STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 15, 2015

Simba yaifumua Polisi na kupaa 4 Bora

Simba waliotakata Jamhuri, Morogoro
Polisi Moro walionyoolewa leo uwanja wa nyumbani
MAGOLI mawili ya kila kipindi yameiwezesha Simba kuchupa toka maeneo ya chini na kuikamata nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Polisi Moro mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri.
Goli la dakika ya 10 lililofungwa na Ibrahim Ajibu na jingine la kipindi cha pili l;a Elias Maguri aliyetumia uzembe wa kipa wa Polisi Tony Kavishe kutoka langoni bila umakini liliisaidia Simba kufikisha jumla ya pointi 20 na kukamata nafasi ya nne baada ya kitambo kirefu kulowea eneo la kati ya namba 8-10.
Katika pambano hilo, Simba iliwafunika kabisa Polisi Moro ambao ni hivi karibu ilitoka kuilaza Mbeya City waliyoinyuka Simba mabao 2-1 kabla ya kuwabana mabingwa watetezi Azam na kutoka nao sare ya 2-2.
Ushindi huo umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa Simba ambao kwa muda mrefu walikuwa hawana furaha.
Kwenye pambano hilo Simba ilimpoteza kipa wake, Ivo Mapunda baada ya kuumia macho na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Manyika Jr na kwa sasa klabu hiyo itakuwa ikianza mipango ya kuwafuata Stand United kwenye pambano lijalo mjini Shinyanga.
Katika hatua nyingine baadhi ya wanachama wanaodaiwa kuwa wa Simba Ukawa wamenaswa na POlisi mjini Morogoro baada ya kukamatwa wakitaka 'kuwanga''.

No comments:

Post a Comment