STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 1, 2013

Afande Sele amvulia kofia ROMA

ROMA

Afande Sele akitumbuiza mashabiki


MKONGWE wa muziki wa Hip Hop nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele' amemvulia kofia msanii anayetisha kwa sasa katika miondoko hiyo, Roma Mkatoliki akidai ndiye 'mfalme' kwa sasa kwa umahiri wake wa kuandika nyimbo zake.
Afande Sele, pia amemuunga mkono msanii huyo kupitia wimbo wake wa 2030 juu ya mistari iliyomchana Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Joseph Mbilinyi 'Mr II' akidai kuna dalili za wazi 'mheshimiwa' huyo amewatupa wasanii walioahidi kuwapigania.
Akizungumza na MICHARAZO, mkongwe huyo alisema ukali wa ROMA unampa faraja kubwa ya kuhisi kwamba warithi wamepatikana kuendeleza hip hop, akimfagilia kwa umahiri wake wa kuitunga nyimbo zinazoelezea matatizo ya wananchi walio wengi.
"Kwa kweli kwa sasa namkubali mno Roma ni mmoja wa wasanii wakali wa Hip hop hasa mashairi yake, na sioni sababu ya kusakamwa na Mr II kwa namna alivyodokeza ukweli kwenye wimbo wake wa 2030," alisema Afande Sele.
Aliongeza kuwa katika muziki wa kizazi kipya nchini kuna usaliti mkubwa hali ambayo inamfanya sasa kuamua kupumzika kwa muda na kujikita kwenye masuala ya filamu.
"Bongofleva hatuna umoja, usaliti na kugeukana na vitu vya kawaida kaka, naona bora nijikite kenye filamu kwani kule kuna aina fulani na umoja na mshikamano wa kweli," alisema.
Msanii huyo alisema wakati akienda mapumziko tayari ameshaachia kazi zake mbili za 'Amani na Upendo' na 'Soma Ule' zinazoendelea kutamba kwenye vituo mbalimbali nchini kwa sasa.

No comments:

Post a Comment