STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 8, 2015

YANGA NJIA NYEUPEE, YAMZIBA MDOMO JULIO KWA 8-0

http://3.bp.blogspot.com/-0Oz18ljyqRQ/VN9iArD-TWI/AAAAAAAAHbU/MyfXP474G2c/s1600/DSC_7835.JPGNJIA nyeupe kwa Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya jioni hii kugawa dozi ya maana kwa Coastal Union, huku watetezi Azam wakilazimishwa na Mbeya City.
Yanga ikiwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam imemfunga mdomo kocha anayechinga sana, Jamhuri Kihwelu 'Julio' baada ya kupata ushindi wa mabao 8-0, huku Amissi Tambwe akifunga mabao manne na kurejea rekodi aliyoiweka msimu uliopita wakati akiwa Simba. Kipigo hicho kimekuja katika Ligi Kuu tangu Yanga ilipoifanyia Kagera Sugar mwaka 1998 ambapo Edibily Lunyamila alifunga pekee yake mabao matano.


Mabao mengi ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Simon Msuva aliyefunga mawili, Salum Telela na Kpah Sherman aliyefunga bao lake la kwanza akiwa na Yanga tangu ajiunge nayo miezi minne iliyopita.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha jumla ya pointi 43 na mabao 36 ya kufunga na kuwaacha Azam kwa pointi sita baada ya watetezi hao kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City kwenye uwanja wa Chamazi.
Kwa kufunga mabao manne, Tambwe amefikisha mabao 9 msimu huu katika Ligi Kuu wakati Msuva amezidi kumuacha mbali Didier Kavumbagu wa Azam kwa kufikisha mabao 13 dhidi ya 10 ya mpinzani wake huyo ambaye leo hakushuka dimbani katika pambano la Mbeya City.

Liverpool yamnyatia Alexandre Lecazette

http://cdn.sports.fr/images/media/football/ligue-1/scans/lyon-domine-lille-grace-a-un-triple-de-lacazette/alexandre-lacazette/12966789-1-fre-FR/Alexandre-Lacazette.jpgKLABU ya Liverpool iko tayari kuungana na vilabu vingine vya Ligi Kuu kumfukuzia nyota wa Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette katika kipindi cha majira ya kiangazi. 
Wakongwe wa Ujerumani Burussia Dortmund pia wamekuwa wakifuatilia mwenendo wake wakati Manchester City nao wamekuwa wakimkodolea macho nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 toka Novemba mwaka jana. Klabu za Chelsea, Arsenal na Tottenham Hotspurs nazo pia zimeshatuma maskauti wao kuangalia mwenendo wa mchezaji huo huku Newcastle wakiendelea kumfuatilia pamoja na kushindwa kumsajili hapo nyuma. 
Safari hii Liverpool wamejipanga kuimarisha safu yao ya ushambuliaji mapema yasije kuwakuta kama walivyomuuza Luis Suarez kwenda Barcelona na kulazimika kumnunua Mario Balotelli ambaye hata hivyo amekuwa hana msaada sana msimu huu. Baada ya Balotelli kushindwa kung’aa na Daniel Sturridge akiendelea kusumbuliwa na majeruhi huku kukiwa hakuna uhakika wa kuendelea kuwa na Raheem Sterling msimu ujao, Brendan Rodgers anahitaji kupata chaguo zaidi katika kikosi chake.

AFCON 2017 KAZI KWELI, STARS WAPEWA MISRI, NIGERIA

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/07/TAIFA1.jpg
Taifa Stars
Kombe la AFCON
SAFARI ya Taifa Stars ya Tanzania katika mchakato wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika nchini Gabon mwaka 2017, inaonekana kuwa ngumu. Hii ni baada ya  Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuipanga kundi moja la G pamoja na vigogo.
Kwa mujibu wa droo iliyofanyika jana jijini Cairo, Misri, Tanzania imepangwa kundi moja na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Misri, pia wakipewa mabingwa wa mwaka jana, Nigeria na Chad. Huku Morocco, Tunisia zilizokuwa zimefungiwa na CAF nazo zikijumuishwa katika droo hiyo.
Timu 16 zitakazopenya katika hatua hiyo ya makundi ndiyo watakaoenda Gabon kusaka ubingwa ambao kwa sasa unashikiliwa na Ivory Coast waliotwaa mapema mwaka huu kwa kuilaza Ghana.
Tanzania kwa mara ya kwanza na mwisho kufuzu fainali hizo ilikuwa mwaka 1980 wakati michuano hiyo ilipofanyika nchini Nigeria na kwa miaka zaidi ya 30 imekuwa ikisota kusaka nafasi ya kushiriki tena bila mafanikio.
Makundi ya michuano hiyo ambayo awali ilikuwa iandaliwe na Libya kabla ya hali ya machafuko ya kisiasa kuifanya ijitoe ni kama yafuatavyo;
Kundi A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
Kundi B: Madagascar, DRC, Angola, CAR
Kundi C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
Kundi D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
Kundi E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
Kundi F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
Kundi G: Nigeria, Egypt, Tanzania, Chad
Kundi H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
Kundi I: Cote d'Ivoire, Sudan, Sierra Leone, Gabon
Kundi J: Algeria, Ethiopia, Lesotho, Seychelles
Kundi K: Senegal, Niger, Nambia, Burundi
Kundi L: Guinea, Malawi, Zimbabwe, Swaziland
Kundi M: Cameroon, South Africa, Gambia, Mauritania

Ally Choki, Super Nyamwela warudi Twanga Pepeta

Luiza Mbutu akiwatambulisha Ally Choki na Super Nyamwela leo jijini juu ya kurudi kwao Twanga pepeta
MUIMBAJI nyota wa muziki wa dansi nchini, Ally Choki ametangazwa kurudi African Stars 'Twanga Pepeta' ikiwa ni miezi michache tangu bendi yake ya Extra Bongo kusambaratika.
Kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu alimtangaza Choki na Super Nyamwela kurudi tena Twanga leo mbele ya wanahabari ikiwa ni miaka michache tangu alipoihama bendi hiyo kwenda kuanzisha bend iliyokufa ya Extra Bongo.
"Tumeamua kuiboresha bendi yetu ya mama ya Twanga Pepeta na huu ni uamuzi wangu binafsi sikushurutishwa na mtu yeyote ieleweke hivyo," alisema Choki katika utambulisho huo uliofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Twanga ni bendi yangu, hakuna ubishi ni bendi ambayo nimeitumikia kwa miaka mingi sana hivyo kwa kuanzia nitatoka na kibao kiitwacho ‘Kichwa Chini’ ambacho nitaimba na Luiza ukitoa somo kwa wanaume,” alisema Choki .
Aliongeza tayari kuna nyimbo mbili zilizo tayari kufyatuliwa na kuzitaja kuwa ni ‘Usiyaogope  Maisha’ na ‘No Discuss’.
Choki alidokeza pia kuwa hana mpango wa kuasisi tena bendi kwa sababu hataki ‘stress’ kwani kumiliki bendi ni pasua kichwa.
Naye Nyamwela alisema amerudi nyumbani na yupo tayari kwa ajili ya kuchapa kazi na Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu alisema wanatarajia kuandaa onyesho maalum la utambulisho wa wakali hao Aprili 18, jijini Dar es Salaam

TFF yampongeza Tenga, kuziona Twiga, Shepolopolo buku 2

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/malinzi1.jpg
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe  waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.
Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na  kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA.

Wakati huo huo kiingilio cha kuziona timu za Twiga Stars dhidi ya Wazambia ni Sh 2000 katika pambano la marudiano ya kuwania Fainali za Soka za Wanawake Afrika. Mechi inatarajiwa kuchezwa wikiendi hii.

Monday, April 6, 2015

YANGA KWELI WANAUMEEEEEEE!

http://3.bp.blogspot.com/-rwwM0C-aX54/VNeMeNEcbvI/AAAAAAABS-s/a7HSjWSMsDg/s1600/DSC_0067.JPGYANGA kweli wanaume! Ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia kwenye michuano ya kimataifa kwa mwaka huu baada ya Azam, KMKM na Polisi Zanzibar kung'olewa mapema. Pia ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki iliyosalia kwenye michuano ya kimataifa, kadhalika ni moja ya klabu tatu pekee za ukanda wa CECAFA zilizopenya katika raundi ya pili ya michuano ya Afrika 2015.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwishoni mwa wiki kwa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, Yanga ni timu pekee ya Afrika Mashariki na Kati kusalia katika Kombe la Shirikisho, lakini ikiungana na klabu za Al Merreikh na Al Hilal za Sudan zilizopenya raundi hiyo kupitia Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Yanga ilipata nafasi hiyo ya kuvuka hatua hiyo na kukabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Watunisia wa Etoile du Sahel baada ya kuing'oa FC Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2. Mwishoni mwa wiki walitandikwa bao 1-0, lakini ushindi mnono wa mabao 5-1 katika mechi ya awali umewabeba.
Kwa mujibu wa 16 Bora iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu zilizopenya raundi ya pili katika Kombe la Shirikisho ni; Onze Créateurs ya Mali, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Djoliba ya Mali,  Hearts of Oak ya Ghana, ASO Chief ya Algeria, Club Africain ya Tunisia, Warri Wolves ya Nigeria MK Etancheite wa DR Congo, Zamalek ya Misri na FUS Rabat ya Morocco.
Nyingine ni CF Mounana ya Gabon, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Yanga ya Tanzania, Etoile du Sahel ya Tunia, Royal Leopards ya Swaziland na AS Vita ya DR Congo.
Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, zipo timu za USM Alger ya Algeria, AS Kaloum ya Guinea,
SM Sanga Balende ya DR Congo,  Al-Hilal ya Sudan, Al-Merreikh ya Sudan, Espérance de Tunis ya Tunisia, MC El Eulma ya Algeria, CS Sfaxien ya Tunisia, AC Léopards ya Congo na Smouha ya Misri.
Klabu nyingine ni Moghreb Tétouan ya Morocco, Al-Ahly ya Misri, Raja Casablanca ya Morocco, watetezi ES Sétif ya Algeria, Stade Malien ya Mali na TP Mazembe ya DR Congo.
Mechi za awali ya hatua hizo zitachezwa kati ya Aprili 17-19 na marudiano kufanyika Mei 1-3 na timu ambazo zitapenya katika Kombe la Shirikisho zitaumana na zile zitakazoangushwa katika Ligi ya Mabingwa kwa ajili ya kuwania kutinga hatua ya makundi kuanza safari ya kusaka mamilioni ya CAF.

Simba wanacheka, walipa kisasi kwa Kagera, Mtibwa hoi

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/HMB_8444.jpg
Simba katika moja ya mechi zao za Ligi Kuu msimu huu
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/KIKOSI-SIMBA-SC.jpg
WANAUMEEEE!
SIMBA wanachekaaaa! Baada ya jioni hii kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya timu ngumu ya
Kagera Sugar katika mechi ya kiporo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Simba ambayo inaendelea kuomboleza vifo vya wanachama wake wa tawi la Maendeleo maarufu
kama Simba Ukawa waliofariki kwa ajali ya gari mjini Morogoro wakati wakielekea Shinyanga
kuwahi pambano hilo pamoja na kifo cha baba wa nahodha wao msaidizi, Jonas Mkude imepumua.
Ushindi huo wa mjini Shinyanga licha ya kusaidia kulipa kisasi kwa wapinzani wao, lakini pia
imewafanya wapunguze pengo la pointi dhidi ya mabingwa watetezi Azam wanashika nafasi ya
pili.
Simba imefikisha pointi 35, moja pungufu na ilizonazo Azam ambao keshokutwa watashuka dimba
la Taifa kuvaana na Wagonga Nyundo wa Mbeya City katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabao ya washindi katika pambano hilo lililoahirishwa toka Jumamosi kutokana na uwanja wa
Kambarage kujaa maji ya mvua, yaliwekwa kimiani na Ramadhani Singano 'Messi' katika dakika ya
49 kwa shuti kali la mbali na panalti ya Ibrahim Ajibu katika dakika ya 65.
Penalti hiyo ilikuja baada ya mabeki wa Kagera kunawa mpira langoni mwao katika harakati za
kuokoa goli na Ajibu kufunga kiufundi. Kabla ya hapo Rashid Mandawa alifunga bao lake la 10
msimu huu na kumkamata Didier Kavumbagu pale aliposawazisha bao la Messi dakika ya 60.
Katika mechi ya kiporo kingine mapema leo asubuhi Mtibwa Sugar walishindwa kuhimili vishindo vya Stand United na kukubali kichapo cha bao 1-0, kikiwa ni kipigo cha pili kwao mjini Shinyanga.
Awali wiki iliyopita walicharazwa mabao 2-1 na Kagera Sugar na kwa kichapo hicho wameifanya timu hiyo waliokuwa wakiongoza Ligi kwa muda mrefu kuporomoka hadi nafasi ya 12. Nafasi moja juu ya mstari wa timu mbili za kushuka daraja msimu huu kwenda Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
 

Msimamo baada ya matokeo ya  leo ni kama ufuatavyo;

                        P   W   D     L     F      A    Pts
1. Yanga          19   12   4    3    28    11    40
2. Azam FC      18   10   6    2    25    12    36
3. Simba         21    9    8    4    27    15    35
4. Kagera        21    7    7    7    19    20    28
5. Mgambo      20    8    3    9    17    19    27
6. Ruvu           19    6    8    5    13    16    26
7.Coastal         21    5    9    7    14    15    24
8. Mbeya City   20    5    9    6    15    17    24
9. JKT Ruvu     21    6    6    9    16    20    24
10. Ndanda      21    6    6    9    18    24    24
11. Stand         20    6    6    8    15    23    24
12. Mtibwa       21    5    8    7    19    20    23
13. Polisi Moro  21    4    9    8    13    21    21
14. Prisons       19    3    11   5    14    20    20

Mechi zijazo:
KESHO JUMATANO
Azam vs Mbeya CitySunday, April 5, 2015

NI YANGA NA WATUNISIA, TP MAZEMBE YAPENYA


YAMETIMIA! Wawakilishi pekee wa Tanzania Yanga imefahamika sasa kukutana na Etoile du Sahel ya Tunisia baada ya waarabu hao kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Benfica de Luanda ya Angola katika mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho.
Etoile imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya mchezo wa kwanza nyumbani kushinda bao 1-0 na sasa watavaana na Yanga waliosonga mbele dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe ambao jana waliwacharaza bao 1-0.
Kipigo hicho cha ugenini hakikuizuia Yanga kusonga mbele kwani ilikuwa na hazina ya ushindi wa mabao 5-1 yaliyopatikana katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Mechi ya mkondo wa kwanza ya Yanga na Etoile itachezwa kati ya April 17-19 jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana mjini Tunisia wiki mbili baadaye ambapo mshindi atasubiri kucheza mchujo wa mwisho dhidi ya timu zitakazoangukia pua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye Juni tayari kwa ajili ya kutinga hatua ya makundi kuvuna mamilioni ya CAF.
Aidha TP Mazembe ya DRC imesonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya leo kushinda nyumbani 3-1 na kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 ugenini.

Friday, April 3, 2015

Yanga yaenda Zimbabwe matumaini kibao, TFF yaitilia ubani

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/yanga1.jpg
Yanga Kila la Heri katika mechi yenu ya kesho dhidi ya FC Platinum
WAKATI Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi ikiwatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika, Yanga, kikosi cha timu hiyo kimeondoka leo nchini kuelekea Zimbabwe.
Yanga wameondoka leo majira ya asubuhi kuwahi pambano lao la kesho dhidi ya FC Platinum litakalochezwa kwenye Uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
Yanga wakiwa na ari kubwa wameondoka leo nchini na kuahidi kuendelea kuwapa raha watanzania kwa kupata ushindi ugenini mbele ya wachimba madini hao wa Bulawayo.
Yanga inahitaji sare ya aina yoyote na hata kama itapoteza mechi hiyo ya marudiano chini ya mabao manne inaweza kusonga mbele kwa ajili ya raundi ya pili.
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi saba wameondoka wakisema wanaenda kupambana kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwepo miongoni mwa wawakilishi wa michuano ya kimataifa baada ya Azam, KMKM na Polisi kung'oka mapema.

Wenger, Giroud wang'ara England, watwaa tuzo

LONDON, England
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ametangazwa kuwa kocha wa mwezi wa Ligi Kuu ya England na mshambuliaji Olivier Giroud akiwa mchezaji wa mwezi.Gi

Arsenal ilishinda mecwon four successive Premier League ghi nne mfululizo za Ligi Kuu mwezi Machi, ikifunga mabao tisa na kufungwa mawili tu.

Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Giroud alifunga mara tano, wakati Newcastle ilipocheza dhidi ya Everton, QPR na  West Ham.

Hii ni mara ya 14 Wenger, mwenye umri wa miaka 65, kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi katika miaka yake 19 ya kuifundisha Arsenal.

Arsenal kwa sasa iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wakati zikiwa zimebaki mechi nane kabla ya ligi hiyo haijafikia mwisho.

Timu hiyo iko pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, ambao wana mchezo mmoja mkononi.

The Gunners itawakaribisha Liverpool iliyopo katika nafasi ya tano kwenye uwanja wa Jumamosi.

Mechi zilizobaki za Arsenal za nyumbani ni pamoja na ile dhidi ya Chelsea itakayofanyika Aprili 26 na safari ya Manchester United iliyopo katika nafasi ya nne Mei 17.

SPURS YAJIANDAA KUMTEMA ADEBAYOR

https://spursstatman.files.wordpress.com/2013/04/emmanuel-adebayor.jpgKLABU ya Tottenham Hotspurs inajipanga kumlipa Emmanuel Adebayor ili hatimaye waachane naye katika kipindi cha majira ya kiangazi. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Togo amekuwa hana namba katika kikosi cha kwanza cha Spurs, huku yeye pamoja na meneja wa timu hiyo Mauricio Pochettino wakifurahishwa na hatua hiyo pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa. 
Lakini tatizo kubwa linatarajiwa kuwa mshahara wake, kwani mshambuliaji huyo hayuko tayari kuchukua chini ya kiasi cha paundi milioni 5.2 kabla ya kuondoka. 
Hata hivyo, Spurs sasa wako tayari kulipa asilimia fulani ya mshahara wa Adebayor msimu ujao ili kuhakikisha anaondoka klabu kwao. 
Adebayor anatarajia kuingia miezi 12 ya mwisho katika mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na anatarajiwa kuwekwa sokoni kwa mkopo au kwa dili la moja kwa moja.
Kabla ya kuchemesha mshambuliaji huyo alikuwan tegemeo White Hart Lane kwa kufunga mabao muhimu, hata hivyo kazi hiyo kwa sasa inafanywa na Harry Kane.

Jennifer Mgendi andaa Tamasha la Kumshukuru Mungu

 
MIAKA 20 si mchezo, hasa katika huduma ya uimbaji. Ndivyo ambavyo mwanadada mkali wa muziki wa Injili, Jennifer Mgendi amepanga kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kufikisha umri huo katika huduma hiyo na kulihubiri Neno kwa njia ya nyimbo.
Jennifer alisema anatarajia kufanya Tamasha la Shukrani ya Miaka 20 ya Uimbaji wake siku ya uzinduzi wa video ya albamu yake mpya ya 'Wema ni Akiba'.
Muimbaji huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu, alisema uzinduzi huo utakaoenda na tamasha hilo utafanyika June 28 katika Kanisa la Dar es Salaam Calvary Temple (DCT) lililopo Tabata Shule, Dar es Salaam.
Jennifer alisema ni wajibu wake kumshukuru Mungu kwa wema aliyomfanyia katika miaka hiyo 20 akiwa ametoa albamu nane, mpya ikiwa ni 'Wema ni Akiba' aliyoiachia wiki iliyopita ikiwa na nyimbo saba.
Miongoni mwa nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni; 'Nakugonja' alioimba na Mchungaji Abiudi Misholi na 'Wema ni Akiba' ambao unasumbua hewani tangu auachie mapema mwaka huu.
"Ni lazima nimshukuru Mungu kwa ukarimu na wema wake alionifanyia kuweza kumudu ndani ya huduma ya uimbaji kwa miaka 20 nikiwa nimetoa albamu nane na filamu kadhaa," alisema Jennifer.

VUMBI LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI HII

Kagera Sugar
JKT Ruvu
Ruvu Shooting
Ndanda FC itaialika Mbeya City

Coastal wanawakaribisha vibonde Prisons-Mbeya

Simba watakuwa Shinyanga kujiuliza kwa Kagera Sugar
VUMBI la Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo sita. Minne ikichezwa kesho Jumamosi na miwili siku ya Jumapili.
Simba wanaopigana kuingia kwenye Mbili Bora wapo ugenini kukabiliana na Kagera Sugar katika mechi ya kisasi itakayochezwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Kagera iliyotoka kuifumua Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 juzi kwenye uwanja huo, imeapa kuishikisha adabu Simba ikitaka kufuata nyayo za Stand United.
Stand iliitambia Simba kwa kuilaza bao 1-0 katika mechi baina yao iliyochezwa Februari mwaka huu.
Hata hivyo Simba kupitia Msemaji wakem, Haji Manara ametamba kuwa kikosi chao kipo kamili kutoa kichapo kesho Jumamosi.
Mbali na mechi hiyo pia kesho kuna michezo miwili mitatu jijini Tanga Coastal Union watawakaribisha maafande wa Magereza, Prisons-Mbeya kwenye Uwanja wa Mkwakwani. 
Ndanda wenyewe watakuwa nyumbani mjini Mtwara kuwakaribisha Wagonga Nyundo wa Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona na maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatini huko Mlandizi, Pwani.
Jumapili Stand United watakuwa nyumbani kuialika Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage na Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
Msimamo wa Ligi hiyo unaonyesha kuwa Yanga waliopo ugenini nchinio Zimbabwe wanaongoza wakiwa na pointi 40 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 36 na Simba wanakamata nafasi ya tatu na pointi zao 32 kisha Kagera Sugar wenye pointi 28.
 MSIMAMO WA LIGI ULIVYO KWA SASA:                      P     W      D    L    F      A     Pts
1. Yanga        19    12    04   03  28    11    40
2. Azam FC    18    10    06   02  25    12    36
3. Simba        20    08    08   04  25    14    32
4. Kagera       20    07    07   06  18    18    28
5. Coastal      20    05    09   06  14    14    24
6. JKT Ruvu   20    06    06   08   16    19    24
7. Mgambo    19    07    03   09   13    19    24
8. Mtibwa      19    05    08   06   19    19    23
9. Mbeya City 19   05    08   06    14    16    23
10.Ruvu        18    05    08   05    12    16    23
11. Ndanda    20   06    05   09    17    23    23
12. Stand       19   05    06   08    14    23    21
13. Polisi Moro20   04    09   07    13    17    21
14. Prisons     18   02    11   05    13    20    17

Kiongozi Simba ainyima Simba ubingwa

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/Kikosi-cha-Simba1.jpg
Kikosi cha Simba
SIMBA iwe bingwa, nani kasema? Labda kama itakomalia kuwania nafasi ya pili, ili kupata nafasi ya uwakilishi wa michuano ya kimataifa mwakani.
Katibu Mwenezi wa zamani wa Simba, Said 'Seydou' Rubeya, aliliambia MICHARAZO kuwa, kwa Simba hii ni ngumu kuweza kutwaa ubingwa.
Seydou alisema kuwa, ni kweli Simba inafanya vema baada ya kusuasua mwanzoni mwa msimu, lakini haiwezi kurejesha taji ililolitema msimu wa 2012-2013 kwa watani zao Yanga na Azam kulinyakua msimu uliopita.
"Simba haina safu ya ushambuliaji, inamtegemea Emmanuel Okwi pekee yake, hilo ni jambo linaloiangusha timu, japo kocha Goran Kopunovic ameibadilisha mno timu kwa kipindi kifupi," alisema Seydou.
"Kwa nafasi ya pili inawezekana kama wachezaji watapambana kiume, ila kwa ubingwa siyo rahisi kwa Simba hii, ni lazima tujipange vema kwa msimu ujao ili turejeshe makali yetu za zamani," aliongeza.
Seydou aliyejiweka kando kwa masuala ya michezo, tangu aondoke uongozini  chini ya Mwenyekiti wake Hassan Dalali 'Field Marshal', aliwataka wachezaji wa Simba kuacha 'utoto' uwanjani kuisaidia timu.
Alisema baadhi ya chipukizi waliong'ara msimu uliopita wamebweteka na mara nyingi wamekuwa wakifanya utoto dimbani unaoigharimu Simba na kuwataka kuamka ili kuisaidia timu kurejesha heshima yake.

Owino ajiweka sokoni kiaina


AMEJIWEKA sokoni. Beki wa kimataifa wa Simba, Joseph Owino amesema bado hajaamua hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Akiwa ni mmoja wa nyota wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu, Owino alisema itategemea kama abaki Simba au arejee kwao Uganda.
Akaweka bayana kwamba kama itajitokeza klabu itakayompa ofa nzuri atabaki Tanzania ili kuendelea kucheza katika Ligi Kuu.
"Itategemea hapo baadaye, ila ikitokea klabu ikanipa ofa nzuri nitabaki Bongo," alisema beki huyo aliyeichezea Azam.
Kwa muda mrefu sasa, Owino amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Goran Kopunovic.
Mbali na Owino wengine wanaomaliza mikataba Msimbazi ni; Said Ndemla, William Lucian 'Gallas', kipa Ivo Mapunda, Nassor Masoud 'Chollo', Ibrahim Twaha 'Messi' na Abdallah Seseme ambaye baba yake mzazi amefichua kuwa hawezi kubaki Simba kwa vile klabu tatu za Mwadui, Kagera Sugar na Coastal Union zinamtaka na zimeanza kuzungumza naye.