STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 1, 2013

KUZIONA TAIFA STARS, CAMEROON BUKU TANO TU!


Kikosi cha Taifa Stars kinachotarajiwa kuivaa Cameroon Jumatano ijayo


KIINGILIO cha chini kwenye mechi ya FIFA Date kati ya Taifa Stars na Cameroon itakayochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani.
Viti vya bluu ni sh. 7,000 wakati viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000. Kwa viti vya VIP viingilio ni kama ifuatavyo; VIP C sh. 15,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohia/Samora, kituo cha mafuta OilCom Ubungo, Dar Live Mbagala na kituo cha mafuta Buguruni.

FECAFOOT YATAJA NYOTA WAKE 21, ETO’O NDANI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36 wakiwemo wachezaji 21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions) wakiongozwa na nahodha Samuel Et’oo Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT, John Ndeh.
Mbali ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.
Wengine ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono (Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).
Pia wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu), Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).
Wakati huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.

YANGA, MTIBWA SUGAR KAZI KWELIKWELI

Yanga na Mtibwa Sugar zinapambana kesho (Februari 2 mwaka huu) katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mechi iliyopita walilala mbele ya Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa ligi kwa sasa.
Polisi Morogoro itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro wakati Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa.
Keshokutwa (Jumapili) kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

VILLA SQUAD, MORO UNITED UWANJANI FDL

Villa Squad na Moro United zinaumana kesho (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoanza mzunguko wa lala salama.
Kundi A litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mechi nyingine ya Kundi B itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Kundi C ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

AJALI MBAYA: WATANO WAFA 20 WAJERUHIWA MBEYA LEO

ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKISHA MAJERUHI PAMOJA NA WATU WALIO FARIKI HOSPITALINI HAPO
 RIPOTI IKIWA INATOLEWA JUU YA AJALI HIYO HUSSEIN KIF
MMOJA YA ABIRIA WALIOKUWEMO KATIKA AJALI HIYO

AJALI MBAYA IMETOKEA MAPEMA LEO MBALALI AMBAPO LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA ILIKUWA IMEBEBA WATU ZAIDI YA MIAMBILI (200) AMBAO WALIKUWA WANAELEKEA KATIKA KITONGOJI KIMOJA CHA MWEKEZAJI .

AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI HILO LENYE NAMBA ZA USAJILI T 398 BSE KUANGUKA NA KUSABABISHA WATU 5 KUFARIKI DUNIA NA WENGINE 20 KUJERUHIWA VIBAYA.

HATA HIVYO MAJERUHI WOTE WANAKIMBIZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA ILIYOPO MBEYA MJINI MUDA HUU.

HIZI NI TAARIFA ZA AWALI TUU, HABARI NA PICHA ZOTE ZINAKUJA HAPA HAPA 

PICHA KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG

ETOO KUIONGOZA CAMEROON MBELE YA STARS JUMATANO

Nahodha wa Cameroon, Samuel Et'oo
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36 wakiwemo wachezaji 21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions) wakiongozwa na nahodha Samuel Et’oo Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT, John Ndeh.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema mbali ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.
Wengine ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono (Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).
Pia wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu), Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).

Wakati huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.

NANI KAINGIA NA KUIOKA WAPI KLABU ZA LIGI KUU ENGLAND?

Nacho Monreal - ametua Arsenal

DIRISHA dogo la usajili wa Ligi Kuu ya England la Januari lilifungwa jana usiku. hapa tunakuletea orodha kamili ya nani ameingia nani ametoka katika klabu za Ligi Kuu ya England:


ARSENAL
Aliyeingia: Nacho Monreal [Paundi milioni 10 kutoka Malaga]

Walioondoka: Johan Djourou [kwa mkopo kwenda Hannover 96], Marouane Chamakh [kwa mkopo kwenda West Ham] , Chuks Aneke [kwa mkopo kwenda Crewe], Emmanuel Frimpong [kwa mkopo kwenda Fulham]

ASTON VILLA
Aliyeingia: Yacouba Sylla [Paundi milioni 2 kutoka Clermont Foot],

Aliyeondoka: Stephen Warnock [bure kwenda Leeds]

CHELSEA

Demba Ba
 
Aliyeingia: Demba Ba [ada haitajwi, lakini inaaminika kuwa ni paundi milioni 7, akitokea Newcastle]

Walioondoka: Lucas Piazon [kwa mkopo kwenda Malaga], Sam Walker [kwa mkopo kwenda Colchester], Billy Clifford [kwa mkopo kwenda Colchester], Todd Kane [kwa mkopo kwenda Blackburn], Daniel Sturridge [kwa ada isiyotajwa, inayoaminika kuwa paundi milioni 12, kwenda Liverpool], Patrick Bamford [kwa mkopo kwenda MK Dons]

EVERTON
Aliyeingia: John Stones [Bei haitajwi, inaaminika kuwa paundi milioni 3]

Waliotoka: Ross Barkley [kwa mkopo kwenda Leeds], Anton Forrester [bure kwenda Blackburn Rovers], Magaye Gueye [kwa mkopo kwenda Brest]

FULHAM
Walioingia: Chris David [bei haitajwi kutoka FC Twente] , Emmanuel Frimpong [kwa mkopo kutoka Arsenal], Urby Emanuelson [kwa mkopo kutoka AC Milan], Stanislav Manolev [kwa mkopo kutoka PSV Eindhoven]

Walioondoka: David Stockdale [kwa mkopo kwenda Hull], Stephen Kelly [bei haitajwi kwenda Reading]

LIVERPOOL

Daniel Sturridge
 
Walioingia: Daniel Sturridge [bei haitajwi, inaaminika paundi milioni 12, kutoka Chelsea], Philippe Coutinho [paundi milioni 8.5 kutoka Inter Milan]

Walioondoka: Danny Wilson [kwa mkopo kwenda Hearts], Nuri Sahin [amerejea Real Madrid, kisha kwenda Borussia Dortmund], Joe Cole [bure kwenda West Ham], Adam Morgan [kwa mkopo kwenda Rotherham] , Alexander Doni [kwa mkopo kwenda Botafogo], Michael Ngoo [kwa mkopo kwenda Hearts]

MANCHESTER CITY

 



Aliyeingia: Godsway Donyoh [Bei haijawi]

Walioondoka: Mario Balotelli [paundi milioni 19 kwenda AC Milan], Alex Nimely [kwa mkopo kwenda Crystal Palace], Godsway Donyoh [kwa mkopo kwenda Djurgarden], Jeremy Helan [kwa mkopo kwenda Sheffield Wednesday], Reece Wabara [kwa mkopo kwenda Blackpool]

MANCHESTER UNITED

Wilfried Zaha
 
Aliyeingia: Wilfried Zaha [paundi milioni 10 + paundi milioni 5 za ziada kutoka Crystal Palace]

Walioondoka: Davide Petrucci [kwa mkopo kutoka Peterborough], Scott Wootton [kwa mkopo kwenda Peterborough], Robbie Brady [bei haitajwi, inaaminika kuwa paundi milioni 2, kwenda Hull], Angelo Henriquez [kwa mkopo kwenda Wigan], Josh King [bei haitajwi kwenda Blackburn], Luke McCullough [kwa mkopo kwenda Cheltenham], Wilfried Zaha [kwa mkopo kwenda Crystal Palace], Federico Macheda [kwa mkopo kwenda Stuttgart]

NEWCASTLE

Mapou Yanga-Mbiwa
 
Walioingia: Mathieu Debuchy [bei haitajwi, inaaminika kuwa paundi milioni 5, kutoka Lille], Kevin Mbabu [bei haitajwi kutoka Servette], Moussa Sissoko [bei haitajwi kutoka Toulouse], Massadio Haidara [bei haitajwi kutoka Nancy], Yoan Gouffran [bei haitajwi kutoka Bordeaux], Mapou Yanga-Mbiwa [bei haitajwi, inaaminika kuwa paundi milioni 6.7, kutoka Montpellier]

Walioondoka: Demba Ba [bei haitajwi, inaaminika kuwa paundi milioni 7, kwenda Chelsea], Conor Newton [kwa mkopo kwenda St Mirren], Xisco [bure kwenda Cordoba]

NORWICH
Walioingia: Luciano Becchio [kubadilishana wachezaji kutoka Leeds], Kei Kamara [kwa mkopo kutoka Sporting Kansas City]

Walioondoka: Jacob Butterfield [kwa mkopo kwenda Crystal Palace], Elliott Ward [kwa mkopo kwenda Nottingham Forest] , Steve Morison [kubadilishana wachezaji kwenda Leeds], Declan Rudd [kwa mkopo kwenda Preston]

QPR

Loic Remy
Christopher Samba
 
Walioingia: Loic Remy [bei haitajwi, inaaminika kuwa paundi milioni 8, kutoka Marseille], Tal Ben Haim [haijaambatanishwa], Christopher Samba [paundi milioni 12.5 kutoka Anzhi Makhachkala], Yun Suk-young [bei haitajwi kutoka Chunnam Dragons], Jermaine Jenas [bei haitajwi kutoka Tottenham], Andros Townsend [mkopo kutoka Tottenham]

Walioondoka: Djibril Cisse [kwa mkopo kwenda Al Gharafa], Anton Ferdinand [kwa mkopo kwenda Bursaspor], Frankie Sutherland [kwa mkopo kwenda Portsmouth], Michael Harriman [kwa mkopo kwenda Wycombe], Alejandro Faurlin [kwa mkopo kwenda Palermo], Michael Doughty [kwa mkopo kwenda St Johnstone], Jordan Gibbons [kwa mkopo kwenda Inverness CT], Rob Hulse [kwa mkopo kwenda Millwall],

READING
Walioingia: Stephen Kelly [bei haitajwi kutoka Fulham], Hope Akpan [bei haitajwi kutoka Crawley], Nick Blackman [bei haitajwi kutoka Sheffield United]

Walioondoka: Gozie Ugwu [kwa mkopo kwenda Plymouth], Dominic Samuel [kwa mkopo kwenda Colchester], Jordan Obita [kwa mkopo kwenda Oldham], Michael Hector [Anton Ferdinand [kwa mkopo kwenda Bursaspor] 

SOUTHAMPTON
Walioingia: Vegard Forren [bei haitajwi kutoka Molde]

Walioondoka: Dan Seaborne [kwa mkopo kwenda  Bournemouth], Ryan Dickson [kwa mkopo kwenda  Bradford], Sam Hoskins [kwa mkopo kwenda Stevenage], Jonathan Forte [kwa mkopo kwenda Sheffield United], Steve de Ridder [kwa mkopo kwenda Bolton]

STOKE
Walioingia: Jack Butland [paundi milioni 3.5 kutoka Birmingham], Brek Shea [paundi milioni 2.5 kutoka FC Dallas]

Walioondoka: Michael Tonge [bei haitajwi kwenda Leeds], Danny Higginbotham [bur kwenda Sheffield United], Rory Delap [kwa mkopo kwenda Barnsley], Ryan Brunt [bei haitajwi kwenda Bristol Rovers], Jack Butland [kwa mkopo kwenda Birmingham], Matthew Upson [kwa mkopo kwenda Brighton]

SUNDERLAND
Walioingia: Kader Mangane [kwa mkopo kutoka Al Hilal], Alfred N'Diaye [bei haitajwi kutoka Bursaspor], Danny Graham [paundi milioni 5 kutoka Swansea]

Walioondoka: Blair Adams [bei haitajwi kwenda Coventry], David Meyler [bei haitajwi, inaaminika kuwa paundi milioni 1.5, kwenda Hull], Ahmed Elmohamady [kwa mkopo kwenda Hull City], Jonny Maddison [loan to Crawley], Fraizer Campbell [undisclosed, believed to be £650,000, to Cardiff City]

SWANSEA
Walioingia: Hamna

Walioondoka: Jamie Proctor [bei haitajwi kwenda Crawley], Danny Graham [paundi milioni 5 kwenda Sunderland], Curtis Obeng [kwa mkopo kwenda York City], Leroy Lita [kwa mkopo kwenda Sheffield Wednesday], Ashley Richards [kwa mkopo kwenda Crystal Palace] , Gwion Edwards [kwa mkopo kwenda St Johnstone]

TOTTENHAM

Heurelho Gomes
 
Walioingia: Lewis Holtby [imeripotiwa paundi milioni 1.5 kutoka Schalke], Zeki Fryers [paundi milioni 3 kutoka Standard Liege]

Walioondoka: Heurelho Gomes [kwa mkopo kwenda Hoffenheim], Alex Pritchard [kwa mkopo kwenda Peterborough], Jermaine Jenas [bei haitajwi kwenda QPR], Andros Townsend [kwa mkopo kwenda QPR]

WEST BROM
Walioingia: Hamna

Walioondoka: Sam Mantom [bure kwenda to Walsall], Gonzalo Jara [kwa mkopo kwenda Nottingham Forest], Chris Wood [bei haitajwi, inaaminika paundi milioni 1, kwenda Leicester], Craig Dawson [kwa mkopo kwenda Bolton]

WEST HAM

Marouane Chamakh
 
Walioingia: Wellington Paulista [kwa mkopo kutoka  Cruzeiro], Marouane Chamakh [kwa mkopo kutoka Arsenal], Joe Cole [bure kutoka Liverpool], Sean Maguire [bei haitajwi kutoka Waterford United]

Walioondoka: Alou Diarra [kwa mkopo kwenda Rennes]

WIGAN
Walioingia: Joel Robles [kwa mkopo kutoka Atletico Madrid], Roger Espinoza [bure kutoka Sporting Kansas City], Angelo Henriquez [kwa mkopo kutoka  Manchester United], Paul Scharner [kwa mkopo kutoka Hamburg]

Walioondoka: Rob Kiernan [kwa mkopo kwenda Brentford] , Mauro Boselli [kwa mkopo kwenda Palermo] 

CHANZO:STRIKAMKALI
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za TASWA, Haji Manara

TUZO ZA WACHEZAJI BORA ZA TASWA KUFANYIKA APRILI 27


TUZO za Wanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2012 zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitafanyika Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za TASWA, Haji Manara, kamati hiyo ilifanya kikao chake cha kwanza Jumanne wiki hii, ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikubaliana mambo mbalimbali ya kimsingi kuhakikisha tuzo zinakuwa na mvuto kama ilivyokuwa miaka iliyopita na pengine ziwe bora zaidi.

Kutokana na hali hiyo vyama vyote vya michezo vilivyosajiliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambavyo vipo hai na vinaendesha mashindano vitaandikiwa barua kwa ajili ya kutoa mependekezo yao ya wanamichezo waliofanya vizuri kwa mwaka jana upande wa michezo yao na yawasilishwe kabla ya Februari 28, mwaka huu.

"Tunaomba ieleweke kuwa vyama vitatoa mapendekezo na hivi sasa Kamati ya Tuzo inafanya mazungumzo na kampuni mbalimbali zinazohusika na mambo ya mawasiliano ili kuona namna zitakavyoshirikiana na wadau katika kuchambua majina hayo, ambapo kila chama kimetakiwa kiwasilishe majina matano ya wanamichezo wao kwa kila jinsia kama ni mchezo unaochezwa na jinsia mbili, lakini kama ni mchezo wa jinsia moja watatakiwa kuwasilisha majina matano ya jinsia husika tu," alisema Manara.

Aliongeza kuwa kuna marekebisho kadhaa yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya tuzo kutoka 36 za mwaka jana hadi kufikia 42 mwaka huu na idadi inaweza kuongezeka ama kupungua kulingana na sifa za wanamichezo ambazo vyama vitaleta.

"Tunaomba wadau watupe ushirikiano wa kutosha katika jambo hili ili kuzifanya tuzo ziwe bora na kuhakikisha kila anayestahili kupata tuzo anazawadiwa kwa kuthamini kile alichokifanya, ambapo ukumbi utakapofanyika tuzo hizo utatangazwa hivi karibuni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.

"Idadi ya michezo itakayopewa tuzo pamoja na aina nyingine ya tuzo zitakazotolewa ikiwamo Tuzo ya Heshima tutaendelea kujulishana kadri siku zitakavyokuwa zinasonga mbele. Washindi wa kila tuzo ndiyo mmojawapo ataibuka kuwa Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2012.

"Dhamira ya kamati yangu ni kutaka kuhakikisha kuwa TASWA haikukosea kututeua na tutaleta wanammichezo sahihi na hatimaye kumpata yule bora ambaye ataungana na wengine waliopata kutwaa tuzo hiyo miaka ya nyuma," alisema.

Wanamichezo ambao wamepata kutwaa Tuzo ya Mwanamichezo Bora Mwaka wa Tanzania ni Samson Ramadhan (2006),  Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wakiwa wanariadha, wakati mwaka 2009 alikuwa Mwanaidi Hassan na mwaka 2010 alikuwa pia Mwanaidi Hassan ambaye ni mcheza netiboli na mwaka 2011 alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe.

Zahoro Pazi akwama 'bondeni' Mzimbabwe amzidi kete Bloemfotein Celtic

Pazi (kulia) alipokuwa Azam kwenye mazoezi ya timu hiyo


MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu za Mtibwa na Azam aliyetua JKT Ruvu kwa mkopo, Zahoro Pazi, amekwama kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini alipoenda kujaribiwa kwa siku 10 katika klabu ya Ligi Kuu ya Bloemfotein Celtic.
Akizungumza na NIPASHE, Pazi aliyerejea usiku wa kuamkia jana alisema kuwa pamoja na kufanya vema majaribio yake amekwama kunyakuliwa na timu hiyo kutokana na kuwepo kwa nafasi mmoja tu ya mchezaji aliyehitajiwa na klabu hiyo.
Pazi, alisema mchezaji aliyemzidi kete ni mshambuliaji kutoka nchini Mzimbabwe, ambaye walikuwa wakifanyiwa majaribio kwa pamoja nchini humo.
"Kaka nimerejea usiku wa kuamkia leo baada ya majaribuo yangu ya siku 10 ambapo bahati haikuwa kwangu baada ya Mzimbabwe kunizidi kete kwa sababu nafasi iliyokuwa inawania kuwa moja," alisema Pazi.
Mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Idd Pazi 'Father' alisema pamoja na ndoto zake za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kukwama, hajakata tamaa kutokana na kumwagiwa sifa na kocha mkuu watimu hiyo, Clinton Larsen aliyevutiwa naye.
"Sijakata tamaa kwa sababu nashukuru sikuharibu katika majaribio yangu, tatizo nafasi ilikuwa moja na alihitajika mshambuliaji wakati mie nilienda kule kama winga, na kocha wa klabu hiyo alionekana kuvutiwa nami hivyo nadhani safari bado ipo," alisema Pazi.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kujaribiwa katika klabu iliyowahi kutamba kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, Kaiserlauten, alisema kurejea kwake kunamfanya aungane na kikosi cha wana JKT kuendelea na Ligi ya nyumbani ambako kesho timu hiyo itaivaa Simba.

Mwisho

ATLETICO MADRID YAJIWEKA PAZURI, YAILAZA SEVILLA

Wachezaji wa Atletico Madrid na Sevilla wakichuana usiku wa kuamkia leo katika nusu fainali ya Koimbe la Mfalme nchini Hispania
TIMU ya soka ya Atletico Madrid usiku wa kuakia leo (Februari 1) ilijiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu fainali za Kombe la Mfalme nchini Hispania baada ya kuilaza Sevilla mabao 2-1 katika nusu fainali ya michuano hiyo.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Atletico wa Vicente Calderon mjini Madrid na kuhudhuriwa na watazamaji 45,000 ilishuhudiwa magoli yote yakifungwa kwa penati.
Mikwaju miwili ya penati iliyotumbukizwa katika dakika ya 50 na 71 na Diego Costa na moja la dakika ya 56 la Alvaro Negredo wa Sevilla yaliweza kutoa matokeo ya mechi hiyo iliyokuwa kali.
Pia katika mechi hiyo ya jana ilishuhudiwa kadi nyekundu tatu zikitolewa kwa wachezaji watatu, mmoja wa Madrid na wawili wa Sevilla baada ya kuonyeshwa kadi za njano awali.
Sasa Atletico itasubiri mpaka baada ya pambano lao la marudiano na wapinzani wao watakaokuwa nyumbani Februari 27 kujua hatma yao ya kucheza fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya wapinzani wa jadi Barcelona na Real Madrid zilizotoshana nguvu juzi kwa kufungana bao 1-1 kwa ajili ya fainali ya michuano hiyo.
Fainali hizo zinatarajiwa kuchezwa  
wenyeji walisubiri hadi kipindi cha pili kujihakikishia ushindi huo.

EPL kuendelea kesho, Jumapili ni vita ya Man City dhidi ya Liverpool

KITATANGE cha Ligi Kuu ya England kinatarajiwa kuendelea kesho kwa mechi kadhaa za ligi hiyo, lakini macho ya mashabiki yakielekezwa kwenye pambano la Jumapili kati ya Mabingwa watetezi Manchester City dhidi ya Liverpool.
Mechi zitakazochezwa kesho ni QPR dhidi ya Norwich City, huku Arsenal itavaana na Stoke City, wakati Everton itakuwa nyumbani kuumana na Aston Villa.
Mapambano mengine ya ligi hiyo kesho ni kati ya Newcastle United dhidi ya Chelsea, huku Reading itakwaruzana na Sunderland na West Ham United itavaana na Swansea City.
Michezo mingine ya kesho ni kati ya Wigan Athletic itakaoikaribisha Southampton na Fulham itakuwa uwanja wa nyumbani kuwaalika vinara Manchester United.
Mbali na pambano la Jumapili kati ya Liverpool itakayoalikwa ugenini uwanja wa Al Itihad dhidi ya watetezi Manchester City, siku hiyo pia kutakuwa na mechi nyingine kati ya West Bromwich itakayoialika Tottenham Hotspur.

Kampira awasihi wapiga kura uchaguzi mkuu wa TFF

Ramadhani Kampira


ALIYEWAHI kuwa mchezaji wa soka wa Yanga na TAMCO Kibaha, Ramadhani Kampira amewakumbusha wapiga kura watakaoshiriki uchaguzi mkuu wa TFF, kuwachagua viongozi watakaouendeleza mchezo huo kama alivyokuwa Leodger Tenga.
Aidha amewasihi wapiga kura wasije wakachagua kiongozi kwa uwezo wake kifedha au ahadi tamu bali wawasikilize kwenye kampeni sera na mipango yao yenye tija kwa soka la Tanzania ambalo alidai linahitaji ukombozi kuinuka mahali lilipo.
Kampira, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka wilaya ya Kinondoni, alisema wapiga kura wa TFF wanapaswa kutambua kuwa soka la Tanzania linahitaji viongozi wenye uchungu wa kweli wa mchezo huo kama alivyokuwa Tenga aliyemwagia sifa.
"Nilikuwa nawaomba wapiga kura wa TFF, kuhakikisha wanawachagua viongozi wwenye uchungu wa kweli na soka la Tanzania ili kuendeleza pale alipopaacha Tenga, kosa lolote watakalofanya wapiga kura hao wataurudisha tulipotoka," alisema Kampira.
Kampira aliongeza mara baada ya kuanza kwa kampeni, wapiga kura wanapaswa kuzisikiliza sera na mipango ya wagombe na kuzipima kabla ya kuwapigia kura wale ambao wanaona wanafaa kuliongoza shirikisho hilo.
Alisema itakuwa kosa kubwa kama wapiga kura hao wataamua kuwaangalia au kuwapima wagombea kwa umahiri wao wa kuzungumza na kutoa ahadi sawia na uwezo wao kifedha bila kujali kama watakuja kuliangamiza soka la Tanzania.
"Wapiga kura wasiangalie uwezo wa kifedha za wagombea, bali wachague viongozi ambao watalitoa soka la Tanzania kutoka mahali lililpo hadi kwenye maendeleo ya kweli," alisema.
Uchaguzi mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika Februari 24 jijini Dar es Salaam ambapo mrithi wa Tenga na viongozi wengine ndani ya shirikisho hilo watafahamika rasmi.

DURU LA LALA SALAMA FDL KUANZA KESHO NCHINI


KIVUMBI cha Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) duru la pili kinatarajiwa kuanza kutimka rasmi leo kwenye viwanja tisa tofauti nchini.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mapema wiki hii na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kivumbi cha ligi hiyo kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, kitahusisha timu 18 kati ya 24 zinazoshiriki michuano hiyo.
Ratiba hiyo inaoonyesha kuwa kundi A litakuwa na mechi tatu ambapo Mbeya City ya Mbeya itakayoikaribisha timu ya Burkina Faso ya Morogoro kwenye uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya, Majimaji-Songea dhidi ya Kurugenzi Lindi mechi itakayochezwa uwanja wa Majimaji, Ruvuma na Polisi Iringa kuivaa Mkamba Rangers ya Morogoro uwanja wa Samora, Iringa.
Kundi B litakuwa na mechi mbili tu kati Transit Camp dhidi ya Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini, Pwani na Moro United itaumana na Villa Squad uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mechi nne zitapigwa kwa timu za kundi C ambapo Polisi Dodoma na Kanembwa JKT zitaumana Jamhuri, Dodoma), Morani itaumana na Mwadui mjini Kiteto-Manyara, Polisi Mara dhidi ya Pamba mjini Musoma na Polisi Tabora na Rhino Rangers wataumana uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa mechi za kundi B ambapo Tessema ya Temeke itavaana na Green Warriors ya Kinondoni kwenye uwanja wa Mabatini-Pwani na Ashanti United itaavana na 'Vijana wa Kova' Polisi Dar kwenye uwanja wa Karume Dar.
Ligi hiyo imepangwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo kila mshindi wa kwanza wa kundi atafuzu moja kwa moja kwa Ligi Kuu msimu wa 2013-2014.

VUMBI LA LIGI KUU BARA KUENDELEA KESHO



Aliyekuwa kocha wa Yanga, Tom Saintfiet aliposhuhudia kipigo cha Mtibwa kabla ya kutimuliwa.

Wachezaji wa Yanga na Mtibwa walipokuwa wajiandaa kuumana katika duru la kwanza ambapo Yanga ililala mabao 3-0
KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania bara kinatarajiwa kuendelea tena kesho kwa michezo mitatu, ambapoi vinara Yanga watakuwa dimba la Taifa, Dar es Salaam kujaribu kulipiza kisasi kwa Mtibwa Sugar.
Yanga ilinyukwa mabao 3-0 na Mtibwa katika pambano lao la duru la kwanza, hivyo itashuka dimbani kesho kwa nia ya kuendeleza wimbi la ushindi sambamba na kulipa kisasi cha mabao hayo.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, waliokuwa ughaibuni nchini Uturuki kujiandaa na duru hilo la pili, imetamba kuwa kesho ni zamu yao ya kucheka mbele ya Mtibwa.
Mechi nyingine za kesho ni katio ya Polisi Moro iliyopo mkiani mwa msimamo itakayovaana na African Lyon, mjini Morogoro na Mgambo JKT ya Tanga yenyewe itakuwa dimba la Mkwakwani kuvaana na Ruvu Shooting.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba wenyewe watashuka dimbani Jumapili kwa kuvaana na  JKT Ruvu, huku Coastal Union ya Tanga itaialika Prisons ya Mbeya uwanja wa Mkwakwani.
Mpaka sasa Yanga ndio wanaoongoza msimamo wakiwa na piointi 32 wakifuatiwa na Azam kisha Simba zilizopo nafasi ya pili na tatu.

Mshindi Tigo kushuhudia marudiano Barca, Real



Meneja Ubunifu na Ofa wa TIGO, David Sekwao (kati) akizungumza na mshindi wa promosheni yao ya 'Smartcard' jana
JULIUS Kanza, mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi wa droo ya promosheni ya ‘smartcard’ na hivyo kupata zawadi ya kugharimiwa usafiri, malazi, chakula na tiketi ya kwenda kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Mfalme itakayowakutanisha vigogo Real Madrid na Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Mechi hiyo itachezwa Februari 27 ambapo Kanza atakuwa ni miongoni mwa mashabiki takriban 100,000 watakaofurika uwanjani kushuhudia pambano hilo ambalo litakuwa na msisimko zaidi baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Meneja wa ubunifu wa ofa za Tigo, David Sekwao, ndiye aliyemtangaza mshindi wakati akizungumzia promosheni hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Sekwao alisema kuwa droo hiyo ilizinduliwa mwaka jana kwa ajili ya wateja wao, na hasa wanaotumia simu za Blackberry, Android na iphone.
“Droo hizi zinaendelea kufanyika kila mwezi, robo mwaka, na kila mwaka,” alisema Sekwao, huku akitaja zawadi nyingine mbalimbali kuhusiana na droo hiyo, zikwiamo za vocha za kununulia bidhaa mbalimbali, tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai na malazi ya siku 5, na vilevile tiketi na gharama za kwenda na kurudi Uingereza kuangalia ‘live’ mechi ya ligi kuu kati ya Arsenal na Man U itakayochezwa Aprili mwaka huu.
Alisema washindi hupatikana kwa njia ya kujibu  maswali yanayoulizwa kwa washiriki kupitia simu zao.



Chamoyo, Man Bizo wana mpya

Cha Moyo akiwa katika pozi zake za 'kiteja'

Man Bizzo katika pozi


WACHEKESHAJI wanaotamba kupitia kipindi cha 'Vituko Show', Abdallah Soud 'Cha Moyo' na Ally Boffu 'Man Bizo' wapo mbioni kuachia wimbo wao mpya wa pamoja uitwayo 'Ma Mjengo'.
Kibao hicho kinafuatia baada ya wasanii hao kuachia wimbo mwingine unaoendelea kutamba katika vituo vya redio na televisheni cha 'Mamido'.
Akizungumza na MICHARAZO, Cha Moyo, anayeigiza kama 'teja' lisema wimbo huo mpya umekamilika na kwa sasa wanafanya mipango ya kuusambaza ili urushwe hewani.
Cha Moyo alisema wimbo huo wa 'Ma Mjengo' ni miongoni mwa nyimbo 10 zitakazokuwa katika albamu yao waliyopanga kuitoa mwaka huu itakayofahamika kwa jina la 'Tufe Sote'.
Msanii huyo alisema wamepanga kuachia wimbo mmoja mmoja kuitambulisha albamu hiyo kabla ya kuitoa hadharani sambamba na video yake.
"Baada ya 'Mamido' kwa sasa mie na Man Bizo' tunajiandaa kuitoa hadharani wimbo wetu mwingine uitwao 'Ma Mjengo' ikiwa ni maandalizi ya kupakua albamu kamili itakayokuwa na nyimbo 10 itakayofahamika kama 'Tufe Sote'," alisema Cha Moyo.
Cha Moyo alisema wakati wakiwa katika harakati za kufyatua albamu hiyo, pia wao na wasanii wengine wa kundi lao wanaendelea kuandaa filamu za komedi katika utaratibu wa kuwapa raha mashabiki wao.

Mwisho

Afande Sele amvulia kofia ROMA

ROMA

Afande Sele akitumbuiza mashabiki


MKONGWE wa muziki wa Hip Hop nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele' amemvulia kofia msanii anayetisha kwa sasa katika miondoko hiyo, Roma Mkatoliki akidai ndiye 'mfalme' kwa sasa kwa umahiri wake wa kuandika nyimbo zake.
Afande Sele, pia amemuunga mkono msanii huyo kupitia wimbo wake wa 2030 juu ya mistari iliyomchana Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Joseph Mbilinyi 'Mr II' akidai kuna dalili za wazi 'mheshimiwa' huyo amewatupa wasanii walioahidi kuwapigania.
Akizungumza na MICHARAZO, mkongwe huyo alisema ukali wa ROMA unampa faraja kubwa ya kuhisi kwamba warithi wamepatikana kuendeleza hip hop, akimfagilia kwa umahiri wake wa kuitunga nyimbo zinazoelezea matatizo ya wananchi walio wengi.
"Kwa kweli kwa sasa namkubali mno Roma ni mmoja wa wasanii wakali wa Hip hop hasa mashairi yake, na sioni sababu ya kusakamwa na Mr II kwa namna alivyodokeza ukweli kwenye wimbo wake wa 2030," alisema Afande Sele.
Aliongeza kuwa katika muziki wa kizazi kipya nchini kuna usaliti mkubwa hali ambayo inamfanya sasa kuamua kupumzika kwa muda na kujikita kwenye masuala ya filamu.
"Bongofleva hatuna umoja, usaliti na kugeukana na vitu vya kawaida kaka, naona bora nijikite kenye filamu kwani kule kuna aina fulani na umoja na mshikamano wa kweli," alisema.
Msanii huyo alisema wakati akienda mapumziko tayari ameshaachia kazi zake mbili za 'Amani na Upendo' na 'Soma Ule' zinazoendelea kutamba kwenye vituo mbalimbali nchini kwa sasa.

DIAMOND ANASA KWA PENNY WA DTV?




 
Hauwezi kupita mwezi bila kuibuka kitu kitakachomfanya aandikwe tena na tena. 
Katika picha iliyowekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa msichana aitwaye Skyner Ally kuna picha inayomuonesha Diamond akiwa amelala usingizi wa pono na msichana anayedaiwa kuwa ni mtangazaji wa DTV, Penny Mungilwa aka Vj Penny.

Picha hii inajieleza yenyewe kwa pozi walilolaa kuwa ni wapenzi ama ni one night stand?
Hata hivyo tulipowasiliana na Penny alisema hiyo ni picha iliyopigwa walipokuwa kwenye scene ya movie wanayoigiza pamoja ambayo amesema hana uhakika lini itatoka!

Penny na Diamond ndani ya movie?????...!!? Ngoja tuisubiri hiyo movie

SIKWENDA UINGEREZA KUUZA SURA...!-IRENE WOYA





MSANII mahiri wa filamu Irene Uwoya, ameamua kuweka wazi kuwa safari yake aliyowahi kuifanya ya nchini Uingereza mwaka jana kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya filamu ya kimataifa bado hayajazaa na matunda na hadi sasa wapo kwenye mazungumzo.

Kauli ya msanii huyo ilimfanya mwandishi wetu amdadisi zaidi, ambapo alisema kuwa kwa sasa kitu wanachokizungumzia ni namna watakavyoandika story ingawa hakutaka kuweka wazi ni story ya namna gani.

Hata hivyo alisema kuwa bado hawajafikia mazungumzo ya kulipwa kiasi gani na lini watafanya lakini anaamini kila kitu kitakuwa safi kwani watu hao wameonesha nia ya kufanya nae kazi.

Pamoja na hayo alishindwa kuwaweka wazi watu hao hata kwa kuwataja majina, kwa madai kuwa kwa sasa siyo wakati wake kwani muda ukifika mashabiki wake watajua anaenda kufanya kazi na kampuni gani.

“Bado tunaendelea na mazungumzo.Sikuenda huko kuuza sura .Najua watu wanasubiri kuona ukweli juu ya maneno yangu haya lakini nachotaka kusema ni kwamba ni kweli nilienda kwa ajili ya mazungumzo ila bado mambo hayajakaa sawa,” alisema Uwoya

BECKHAM KUKIPUTA BURE PSG, MSHAHARA WAKE KUSAIDIA JAMII

Mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England David Beckham amesaini mkataba wa miezi mitano kuichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Katika kuonyesha uhamisho haukusababishwa na pesa kama kivutio David Beckham amesema mshahara wake wote wa £150,000 kwa wiki katika kipindi chote cha mkataba wake zitaenda kusaidia jamii watoto wasiojiweza huko jijini Paris Ufaransa.

Beckham amepewa jezi namba 32.
http://www.dailymotion.com/video/xky9un_live-psg-tv_sport
 
CHINI NI BADHI YA USAJILI ULIOKAMILIKA KABLA YA USIKU WA JANA
1.Mario Balotelli (Man City to AC Milan, £19.5m),
2.Luciano Becchio (Leeds to Norwich, swap)
3.Urby Emanuelson (AC Milan to Fulham, loan),
4. Alejandro Faurlin (QPR to Palermo, loan),
5.Danny Graham (Swansea to Sunderland, £5m)
6.Steve Morison (Norwich to Leeds, swap),
7.Christopher Samba (Anzhi to QPR, £12.5m),
8.Paul Scharner (Hamburg to Wigan, loan),
9.Kieron Dyer (released by QPR to Middlesbrough)

MANSU-LI KUVUNJA UKIMYA JUMAPILI SUN CIRRO