Septemba 6.