STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 28, 2014

Rooney nahodha mpya England Hodgson atangaza kikosi

http://static.guim.co.uk/sys-images/SPORT/Pix/pictures/2012/6/27/1340795627494/Roy-Hodgson-008.jpg
Sasa wewe ni nahodha wa kikosi usiniangushe, Kocha Hodgson akifurahia jambo na Rooney
NYOTA wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney ametajwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Uingereza Three Stars na kocha Roy Hodgson. 
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amechukua kitambaa hicho akimrithi kiungo wa Liverpool Steven Gerrard aliyestaafu rasmi soka la kimataifa baada ya nchi hiyo kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia. 
Mshambuliaji huyo nyota amefunga mabao 40 katika mechi 95 za kimataifa na alitajwa kuwa nahodha wa United na kocha Louis van Gaal mapema mwezi huu. 
Rooney alithibitisha uteuzi huo katika mtandao wake na kudai kuwa ataitumikia nafasi hiyo kwa bidii na kujivunia huku akidai kuwa zilikuwa ndoto zake za muda mrefu. 
Rooney ataanza kuvaa beji rasmi akiwa na timu ya taifa Septemba 3 mwaka huu wakati Uingereza watakapoikaribisha Norway katika Uwanja wa Wembley kwa ajili ya mchezao wa kirafiki wa kimataifa.
Kocha huyo amekitangaza kikosi cha wachezaji wake watakaocheza mechi hiyo na ile ya kuwania kufuzu EURO 2016 dhidi ya Uswisi akiwajumuisha wachezaji wanne ambao hawajawahi kabisa kuichezea timu hiyo.
Makinda hao waliotwa katika timu hiyo ni Jack Colback, Calum Chambers, Danny Rose na Fabian Delph, huku Andros Townsend akirejeshwa kikosini tena.
 
Kikosi kamili ni kama ifuatavyo; MAKIPA: Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)
MABEKI: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Everton)
VIUNGO: Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)
WASHAMBULIAJI: Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).

No comments:

Post a Comment