STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 15, 2015

Kagera Sugar wazipumulia Azam, Yanga

http://api.ning.com/files/cPakA0chAEyfyqjZRP3k2djpZ9GyxNW23W69D7FY4fYhsuNz2vmH6gr7yEITcci18IdnTvIgOej4xydmYu8LtJiXW0uQDhCL/16.jpg
Kagera Sugar walioifyatua JKT Ruvu
BAO pekee la dakika ya 38 lililofungwa na kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Coastal Union, Atupele Green limeiwezesha Kagera Sugar kuichapa JKT Ruvu na kuchupa hadi nafasi ya tatu ikizipumulia timu za Azam na Yanga zinazoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kagera ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Kambarage-Shinyanga baada ya kuilaza maafande hao wa JKT kwa bao 1-0.
Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa timu hiyo kwenye uwanja huo tangu walipohamia wakitokea CCM Kirumba walipokuwa wakiambulia vipigo mfululizo.
Kwa ushindi huo Kagera imefikisha pointi 21 na kushika nafasi ya tatu, pointi nne nyuma ya Azam na Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 25 ingawa timu hizo mbili zina michezo miwili mikononi zaidi ya Kagera.
Kagera wenyewe wamecheza michezo 15 wakati Azam na Yanga wamecheza mechi 13 tu ingawa katikati ya wiki hii watakuwa viwanja kucheza viporo vyao.
Simba wamechupa nafasi ya nne baada ya kuisulubu Polisi Moro mabao 2-0 uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa kufikisha pointi 20 baada ya mechi 14.
MSIMAMO LIGI KUU TZ BARA 2014-2015
                              P   W   D    L    F    A   GD  Pts
01.  Yanga              13  07  04  02  15  07  08   25
02.  Azam               13  07  04  02  22  12  10   25
03. Kagera Sugar    15  05  06  04  12  11  01   21
04. Simba               14  04  08  02  15  11  04   20
05. Mtibwa Sugar    14  04  07  03  15  14  01   19
06. Polisi Moro        15  04  07  04  12  13   -1   19
07. Coastal Union   15  04  07  04  11   10  01   19
08. JKT Ruvu          15  05  04  06  14   15  -1   19
09. Ruvu Shooting  14  05  04  05  10   11  -1   19
10. Mbeya City       14  04  05  05   09   11  -2   17
11. Ndanda Fc        15  04  04  07   13   18  -5   16
12. Stand Utd         15  03  06  06   13   18  -5   15
13. Mgambo JKT     13  04  02  07   07   15  -8   14
14. Prisons             13  01  08   04   10   12  -2  11
Wafungaji:

 8- Didier Kavumbagu(Azam)
6-
Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ame Ali (Mtibwa), Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
 

5-Danny Mrwanda (Yanga), Kipre Tchetche (Azam)
 

4- Rama Salim (Coastal),  Simon Msuva (Yanga),  Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Heri Mohammed (Stand Utd)
 

3- Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda),Frank Domayo (Azam), Malimi Busungu (Mgambo), Achidilele (Stand Utd), Atupele Green (Kagera)

Toto Afrika, Mwadui zarudi Ligi Kuu 2005-2016

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgaPRe88ZbguLMay9hq8z-MrwZbKRJuuDlKpnOd2wtCCvgsjqCFEWatffl7Dv95XsNWxsZcZutmnogqEcrMxCmWUYaFQlW7HdciyoGr9TrkJealnP3YNu3bp8bM8-sqrTXkYziW61qIkaiy/s1600/TFF+Toto+Africans.jpg
Toto Africans
http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/DSC_4165.jpg
Mwadui Shinyanga waliopanda Ligi Kuu
TIMU za Toto Africans na Mwadui Shinyanga zimeungana na timu za Majimaji-Songea na Africans Sports kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kupata ushindi katika mechi zao za kufungia msimu wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara zilizochezwa mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Toto ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora wakati Mwadui imeishindilia Burkina Faso kwa mabao 4-3 na kuungana na Majimaji Songea na Africans Sports zilizotangulia mapema kurejea ligi kuu.
Timu hizo zote nne zilizopanda daraja ziliwahi kucheza Ligi Kuu kwa nyakati tofauti, huku Majimaji na Africans Sports zikiwahi kuwa mabingwa miaka tofauti kabla ya kuporomoka hadi madaraja ya chini.

AZAM YAIFYATUA EL MERREIKH 2-0

Azam waliowapa raha Watanzania leo Chamazi
MABINGWA wa soka nchini Azam wameanza vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifumua El Merreikh ya Sudan kwa mabao 2-0 katika pambano la awali la mkondo wa kwanza lililochezwa uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Ushindi huo umekuwa siku moja tu baada ya wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Yanga, kupata ushindi kama huo dhidi ya BDF XI ya Botswana, shukrani zikienda kwa Mshambuliaji wa Kirundi, Amissi Tambwe aliyefunga mabao yote mawili katika kila kipindi jana.
Mabao ya washindi yalifungwa na Didier Kavumbagu na John Bocco Ádebayor' katika kila kipindi na kuifanya Azam kuendeleza rekodi yake katika michuano ya kimataifa kwa kutoruhusu kipigo katika uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao.
Ushindi huo pia kumeiweka Azam katika nafasi nzuri kwa mechi ya marudiano wiki mbili zijazo, inagwa Azam haipaswi kubweteka kwa ushindi huo.

Simba yaifumua Polisi na kupaa 4 Bora

Simba waliotakata Jamhuri, Morogoro
Polisi Moro walionyoolewa leo uwanja wa nyumbani
MAGOLI mawili ya kila kipindi yameiwezesha Simba kuchupa toka maeneo ya chini na kuikamata nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Polisi Moro mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri.
Goli la dakika ya 10 lililofungwa na Ibrahim Ajibu na jingine la kipindi cha pili l;a Elias Maguri aliyetumia uzembe wa kipa wa Polisi Tony Kavishe kutoka langoni bila umakini liliisaidia Simba kufikisha jumla ya pointi 20 na kukamata nafasi ya nne baada ya kitambo kirefu kulowea eneo la kati ya namba 8-10.
Katika pambano hilo, Simba iliwafunika kabisa Polisi Moro ambao ni hivi karibu ilitoka kuilaza Mbeya City waliyoinyuka Simba mabao 2-1 kabla ya kuwabana mabingwa watetezi Azam na kutoka nao sare ya 2-2.
Ushindi huo umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa Simba ambao kwa muda mrefu walikuwa hawana furaha.
Kwenye pambano hilo Simba ilimpoteza kipa wake, Ivo Mapunda baada ya kuumia macho na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Manyika Jr na kwa sasa klabu hiyo itakuwa ikianza mipango ya kuwafuata Stand United kwenye pambano lijalo mjini Shinyanga.
Katika hatua nyingine baadhi ya wanachama wanaodaiwa kuwa wa Simba Ukawa wamenaswa na POlisi mjini Morogoro baada ya kukamatwa wakitaka 'kuwanga''.

BREAKING NEWZZ! BABA WA DULLY SYKES AFARIKI DUNIA



BABA wa msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Dully Sykes, Mzee Ebby Sykes (63) amefariki dunia leo.

Kwa mujibu wa taarifa  ambazo MICHARAZO imezipata zinasema kuwa Mzee Sykes ambaye pi ni msanii wa muziki akiimba miondoko ya reggae na mingine alifariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.
Taarifa zaidi mtaletewa, ila MICHARAZO inampa pole Prince Dully Sykes na ndugu, jamaa na familia ya marehemu kwa msiba huo mzito kwa kukumbuka kuwa Kila Nafsi itaonja mauti.