STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 28, 2014

Afande Bright aachia mpya za Injili

Kava la albamu ya Afande Bright linavyoonekana kwa wanayoitaka wanaweza kuwasiliana kwa namba zinazoonekana chini kushoto kwenye kava hilo
Afande Bright katika pozi
MSANII aliyekuwa anakuja juu kwenye muziki wa kizazi kipya aliyejitosa kwenye muziki wa Injili baada ya kuponea chupuchupu kufa ajalini, Bright Mbwilo 'Afande Bright' ameachia albamu yake ya kwanza ya miondoko hiyo mipya iitwayo 'Ahsante Bwana'.
Akizungumza na MICHARAZO, Bright alisema albamu hiyo ambayo kwa sasa ipo sokoni wakati akijipanga kuitengenezea video yake, ina nyimbo nane.
Bright alizitaja nyimbo hizo ni 'Ahsante Bwana', 'Upendo', 'Vita', 'Hamjui', 'Itakuwaje', 'Twakuheshimu', 'Jinsi Gani' na 'Vita Remix', huku akisema karibu nyimbo zote ni simulizi la kweli zilizowahi kumpata au kuwapata watu wake wa karibu.
"Baada ya kunusurika katika ajali mjini Morogoro, nimeamua kumgeukia Mungu na sasa naimba muziki wa Injili nikiwa nimeachia albamu inayofanya vyema sokoni na kwenye vituo vya redio iitwayo 'Ahsante Bwana' yenye nyimbo nane," alisem Bright.
Aliongeza kabla ya kutumbukia kwenye muziki huo wa kumtukuza MUNGU alikuwa kiimba muziki wa kizazi kipya na aliwahi kutoa albamu moja iliyofanya vyema sokoni iitwayo 'Tanzania' iliyokuwa na nyimbo nane.
Baadhi ya nyimbo hizo ni 'Tanzania', 'Ndani ya Dancehall', 'Zako Style', 'Kiza Kinene', 'Jakaya', 'Nimedata', 'Hawapendi', 'Watanzania', 'Nikiachwa leo' na 'Leave Me Alone'.

1 comment: