STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 8, 2015

Ally Choki, Super Nyamwela warudi Twanga Pepeta

Luiza Mbutu akiwatambulisha Ally Choki na Super Nyamwela leo jijini juu ya kurudi kwao Twanga pepeta
MUIMBAJI nyota wa muziki wa dansi nchini, Ally Choki ametangazwa kurudi African Stars 'Twanga Pepeta' ikiwa ni miezi michache tangu bendi yake ya Extra Bongo kusambaratika.
Kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu alimtangaza Choki na Super Nyamwela kurudi tena Twanga leo mbele ya wanahabari ikiwa ni miaka michache tangu alipoihama bendi hiyo kwenda kuanzisha bend iliyokufa ya Extra Bongo.
"Tumeamua kuiboresha bendi yetu ya mama ya Twanga Pepeta na huu ni uamuzi wangu binafsi sikushurutishwa na mtu yeyote ieleweke hivyo," alisema Choki katika utambulisho huo uliofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Twanga ni bendi yangu, hakuna ubishi ni bendi ambayo nimeitumikia kwa miaka mingi sana hivyo kwa kuanzia nitatoka na kibao kiitwacho ‘Kichwa Chini’ ambacho nitaimba na Luiza ukitoa somo kwa wanaume,” alisema Choki .
Aliongeza tayari kuna nyimbo mbili zilizo tayari kufyatuliwa na kuzitaja kuwa ni ‘Usiyaogope  Maisha’ na ‘No Discuss’.
Choki alidokeza pia kuwa hana mpango wa kuasisi tena bendi kwa sababu hataki ‘stress’ kwani kumiliki bendi ni pasua kichwa.
Naye Nyamwela alisema amerudi nyumbani na yupo tayari kwa ajili ya kuchapa kazi na Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu alisema wanatarajia kuandaa onyesho maalum la utambulisho wa wakali hao Aprili 18, jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment